Wananchi hawa wa Mbagala Rangitatu, Dar es Salaam, wamedai kubomolewa makazi, vibanda vya biashara zao na Manispaa ya Temeke wakati kesi iko mahakamani, tukio hilo limetokea Mei 2, 2026.
Wananchi wanadai wana zuio la Mahakama Kuu na kesi ipo mahakamani ila Manispaa ya TEMEKE walifika ghafla Mei 1, 2026 kudai watu wote waondoke wanasema Jumamosi (Mei 2, 2026) watavunja.
Wamechomeka bango Saa 7 Usiku wa kuamkia Ijumaa na wakaandika hatua za Kisheria zitachukuliwa ila wamepita jioni na vi-speaker wametangaza kwamba watu watoe vitu watavunja Jumamosi ndiyo unaona taharuki.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.