Wananchi wa Kyela wanatamba na Sukari ya Malawi

Si ukute kule watu hawanywi sana chai/hawatumii sana sukari kwasababu ya umasikini uliokithiri. Malawi ni masikini kupita kiasi ukilinganisha na TZ. Hata Zambia, sukari ni bei chee sana. Shida ya Bongo sema ni kodi, na pia wazalishaji wa sukari wanayo ile monopolization, wanaweza kuzuia kuuza sukari ili uwepo uhaba bei ipande wao wapige pesa ndefu zaidi na hiyo huwa wanakuwa wamekula deal na viongozi ili uhaba wa sukari ukiwepo milango isifunguliwe. Kwasababu kama TZ kuna uhaba, jiulize kwanini ukinunua sukari Malawi au Zambia kuingiza hapa unakamatwa? Kwanini ukileta sukari toka Uganda na Kenya unakamatwa? Kwasababu tunalazimishwa kununua sukari iliyopandishwa bei ili wenye viwanda wapate faida mara mbili yake, na viongozi husika wana mgao wao kwenye ile faida. Tusemeje sasa?
 
Sukari imeambiwa ikusanye hela za uchaguzi za CCM
 
Kila siku tunaambiwa sukari inaua figo, inasababisha magonjwa ya moyo, lakini bado tunalalamika kukosekana kwa sumu hiyo , kwa nini tusitumia fursa hiyo kusema sukari sasa basi?

Matumizi mabaya ndio yanaleta shida. Ila sukari haiwez sitishwa eti kwamba inaleta matatizo, basi tusiendeshe magari kwasababu kuna ajali?

Sukari ina matumizi mengi mno kuliko hayo unayondhania. Haiwez sitishwa
 
dah,ila wananchi wanapata shida sana. binafsi ninamudu, na wengi humu mnamudu, sukari ikiuzwa 5000 kwangu sioni shida, ila kwa wananchi wa hali ya chini kwa kweli wanaumia sana, wengine hata chai wanainywa kwa manyanyaso sana, unakunywa chai maza kakaa paleee anaangalia unaweka vijiko vingapi, ukitaka kuongeza kikombe cha chai unaambiwa sukari ulishaitanguliza. (mfano tu), watu wanaumia sana.
 
Tanzania wanaishi level ya chini sana !
 
Halafu ikawaje nyie mnakosa sukari na Malawi imejaa ?
Miwa ndiyo yenye jibu sahihi kiliko hawa wanaccm waongo, wao wanadai eti miwa haina utamu wa sukari shauri ya mvua, huku Goba kila siku tunakunywa juisi ya miwa yenye sukari ya miwa! Hii ndiyo inanifsnya nisiwaamini hawa waongo ila ukweli wa kwanini tunakosa sukari jibu inalo miwa.
 
Hata Tunduma
 
Sasa unanipinga au unaniunga mkono ? utafiti wabafanya wasiojua , mimi niliyezaliwa na kukulia maeneo hayo natafiti kipi tena ?

Ungekuwa umezaliwa Kyela usingeweka uzi wa namna hii...
 
Matumizi mabaya ndio yanaleta shida. Ila sukari haiwez sitishwa eti kwamba inaleta matatizo, basi tusiendeshe magari kwasababu kuna ajali?

Sukari ina matumizi mengi mno kuliko hayo unayondhania. Haiwez sitishwa
Mazuri ndio yapi?
 
Kwani ni lazima tuzalishe, si waagize tu!
 
Sukari itazalishwa vipi kama nguvukazi ya taifa ipo mijini na vijijini ina-bet tu. Raw materials ya sukari ni miwa ambayo inabidi ilimwe kiwanda wauziwe na wazalishe sukari. Lawama haziwezi kuwa malighafi za uzalishaji. Timiza wajibu wako. Jiulize mimi kama mchangiaji wa mada hii nina ekari ngapi za miwa? Haya matatizo ni our own making. Asubuhi njema
 
Kila siku tunaambiwa sukari inaua figo, inasababisha magonjwa ya moyo, lakini bado tunalalamika kukosekana kwa sumu hiyo , kwa nini tusitumia fursa hiyo kusema sukari sasa basi?
Ingekuwa hivyo basi wazungu ambao waliishaendelea kitambo wote wangekufa kwa matumizi ya sukari
 
Mkuu siyo Kyela ni hii Mbeya yote tunapiga Malawi na ya Zambia. Buku Tano yako tuu ndani ya pakti ni mwendo wa brown sugar
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…