Wananchi wawashambulia wabunge kufuatia adhabu kwa Askofu Gwajima na Silaa

Yes, nchi ina wajinga wengi sana, hata hilo kundi la wasomi uliloorodhesha hapo nao ni wajinga, huwa hawana misimamo wanayumbishwa kama matawi ya miti ili wapate kula yao, kama mnawategemea Chadema kumaliza hizo chanjo msijali.
 
walioharibu ni hao akina Gwajima na Mollel walianza kwa kuisema vibaya chanjo lakini ndiyo hao hao leo wanasema ni nzuri, wananchi washike lipi?

Wewe kama una akili timamu kirusi cha kwanza cha corona kiliitwaje na kasi yake ilkuaje na ss kirusi kinaitwaje na kasi yake ikoje? Kama kirusi kinabadilika unashangaa kubadilika watu? Acha hizo tafakari
 
Hiyo ni kusema kwamba jamaa wamechagua Vita zao na wanashinda! Unabakiwa na chaguo chache Tu chagua Vita yako ikiwa ni kurekebisha Hizo fikra za watu, kujiunga nao au kuwa mtazamaji Tu
Ila upuuzi ndio utadumu kuwa na wafuasi wengi ndio maana watu wa Aina ya Gwajima Mimi nabaki kuwa mtazamaji Tu wa matukio Yao hata kuwachukia ni matumizi mabaya ya chuki
 
Wewe kuandika tu kiswahili ni majanga, unadhani unaweza kujua na kuchambua vizuri hoja za Askofu Gwajima kama “sauti ya nyikani” na kinachoendelea nchini!

Kiswahili ni lugha nyepesi kwangu. Lakini wewe unaleta ulimbukeni wako wa jiwe, na jiwe wako ameshaenda harudi tena
 
Sawa ila kumbe ukichanjwa bado kuumwa unaumwa ...Maana ya chanjo si ni kinga ya kuzuia ugonjwa fulani ukiingia mwilini usilete madhara sasa mbona hayo madhara ya corona bado yatatokea hata kama nimechanjwa hebu nipe elimu
Una ushahidi wa watu waliopata chanjo na kupata madhara kufikia kulazwa "sadaruki-ICU"?!!!

Ni hivi.....

Unapopata chanjo haina maana kuwa HUWEZI KUPATA MAAMBUKIZI....bali Kuna "chance" KUBWA ya kutofikia hatua mbaya.....

Watoto wadogo wanachomwa chanjo dhidi ya INFLUENZA(FLU)....kwani huwa hawapati mafua?!!!

Wazungu wanapokwenda maeneo yenye KIPINDUPINDU huchomwa chanjo dhidi yake siku 7-10 kabla....wakija maeneo yenye malaria(epidemic) humeza dawa za kuzuia kupata maambukizi makali yatakayopelekea "severe malaria"....

Kwa hiyo kwa kuwa mtu amepata hizo chanjo (KIPINDUPINDU+MALARIA) ndio akanywe maji machafu(yenye vinyesi vya binadamu) na kulala pembeni ya mabwawa yenye VIDUDU VYA MALARIA?!!

Kwako mkuu mwenye cheo kikubwa "kisichopewa jina bado ndani ya CCM".......
 
Mkuu sikubaliani na wewe ktk hoja zako tatu hapo juu.
Wanaopinga chanjo ya corona wanao uelewa wa kutosha tu kuhusu masuala ya serikali na bunge. Tunafahamu kwamba kwamba wabunge ni wawakilishi wa wananchi na kwa hivyo ni vyema wakaangalia changamoto/mawazo yao na kuipelekea serikali kupitia bunge.
Si kweli kwamba mawazo/maoni ya wapinga chanjo yanatoka mitandaoni tu, kwani mkuu wewe hufuatilii media zingine? Wewe hufalii vipindi kwa mfano tu kama malumbano ya hoja na vingine vingi tuu ambavyo mtu yeyote, wa itikadi yoyote ananafasi ya kushiriki?
Wewe hufatilii hata watu wanaopiga simu kutoa maoni juu ya chanjo ya corona? Vinginevyo ungetoa njia mbadara ambayo ni sahihi kwako kupata data sahihi.
Pia si kweli kwamba wenye mawazo tofauti na chanjo ni vijana wa upinzani na wasio jielewa. Hapa umetukana watu wengi sana mkuu. Mbona kiongozi mkuu kabisa wa upinzani(Freeman Alkael Mbowe) alitoka hadharani na kutaka chanjo iwe lazima kwa wote na akapata uungwaji mkono na vijana wake maelfu kwa maelfu. Mbana wapo vijana wa ccm tena wanaolifahamu vizuri bunge na serikali hata kukuzidi, mfano akina polepole, jerry na wengine wengi wanamawazo tofauti na chanjo?
Ninachotaka kuuliza hapa ni kwamba, ni ipi njia sahihi ya kupata mawazo ya hao wanaojielewa?
 
