samahani kwa kuandika hivi....simhukumu marehemu Hamza wala kuitetea Serikali najaribu kuwaza tofauti nakujenga hoja fulani.
Elchapo na kundi lake la Sinaloa Cartel kule kwao ni watu wema sana na walijitoa sana kusaidia jamii..Pablo naye pia alikuwa mtu mwema sana pale kwao, Osama binladen wapo wamilioni ya watu wanaamini binladen ni mtu mwema na ameonewa tu na USA na alikuwa akitetea haki zao....wapo majambazi mtaani tunaishi wao ni wati wema sana na hatujui lolote kuhusiana na dark side yao....wale vijana wa 11sept baadhi waliishi Germany na mama aliyekuwa jirani yao aka mpangaji mwezao alisema walikuwa vijana safi sana, wakalimu sana nk....
Kama tunaamini Hamza kaonewa na sio Gaidi basi ni vyema mmoja wetu akadai justice for Hamza kwa either kufungua kesi kudai uchunguzi huru au ukweli wa jambo...kesi sio lazima iwe Tanzania popote pale tunaweza kufungua kudai justice for Hamza....
Issue ya Hamza kudhulumiwa ilianzia mitandaoni kwa raia na mamlaka zinakuja kutumbia Hamza ni gaidi, tuamini mtandaoni au Serikali... wanaharakati wetu ambao wengi wanasheria, wanaharakati wetu kule twita kwanini wasiidai haki ya Hamza kwa kukusanya ushahidi na kuishitaki serikali.?