Wananchi wengi wakilipa kodi ndio wataweza kuwadhibiti viongozi wao. Lakini sio kwa nchi yetu ambayo walipakodi hawafiki hata robo ya idadi

Kwanza sijamtukana popote na si vyema kuniwekea tafsiri yako kwenye nilichokiandika. Unadhani ni sahihi kuwalaumu wananchi kuwa hawalipi kodi na hivyo wanapaswa kuacha kudai huduma za kijamii ambazo ni wajibu wa serikali kuzitoa?.
Kwamba katika nchi ambayo sekta nyingi haziko katika mifumo rasmi ulitaka wananchi walipeje hizo kodi mnazodai. Ni wajibu wa na nani kuhakikisha hizo bidhaa tunazonunua na kulipia kodi, hizo kodi zinafika serikalini? Ni nani asiyeona matumizi makubwa na ubadhilifu uliokithiri unaowavunja moyo wananchi kwa kiasi kikubwa. Kwa hili wananchi hawapaswi kulaumiwa kwa kiwango hicho hata kidogo.
 
Ni kazi ya nani kuhakikisha kodi ninayokatwa kama mlaji wa mwisho inafika serikalini?

Wajibu wako ni kudai risiti.
Kama mlaji unapuuzia risíti kwa nini unaamini aliyekuuzia hajapuuzia kulipa kodi kama wewe ulivyopuuzia kudai risiti?
 

Hakuna aliyelaumiwa.
 
We kweli hujielewi,hapa ninavyoandika tu hivi tayari nimelipa kodi kupitia bando
 

Wewe unajuaje úkinunua mfano kibériti umelipa kodi?
Kama hicho kiberiti kimepitishwa kimagendo au pale bandarini hakijalipiwa kodi kwa nini uamini umelipa kodi kwa kununua kitu.
Nini ushahidi ulionao?

Hao wanaolipa kodi nimekuambia hawafiki robo ya watanzania.
Sio ajabu hiyo robo tatu isiyolipa kodi ndio unanunua bidhaa kutoka kwao.

Tukirudi kwenye magari.
Unajua ni watanzania wangapi wenye Magari kama ukikadiria? Bila shaka hawazidi milioni moja na nusu kati ya watanzania milioni 60.

Vocha, unajua makampuni ya simu yànategemea wateja postpaid ambao hawazidi 10% hao waliobaki ni prepaid yaani Mimi na wewe ambao wengi wetu simu zinaweza kukaa Wiki nzima bila kuingiza vocha ya mia tano.
Bado robo ya watanzania haifiki.

Umetaja bidhaa zikiwa nje ya nchi ni gharama nafuu lakini zikija huku gharama zinaongezeka maradufu.
Mbona kuna bidhaa huku ndani ni gharama kuliko bidhaa zinazotoka nje ya nchi. Mfano Sukari kutoka Brazil.

Vipi mafuta kutoka Singida?
Vipi viatu vya ngozi vinavyotengenezwa hapa Bongo?
 

Utitiri wa kodi ni tafsiri ya kuwa nchi inawalipa kodi wachache ambao ndio wanakamuliwa hasa kwenye Direct tax

Wewe unaponunua bidhaa kwa mfanyabiashara asiyelipa kodi unasemaje kuwa umelipa kodi?

Hiyo ndio hoja. Kitu gani hakieleweki
 

Hapohapo nakuuliza.

Kama ishu ni kodi inayoongeza bidhaa kuwa na gharama(nakubalo nusu na kukataa nusu) mbona kuna wasiolipa kodi na wanauza bidhaa bei moja na wale wanaolipa kodi?

Nakupa Mfano,
Hapo mtaani kwako kuna kiwanda cha kutengenezea viatu vya ngozi. Hakilipi kodi.
Wanauza viatu elfu 30.
Alafu kuna mtu ameagiza viatu china vya aina ileile na analipa kodi na bei ya kiatu ni elfu 25 unazungumziaje hilo?
 
i
Kaka umeongea nadharia nyingi sana

Hoja ya mtoa hoja inasimama kwakweli. Kama nchi tukiwa na walipa kodi wachache ni ngumu kuifanya serikali kuwa acountable.

Watu wanaolipa kodi kikamilifu ni wafayakazi pekee, na ni kwa sababu na wao wamewekewa utaratibu wa lazima na ni rahisi kuwa capture.

Sekta isiyo rasmi hailipi kodi, na ni ngumu kuipata. Mfano watu wenye kipato cha chini ya 4M, hawatozwi kodi y mapato wamesamehewa..sasa hawa watahoji vipi kuhusu accountability ya serikali??? Wakitozwa kodi ni kelele kwenda mbele wakati nchi za wenzetu hata pesa ya matunzo kwa mtoto kwa wana familia walioachana inatozwa Kodi?
 
