Wananchi wa Mlolongo huko Nairobi wamlazimisha kiongozi wao kutembea kwenye maji machafu kuonyesha hali mbaya ya miundombinu

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Inaonekana kama Wakenya wameshachoshwa na ahadi za uongo kwa hivyo wameamua kuchukua sheria mkononi.

Wakazi wa eneo la Mlolongo mjini Nairobi wameamua kumpitisha kwenye dimbwi la maji mchafu, kiongozi wa Kaunti yao Daniel Mutinda ili kumuonesha changamoto wanazozipitia kila siku.

Video zinazozunguka kwenye mitandao ya kijamii zinamuonesha kiongozi kaunti ya Syokimau/Mlolongo alilazimishwa kutembea kwenye maji machafu, huku wakazi wa eneo hilo wakimsisitiza aangalie kwa makini dimbwi hilo maji ili ajionee hali halisi wanayopitia wananchi

Katika video hiyo wakazi wengine walionekana wakimhakikishia kuwa hawakuwa na nia ya kumdhuru, bali walitaka kufikisha ujumbe kwa uwazi.

Soma pia: Wananchi kushirikishwa kumtoa madarakani Naibu Rais wa Kenya

Kwenye video hiyo Mutinda, ambaye alichaguliwa kwenye kiongozi wa Kaunti hiyo mwaka wa 2022, alionekana akiwa na wasiwasi lakini alijaribu kubaki mtulivu huku akiwa amezingirwa na wakazi waliokuwa na ari ya kuonyesha hali mbaya ya miundombinu katika eneo lao.

Hivi kwa nchi aina hii ya wananchi wapo kweli? Kuwawajibisha viongozi waliochaguliwa kwa kura za wananchi ni kama huo utamaduni haupo kabisa Tanzania. Wabongo mnakwama wapi?

Hakuna nchi hii kiongozi wa kupita kwenye maji machafu. Hayupo. Na pia hayupo mwananchi wa kumfanya apite. Kilichobaki kuombeana kifo tu ndio mana mtu maarufu wa kwenye siasa akifa watu asilimia kubwa wanachekelea. Hio ndio faraja yako pekee.
 
Wakuu,

Inaonekana kama Wakenya wameshachoshwa na ahadi za uongo kwa hivyo wameamua kuchukua sheria mkononi.

Wakazi wa eneo la Mlolongo mjini Nairobi wameamua kumpitisha kwenye dimbwi la maji mchafu, kiongozi wa Kaunti yao Daniel Mutinda ili kumuonesha changamoto wanazozipitia kila siku.

Video zinazozunguka kwenye mitandao ya kijamii zinamuonesha kiongozi kaunti ya Syokimau/Mlolongo alilazimishwa kutembea kwenye maji machafu, huku wakazi wa eneo hilo wakimsisitiza aangalie kwa makini dimbwi hilo maji ili ajionee hali halisi wanayopitia wananchi

Katika video hiyo wakazi wengine walionekana wakimhakikishia kuwa hawakuwa na nia ya kumdhuru, bali walitaka kufikisha ujumbe kwa uwazi.

Soma pia: Wananchi kushirikishwa kumtoa madarakani Naibu Rais wa Kenya

Kwenye video hiyo Mutinda, ambaye alichaguliwa kwenye kiongozi wa Kaunti hiyo mwaka wa 2022, alionekana akiwa na wasiwasi lakini alijaribu kubaki mtulivu huku akiwa amezingirwa na wakazi waliokuwa na ari ya kuonyesha hali mbaya ya miundombinu katika eneo lao.

Hivi kwa nchi aina hii ya wananchi wapo kweli? Kuwawajibisha viongozi waliochaguliwa kwa kura za wananchi ni kama huo utamaduni haupo kabisa Tanzania. Wabongo mnakwama wapi?

View attachment 3164652
Huku bongo wangepigwa na policcm mpaka wachakae.. Wengine wangetekwa na kupotezwa
 
Back
Top Bottom