Wananchi wa tanzania wanampenda na kumuamini sana Rais samia, mataifa duniani yanamkubali mno

Kabisa niliona siku Ile amepanda Boti kutoka Zenj jinsi abiria walikuwa wanamfhrahia na kutaka kusalimiana nae.

Ila machadomo yatabisha 😁😁
haya yana hasira mbaya sana na hayajua yanaksirikia nini.
Nadhani hadi kuitwa manyumbu ni kwaajili hiyo tabia...

Dr.SSH anapendwa, anakubalika na anaaminika mno kwa wananchi and this is real
 
Najua ninachofanya....
Mkate huandaliwa mekoni lakini unawe,a kufika hadi chemba ya mfalme
unajifanya mbantu sana na misamiati na vimisemo ili nipotea maboya sio...
 
CCM kila rais aliyepo madarakani anapendwa sana ,wananchi wanataka katiba ibadilishwe ili agombee mpaka kifo☺️ . Huu upuuzi ulianzia kwa Kikwete akawapuuzia, Magufuli akavimba kichwa na kujiona bila yeye Tanzania sio lolote.

Magufuli kata na mlioku mnamwimbia nyimbo za kumsifu na kumwabudu mmeamua kuzihamishia kwa Samia😏😏. What's so special about Samia mpaka mmewahoji watanzania na wameonyesha wana mahaba naye ya kufa na kuzikana?

Mfumuko wa bei,Rushwa iliyopitiliza,raia kuonewa na polisi pamoja na viongozi kukosa uwajibikaji ndani ya serikali yake . Matumizi makubwa ya fedha za umma,makazi ya rais ni Dodoma lakini yeye anaishi dar,waziri Mkuu dar,mawaziri wote dar pamoja na viongozi wa taasisi nyingine za govt.

Hawa wanalipwa extra kwa kufanya kazi nje ya vituo vyao vya kazi wakati wamama waja wazito wanakufa kwa kukosa hela za kujifungulia (huduma inatakiwa kuwa bure). Ajira mpya hakuna,viongozi wanaangalia maslahi yao tu(sheria mpya ya mafao ya wenza wa viongozi). I wish hiyo sheria Inge-cover wenza wa watumishi wote wa umma 😏😏.

Mtu mzima kujipendekeza kwa viongozi wa kisiasa haipendezi,kwenye ground wananchi wanak kaangwa na maisha magumu halafu wewe unaleta ngonjera za mahaba.
 
umejieleza vizuri kiungwana sana mwanzoni, kufafanua changamoto na kasoro ambazo unahisi ni tatizo na ingefaa hayo yawe kipaumbele kwa serikali kushughulika nayo...

Nataman nikueleze kinagaubaga kila changamototo ulotaja hapo juu, lakini nasita kwasababu tone ya maneno yako ya mwisho ilianza kubadidika na kuonyesha where your mindset belong too...

Itoshe kusema tu,
serikali imefanya mengi sana vizuri sana katika kila idara na kila sekta.

Pamoja na kufanya vizuri na kupongezwa sana na wananchi, bado kuna kasoro na changamoto ndani ya mafanikio hayo.

Na serikali inachukua kila hatua kurekebisha na kusahihisha kasoro hizo ili wananchi waendelea kuafaidika na kunufaika na huduma mabalimbali zinafadhiliwa na serikali na hilo ndio chimbuko la mapenzi ya wananchi kwa Rais lakini pia ndio chanzo cha wananchi na waTanzania wengi sana kumkubali na kumuamin sana Dr. Samia Suluhu Hassan

Na tunayaelezea haya kwa ujasiri mkubwa kwasababa ni ukweli mtupu na hatumuonei mtu haya wala aibu hata kidogo..
 
Chawa katika ubora wako. Halafu nikiangilia nauli zinavyopanda Kila mara, na huu mgao wa umeme, nimeamini chawa mnaishi Tanzania yenu.
 
Yaani viongozi kuishi nje ya Dodoma ambako ndio kituo Chao Cha kazi, ndio hizo changamoto wanazozifanyia kazi? Chawa shughuli mnayo safari hii.
 
Yaani viongozi kuishi nje ya Dodoma ambako ndio kituo Chao Cha kazi, ndio hizo changamoto wanazozifanyia kazi? Chawa shughuli mnayo safari hii.
ukimuona kiongozi yeyote yuko dar, mbeya mwanza, arusha , dodom na hata nje ya nchi huyo yupo kzini anachapa kazi.

sasa usipopenda kumuona dar, dodomo ama arusha, hiyo ina baki ni suala lako binafsi. Wapeni nafasi hao viongozi wachape kazi hakuna kulala muda ni mchache....
 
Chawa katika ubora wako. Halafu nikiangilia nauli zinavyopanda Kila mara, na huu mgao wa umeme, nimeamini chawa mnaishi Tanzania yenu.
suala la kupanda gharama za nauli halikwepeki,
hata na hivyo serikali inashughulika nalo usiku na mchana ili huyu mwananchi apate ahueni na unafuu wa maisha katika jambo hilo.

Subra na ustahimilivu ni muhimu sana tunapoliendea jambo hili....

Msiwe na wasiwasi wowote serikali sikivu chini ya kiongozi mkuu shupavu ipo kazini kwa maslahi mapana ya nchi na watanzania wote...

Kwa umakini, umahiri na weledi wa hali ya juu serikali inashughulika kwa bidii sana kuona namna ya kulirahisisha jambo hili licha ya kwamba linachochewa na soko la mafua la dunia na matatizo ya vita maeneo mbalimbali duniani...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…