Kama hukudai risiti kosa ni la nani?
Kama unanunua bidhaa ambapo duka halilipi kodi na hauoni cheti cha kibali kosa nila nani?
Mkuu, haya matatizo yote hayajaibuka ghafla tu. Mwananchi yeyote akizisoma zile ripoti za CAG na akaona ni hatua zipi wanachukuliwa wale watuhumiwa, hatoona kamwe umuhimu wa kudai hizo risiti.
Akiona taabu na mahangaiko anayoyapata kwenye huduma za muhimu za kijamii (maji, afya, nishati, elimu n.k) huwezi kusumbuka na hizo risiti.
Akiona matumizi ya kufuru na ubadhilifu kuanzia ngazi za halmashauri hadi serikali kuu, hawezi hata kusumbuka kudai risiti.
Akiona taabu anayopata kushindia shambani kwa jembe la mkono na uhuni anaofanyiwa akishavuna mazao yake, hawezi hata kuiulizia hiyo risiti.
 

Unachosema ni sahihi
Ila wananchi wengi hawana hiyo Morali authority kutokana nao ni wahalifu. Wengi hawalipi kodi
 
Hakuna aliyelaumiwa.
Mkuu, tukubaliane kabisa kuwa kulipak kodi ni suala la muhimu na lazima kwa maendeleo ya nchi. Ila kama waliopewa dhamana wataendelea na ubinafsi huu, nina hakika wa kulaumiwa ni serikali yenyewe.
Hii nchi wananchi wamebebeshwa mzigo mkubwa sana, wakiamua hata kukwepa kodi ni sahihi kabisa. Wanashiriki na kuchangia ujenzi wa shule, vituo vya afya, vyoo n.k kuanzia msingi, matofali, ukuta, mawe na nguvukazi, serikali inakuja kuapua kwa bati za gauge 32.
Wanashiriki kuchimba mitaro ya kutandaza mabomba na maji yanatoka wiki moja yanakata jumla.
Wanashiriki.
Kila kaya unachangishwa kwa lazima shughuli zote hizo na kama huna wataondoka hata na godoro, masufuria na chochote kile. Nchi hii ina kodi na tozo zilizopitiliza pengine kuliko nchi nyingi tu za kusini mwa jangwa la sahara. Kiujumla nchi hii imeshindwa kabisa kutimiza lengo lake kuu la kuhakikisha ustawi na usalama wa watu wake, kwa mujibu wa katiba yetu.
 
Wajibu wako ni kudai risiti.
Kama mlaji unapuuzia risíti kwa nini unaamini aliyekuuzia hajapuuzia kulipa kodi kama wewe ulivyopuuzia kudai risiti?
Wajibu huo lazima uendane na matumizi sahihi ya hiyo kodi, vinginevyo sitoona umuhimu wa kuidai hiyo risiti, bora nimuachie huyo mwenye duka.
 
Mleta mada ungeainisha ni kodi gani watu hawalipi, maana kuna kodi nyingi sana, katika nchi zenye kodi nyingi huenda TZ pia imo.(mfano ni mafuta ya magari, wanasema karibia 50% ni kodi, maana yake ni kuwa huenda mafuta tulitakiwa kununua kwa 2500 lakini leo yanauzwa 3380)

Sasa uainishe ni kodi ipi watanzania hawalipi, then watu wa kodi waje hapa watoe maelezo ili kila mtu aelewe.


Ila kama ni indirect tax wote tunalipa, kila unachotumia except pumzi unakilipia.
 
Unachosema ni sahihi
Ila wananchi wengi hawana hiyo Morali authority kutokana nao ni wahalifu. Wengi hawalipi kodi
Mkuu, uko sahihi kabisa, lakini mzunguko wote huu utawezwa kuvunjwa na kutupiliwa mbali pale tu viongozi watakapoamua kwa dhati kuuvunjilia mbali. Vinginevyo hiyo moral authority ni lazima ionekane toka serikalini kushuka chini.
 
Wewe jamaa kumbe wakati mwingine huwa unatoa boko kama hili?

Au kwako wewe kodi unatafsiri iwe ile kichwa? Hakuna siku inaisha pasipo mwananchi kulipa kodi iwe directly or indirectly.

Kama unanunua bidhaa ambayo haijalipiwa kodi md hujadai risiti unapata wapi ujasiri wa kusema hakuna ambaye halipi kodi kwa siku?

Hivi unajua Watu milioni 15 wakilipa kodi kila mmoja ni sawa na Tsh 1.5Trilioni?

Kama kwa siku unayosema mtanzania akilipa kodi walau 500 kwa mwezi ni Tsh 15k kwa Mwaka 150k
Sasa kodi 150k × wananchi milioni 30. Unajua ni Trilioni ngapi
 
Hizo nadharia ndiyo hali halisi kutokana na mfumo wetu wa kiuchumi ambao sekta nyingi ziko nje ya mfumo rasmi. Serikali inayajua yote hayo na kufidia mapungufu hayo, imeweka tozo na kodi kubwa kwenye kila bidhaa. tunayonunua (mfano mafuta ya petroli,dizeli nk).
Ukienda kwa hao wenzetu walioendelea kodi ni kubwa na pia almost kila kitu kiko kwenye mfumo rasmi, ila pia hawana hizi tozo na usumbufu kwa wananchi hadi kwenda kufyatua matofali ya kujengea zahanati. Ila pia hao wenzetu viongozi wao wana nidhamu iliyotukuka ya matumizi ya hizo kodi na imechochea kuwepo kwa huduma bora kabisa za kijamii na kupandisha morali ya ulipaji kodi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…