SoC02 Wananchi wamepata elimu ya kutosha kuhusu sensa ya watu na makazi, kwa maendeleo?

SoC02 Wananchi wamepata elimu ya kutosha kuhusu sensa ya watu na makazi, kwa maendeleo?

Stories of Change - 2022 Competition

Madjeshi

New Member
Joined
Jul 27, 2022
Posts
2
Reaction score
0
Sensa ya Watu na Makazi inatarajiwa kufanyika Agosti 23 mwaka huu kote nchini, wengi tunaamini na kufahamu Sensa ni muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu. Bila shaka kuna baadhi ya watu hawajatambua umuhimu wa Sensa katika taifa letu la Tanzania licha ya zoezi hilo kuwasaidia Wananchi hao na kurahisisha mipango mbalimbali.

Licha ya Serikali kuhamasisha kila kona, kila sehemu kuhusu umuhimu wa Sensa, kupitia Vyombo mbalimbali vikiwemo Vyombo vya Habari, lakini kuna idadi ya watu bado haijatambua umuhimu wake kwa maendeleo ya taifa, na ustawi wa nchi yetu hususani kwa maendeleo ya Jamii, Uchumi na nyanja mbalimbali.

Elimu ya Sensa inatolewa kila kukicha kupitia Vyombo mbalimbali, lakini cha kushangaza! mara nyingi nimelisikia kundi la Wanafunzi pekee wakiitaja na kuizungumzia Sensa ya Watu na Makazi, tena kwa kuihusisha na likizo au nyakati za Mitihani, bila shaka hata wao baadhi yao hawatambui umuhimu wake!.

Huenda kwa Watu wenye kiwango fulani cha Elimu wanaelewa umuhimu wa Sensa, bila shaka kutokana na viwango vyao vya uelewa kuhusu zoezi hilo ambalo linatarajiwa kufanyika Agosti mwaka huu, sidhani kama kuna baadhi ya Wasomi hawaelewi au hawatambui umuhimu wa Sensa kwenye taifa letu.

Kwa mwaka huu wa 2022, Sensa inafanyika Agosti 23 nchi nzima, licha ya hamasa kutoka Serikalini na Vyombo vyake mbalimbali kama Serikali za Mitaa. Lakini bado sijawasikia Wananchi wakiizungumzia Sensa kwa ukaribu na kwa umuhimu, maana yake kujiweka tayari kuhesabiwa itakapofika siku husika.

Kama idadi kubwa ya Wananchi hawatatambua umuhimu wa Sensa, maana yake hata siku yenyewe ya kuamkia Agosti 23, watashangaa pindi Makalani watakapopita Nyumba hadi Nyumba kuwahesabu Wananchi hao. Lakini wengi tunaamini endapo watahesabiwa kutakuwa na matokeo mazuri kwa nchi baada ya kujua idadi ya watu na kutambua aina ya watu ambao wanaishi kwenye nchi yetu.

Serikali imefanya jambo la msingi na la maana kujua idadi ya watu wake, kwa kuitambulisha Sensa ya Watu na Makazi nchi nzima. Wananchi wa kila rika wanapaswa kujua umuhimu wake ili Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa na mipango thabiti ya maendeleo katika nyanja mbalimbali kama nilivyosema awali.

Endapo, Serikali itafahamu na kutambua idadi ya watu kwa ujumla wake, itaweza kupanga mipango mbalimbali ikiwemo masuala ya Afya na Ustawi wa Jamii, itasaidia katika usambazaji wa huduma za jamii sehemu mbalimbali kama vile, Shule na Zahanati.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom