Wananchi wadai DC wa Kilosa anasababisha maafa na hafuati Sheria, mwenyewe asema si kweli

Wananchi wadai DC wa Kilosa anasababisha maafa na hafuati Sheria, mwenyewe asema si kweli

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
706
Reaction score
1,716
Wakazi wa Kata ya Chanzulu, Wilaya ya Kilosa, wamekiomba Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Morogoro kuingilia kati migogoro ya ardhi inayoendelea katika eneo hilo ili kupatikana suluhisho la kudumu.

Ombi hilo limetolewa katika mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi, ulioandaliwa na Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Morogoro, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 49 ya kuzaliwa kwa CCM, ambapo wanamtuhumu Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka kutotenda haki katika kushughulikia changamoto zao.

Upande wa Shaka amesema "Kuna watu wanajiona wana haki ya kumiliki ardhi kuliko wengine jambo ambalo siyo sahihi, nimekaa nao mara kadhaa, wameenda kote wanapokujua lakini mimi siwezi kutafuna maneno."

Stori: Michuzi Blog
 
Michuzi bado yupo?
Mbona Quality ya Camera ni mbovu sana bado anatumia Canon za mwaka 2010?
 
Hiyo wilaya Ina ugomvi miaka na miaka, wabadirishe mkuu wa wilaya, wamasai wamesha muhonga huyo DC.


Hawez jua uchungu wa kulima halafu ukute mfugaji anapitisha tu ng'ombe zake ktk shamba lako.

Watafute mtu mwenye hekima ndio ashike hiyo wilaya hivi mtasikia watu Wana anaza kuuana sasa hivi , vita vya wafugaj na wananchi vitaibuka tena kama zaman
 
Back
Top Bottom