Swala la chanjo Gwajima kapata uungaji mkono kwa wananchi wengi kwasababu kuu moja ni Legacy ya upumbavu wa Mwendazake kuwaongopea wananchi na kuwashawishi wananchi kuwa chanjo ni feki na kutumia kivuli Cha dini
Hahah such clown, thinking you know so much than most people about the vaccines?. We'll Never give in to their coercion or fear, once they put it in your blood, it cannot be removed. I am not getting it regardless and the more government tries to force it the more resistance. It's that simple.

Wewe unaona vaccines hazina shida kachome na familia yake usiwe na hasira au wivu kwa wale ambao hawajachoma, wakifa itaku athiri nini wewe? Sababu wewe ukichoma si unakuwa salama na familia yako? Then do just that to stay safe, but the majority have spoken hawataki chanjo. Don't blame it on Magu.
 
Hoja dhaifu sana hii kuchukulia data za mitandaoni kuwa ndio sauti ya wote. Hatuwezi kuwa upande wa upotoshaji kuwa ndio ulioshinda. Huwezi kutofautiana na Chama na Serikali yako mwenyewe huwezi jiuzulu na utoke au uanjishe chama chako.
 
Sawa mkuu....

Ingetokea hayati JPM(RIP) asingepinga chanjo...."huo usemao umma wa wapinga chanjo" WANGEPINGA LEO HII?!!!

WANGEPINGA kwa hoja zipi za KISAYANSI??!!

Ama wanapinga tu "kimbango" na kuongozwa na "conspiracy theories"?!!!

Nakukumbusha kuwa MAJIBU YANGU HAPO JUU nimeyatoa kwa yule aliyesema kuwa "Mh.Gwajima na Mh.Silaa" wameonewa na kamati ya BUNGE.....

Kesi ya Silaa(KODI YA MISHAHARA YA WABUNGE) ni tofauti na ya Gwajima....

Mh.Gwajima hakupewa adhabu na BUNGE kwa kuwa na hoja kinzani dhidi ya CHANJO bali kwa kusema UONGO USIO NA USHAHIDI KUWA VIONGOZI WAMEPEWA "MLUNGULA" ILI WAPOKEE CHANJO....je hapa umemletea ushahidi wake huo?!!!
 
Kuna mambo fulani unakuta ni ya lazima kwa Taifa sasa kuwazima wapotoshaji wakati fulani ni muhimu maana ukiwaacha wataonekana ndio washika hatamu.

Unapokuwa na nchi yenye sifa nilizotaja hapo awali na waliojaaluwa mdomo kama Tzn hii ni muhimu kuwa partial dictator vinginevyo wenye Nia ovu wanaweza kukutoa kwenye reli.
 
GWAJIMA, asitetewe , tatizo lake nikutaka kujifanya anajua kila kitu, kwamba dunia NZIMA inachanja kuangamiza watu wake, na Kama sivyo inawezekanaje iwe TZ

Yeye KWA imani yake hakulazimishwa chanja, na hakuna anaelazimishwa chanja , ila ni kosa pale msimamo wako unapoutumia shawishi ,na katisha watu wengine kupata chanjo Ili Hali unajua, kufa KILA mtu atazikwa na kaburi lake Wala huwezi kuwa na msaada WOWOTE siku ya kifo Cha mtu kikifika Kama ASKOFU,

Ni mtu wa ajabu tu anaweza kubaliana na Gwajima kwenye hoja zake za chanjo,
 
Binafsi nawaunga Mkono Mhe Askofu Gwajima na Mhe. Jerry Silaa. Yale yalikuwa mawazo yao binafsi na yangejibiwa kwa hoja.
 
Unaonekana unafarajika sana kuona baadhi ya watu wanakataa chanjo! Wewe hauitaki chanjo ukikaa kimya na mamno ya chanjo ukatuachia wajinga kunashida gani?





 
Swala la chanjo Gwajima kapata uungaji mkono kwa wananchi wengi kwasababu kuu moja ni Legacy ya upumbavu wa Mwendazake kuwaongopea wananchi na kuwashawishi wananchi kuwa chanjo ni feki na kutumia kivuli Cha dini
Haya wewe mwerevu tusaidie haya majibu.
Chanjo Zina usalama kiasi gani? Zinaweza kumkinga mtu kwa muda gani?
Short term na long term side effects ni zipi?
Kwanini ujaze consent form wakati chanjo zote hatukuwahi kujaza consent form?
Je ukichanjwa hutaugua?
 
Yes, nchi ina wajinga wengi sana, hata hilo kundi la wasomi uliloorodhesha hapo nao ni wajinga, huwa hawana misimamo wanayumbishwa kama matawi ya miti ili wapate kula yao, kama mnawategemea Chadema kumaliza hizo chanjo msijali.
Unasema wanachi ni wapumabavu!

Je nyie chadema ina maana siyo werevu pia? Mbona chanjo bado zipo na zilikuja milion 1 tu?

Ina maana nyie hamfiki milioni hapa nchini?
 
Unasema wanachi ni wapumabavu!

Je nyie chadema ina maana siyo werevu pia? Mbona chanjo bado zipo na zilikuja milion 1 tu?

Ina maana nyie hamfiki milioni hapa nchini?
Huo ni ushahidi kuwa chadema hawafiki milioni, hivyo kelele za kuibiwa kura waachane nazo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…