Yesu Anakuja
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 12,675
- 25,924
Si ukute kule watu hawanywi sana chai/hawatumii sana sukari kwasababu ya umasikini uliokithiri. Malawi ni masikini kupita kiasi ukilinganisha na TZ. Hata Zambia, sukari ni bei chee sana. Shida ya Bongo sema ni kodi, na pia wazalishaji wa sukari wanayo ile monopolization, wanaweza kuzuia kuuza sukari ili uwepo uhaba bei ipande wao wapige pesa ndefu zaidi na hiyo huwa wanakuwa wamekula deal na viongozi ili uhaba wa sukari ukiwepo milango isifunguliwe. Kwasababu kama TZ kuna uhaba, jiulize kwanini ukinunua sukari Malawi au Zambia kuingiza hapa unakamatwa? Kwanini ukileta sukari toka Uganda na Kenya unakamatwa? Kwasababu tunalazimishwa kununua sukari iliyopandishwa bei ili wenye viwanda wapate faida mara mbili yake, na viongozi husika wana mgao wao kwenye ile faida. Tusemeje sasa?Nchi ndogo ya Malawi iliyojaa akili nyingi kwa miaka mingi haijawahi kukumbwa na Uhaba wa sukari , Balo mara zote inazidiwa na sukari kiasi cha kuruhusu ivushwe Tanzania ili kuokoa Uhaba wa sukari wa nchi hiyo duni .
Haya malalamiko yenu kuhusu Uhaba wa sukari , Kyela hayapo kwa vile sukari ya bei chee kutoka Malawi inatosheleza .
Mungu ibariki Malawi .