POTOSHI Wananchi wakichimba barabara ni kutoka maandamano ya Kenya 2025

POTOSHI Wananchi wakichimba barabara ni kutoka maandamano ya Kenya 2025

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
KENYA08JULAI2025.jpg
1751994739671.png
 
Tunachokijua
Baadhi ya watumiaji wa mitandao mbalimbali ya kijamii wamekuwa wakisambaza Picha inayowaonesha wananchi wakichimba barabara ya lami na kueleza kuwa ni tukio kutoka kwenye maandamano yanayoendelea nchini Kenya. Rejea hapa

Je, ni upi uhalisia wa picha hiyo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia google reverse image search umejiridhisha kuwa picha hiyo si kutoka nchini Kenya bali ni kutoka nchini Afrika kusini, ambapo ilichapishwa mtandaoni mwezi Septemba mwaka 2020.

Aidha taarifa iliyochapishwa katika tovuti ya News24, chombo cha habari cha Afrika Kusini, inaeleza kuwa wakazi walikuwa wakiandamana kutokana na ukosefu wa maji na umeme katika jamii yao.

Hivyo kuitumia picha hiyo na kuripoti kuwa ni tukio kutoka kwenye maandamano nchini Kenya ni upotoshaji.

​
Back
Top Bottom