Wananchi wafunga Barabara ya Babati/Singida wakipinga kuuza mazao yao katika mfumo wa stakabadhi ghalani

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760

Wananchi Wakulima na Wafanyabiashara wa Kata Masakata Wilayani Hanang mkoani Manyara, wamefunga barabara ya Babati /Singida na kusababisha msongamano mkubwa wa magari kwa saa moja, huku wakipinga kuuza mazao yao katika mfumo wa stakabadhi ghalani, kwa madai ya kucheleweshewa malipo yao kwa muda mrefu, pamoja na kushinikiza serikali kuyaachia magari yaliyokamatwa, yakidaiwa kutorosha mazao ya dengu na mbaazi.
 
Nchi hii ina mambo ya kijinga sana. Hebu fikiria mtu analima mazao yake kwa tabu na kwa gharama kubwa halafu wanatokea "dudumizi" wachache wanakataa kuwalipa wakulima stahiki zao. Mbona mishahara ya kunenepesha matumbo yao haizuiliwi kulipwa kila mwezi? Sasa why wakulima wanyanyaswe kiasi hiki. Au na hii nayo inahitaji wazungu waje wasimamie wakulima ili walipwe stahiki zao?
 
Iringaa
Song each
Mbeya
Moshi
Dodoma
Rukwa

Hawawaa woteeee wanalalamikaaaaaaa
Kaeni mjipange kana hakuna hela ya malipo msitafute laana acheni waty wauze
Wataishia kupigwa
marunguu Wenyewe watafungua Road 😄
Yah kweli mpunga hakuna sahvi
Pesa ziko kwa wachache

Ova
 
Mfumo ni mzuri,kunahitajika usimamizi wa kutosha ili kuondoa hizo changamoto,ukumbuke huu mfumo kuna matajiri hawautaki kwahiyo mpambano wako sio wa kitoto...
 
Mfumo wa stakabadhi ghalani ni mzuri na unaondoa walanguzi tatizo hao vyama vya msingi waliopewa jukumu la kuuza hayo mazao Wana weka urasimu mwingi mkulima anacheleweshewa malipo yake.
Uzuri gani wakati wakulima wenyewe hawautaki mpaka wanafunga barabara, acheni kujifanya mna akili kuliko wakulima wenyewe wanaouza mazao yao
 
Kwani lazima kuwauzia serikali? Si wawaachie wapambane wenyewe kutafuta soko.!
 
Wakulima wanadai kucheleweshewa malipo hiyo ni changamoto ambayo serikali inatakiwa kuitatua haraka .lakini mfumo kama mfumo wa uuzaji hauna shida. Zamani mkulima alikua anauza kwa bei amayopangiwa na madalali na watu wa kati ambao si wakulima.
 
Serikali hainunui ila imeweka mfumo wa uuzaji ambao utaiimarisha vyama vya ushirika na wakulima waweze kupata bei mzuri
 
Mfumo ni mzuri,kunahitajika usimamizi wa kutosha ili kuondoa hizo changamoto,ukumbuke huu mfumo kuna matajiri hawautaki kwahiyo mpambano wako sio wa kitoto...
Matajiri ndio wanaupiga vita kwa sababu wamezoea kuwalalia wakulima.
 
Wakulima wanadai kucheleweshewa malipo hiyo ni changamoto ambayo serikali inatakiwa kuitatua haraka .lakini mfumo kama mfumo wa uuzaji hauna shida. Zamani mkulima alikua anauza kwa bei amayopangiwa na madalali na watu wa kati ambao si wakulima.
sasa wamefunga barabara na kuwatetea hao mnaowaita watu wa kati muyaachie malori yao, acheni excuses kuna shida
 
Vyama vyote vya ushirika vinatakiwa kuwa na Saccos ili inapotokea mwanachama wa ushirika wao amekwama au anaitaji pesa ya alaka Saccoss in mkopesha watakuja kumkata msimu wa mavuno. Kuna wazazi wanakosa pesa zakuwapeleka watoto wao shule mwezi January lkn ni wanachama wa vyama vya ushirika na wanauzo mazao yao kupitia vyama hvyo. Sasa mtu kama huyo anakwama wapi wakati ushirika hupo. Au maana ya ushirika ni nini?
 
Wananchi Wakulima na Wafanyabiashara wa Kata Masakata Wilayani Hanang mkoani Manyara, wamefunga barabara ya Babati /Singida na kusababisha msongamano mkubwa wa magari kwa saa moja, huku wakipinga kuuza mazao yao katika mfumo wa stakabadhi ghalani, kwa madai ya kucheleweshewa malipo yao kwa muda mrefu, pamoja na kushinikiza serikali kuyaachia magari yaliyokamatwa, yakidaiwa kutorosha mazao ya dengu na mbaazi.
Hebu fikria, unazalisha bidhaa yako,mnunuzi unamuona, lakini kenge wa CCM wanakuja wanakuambia hapana huwezi, kuuza moja kwa moja, leta kwetu tukuuzie, harafu utatulipa kiasi kwenye kila kilo,
 
sasa wamefunga barabara na kuwatetea hao mnaowaita watu wa kati muyaachie malori yao, acheni excuses kuna shida
Changamoto zipo na zinatakiwa kufanyiwa kazi. Kusini Lindi , mtwara na ruvuma mfumo unaotumika ni huu kwa miaka yote na wakulima wameshauzoea na wanaufurahia . Hu ukanda wa kaskazini inaonekana ndio wanaanza kuzoeshwa kwahiyo changamoto ndogo ndogo haikosekani zinatakiwa kurekebishwa mapema ili wakulima wapate fedha zao.
 
Sawa lakini tatizo liko wapi wakiuza kwa jinsi wanavyotaka wao kuliko kuwalazimisha mfumo wenu utumike, kama mfumo wenu ni mzuri watautumia, na acheni mifumo mingi itumike, choice is everything
 
Back
Top Bottom