Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MHE. MARTHA MARIKI - WANANCHI WA KATAVI WAMSHUKURU RAIS SAMIA KWA HUDUMA YA MAJI
Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi Martha Mariki ameishukuru serikali kwa kuwaletea Huduma ya Maji safi na Salama wa kazi wa Kata ya Mwamkulu Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi.
Mhe. Martha Mariki Akiwa katika ziara ya kutembelea Kata zote za Mkoa wa Katavi amefika na kujionea namna mradi huo unavyo wasaidia wananchi kupata huduma ya Maji kwa uhakika tofauti na hapo siku za nyuma ambapo wananchi walikuwa wanatumia Maji ambayo si safi na salama.
"Sisi kama wananchi wa Mkoa wa Katavi mimi kama mwakilishi wa kundi la wanawake na mwakilishi wa wananchi wa mkoa wa Katavi nasema naishukuru sana serikali yetu kutuletea mradi huu wa Maji wenye thamani ya Milioni 400.73 tunasema asante sana mama wananchi wa Mwamkulu wanasema asante kwa mradi huu" - Mhe. Martha Mariki
"Nashukuru Ruwasa Mkoa wa Katavi kwa namna ambavyo wameweza kusimamia mradi huu kuhakikisha mradi huu umetekelezeka kwa wakati na wananchi wa Mwamkulu wameweza kupata maji" - Mhe. Martha Mariki
Amesema kuwa kazi ya serikali nikuhakikisha inawaletea wananchi wake Maendeleo yanayo onekana kwa macho hivyo upatikanaji wa huduma hiyo ya maji ni sehemu ya serikali kutekeleza wajibu wake kwa msukumo wa uwakilishi wa wabunge bungeni kusemea changamoto husika na serikali kutekeleza kwa vitendo.