Wananchi wengi wakilipa kodi ndio wataweza kuwadhibiti viongozi wao. Lakini sio kwa nchi yetu ambayo walipakodi hawafiki hata robo ya idadi

Mkuu, kumbuka nchango wa hizo tozo, ushuru na ada (non tax revenue) ni chini ya asilimia 10 tu ya makusanyo yote kwa mwaka?

Kwa hiyo hoja ya utitiri wa tozo in ngumu kueleweka. sasa, hapo kwenye kodi ya inayokusanywa na serikali kuu ndipo hapo penye changamoto kwa kuwa watu wengi hawachangii na ndipo serikali inapategemea zaidi. Mfano kwa mwaka ujao wa fedha serikali itakusanya takribani Trilion 29 kutokana na mapato ya kodi.

Ni muhimu watu kulipa kodi kwa wingi, hii itasaidia kuihoji serikali na pia kugharamia maendeleo yetu. Tusidanganyane, hizo nchi zilizoendelea watu wanalipa kodi hadi wanachanganyikiwa.
 
Kama ni ya magendo ni udhaifu wa mfumo sio mnunuzi, sisi tunachojua VAT analipishwa hata ukienda kununua diapers za mtoto mchanga
 
Nimeelewa vyema kabisa mkuu, nini kifanyike sasa ili walio wengi walipe kodi katika nchi ambayo sekta nyingi hazijarasimishwa? Ni nani wa kuhakikisha ukepwaji kodi wa wafanyabiashara wakubwa unapunguzwa kwa kiasi kikubwa. Nini wananchi wa kawaida wafanye ili kuhakikisha kuwa hata wakilipa hizo kodi zitakwenda mahala sahihi?
Kwa nchi zilizoendelea hatuwezi kujilinganisha nao, kwani mifumo yao iko vizuri, viongozi wanawajibika na karibia sekta zote ziko kwenye mfumo rasmi. Hata riba zao kwenye mabenki ni chini sana na zinawafavour wananchi wake, huduma za kijamii ni bora kabisa nk nk nk, na yote kwa kiasi kikubwa yanafanywa kwa kodi zao.
 
kama bidhaa inaweza kupita bandarini au kuingia nchini kimagendo Serikali ikashindwa kukata kodi itaweza kukusanya kodi ya mlalahoi kwa uaminifu kweli?Serikali ikishindwa kukusanya kodi kwenye bidhaa inayopita bandarini hyo Serikali labda genge la wahuni linaloongoza nchi!Hyo ni moja.
Mbili,aya yako ya pili umeandika mapichapicha,tatu kama watanzania ni wachache ndio wananunua magari so ndio sabab ya kufanya kodi iwe ya kuruka basi hauna sabab ya kutaka watz wengine walipe kodi maana ni kama hao wachache unawabebesha mzigo wa wale ambao hawanunui hayo magari.Kwenye petrol umeweka kodi 21,kwenye vipuli vya magari kuna kodi,kwenye bima ya magari nk na bado kwenye kuliagiza gari yaan unanyonga na kunyonga huyo mtu halaf unalialia kwamba watz hawalipi kodi!!!Hebu chukulia huyo mtz mmoja anafamilia tuseme unamkata maji,umeme,nyumba.Tuseme unamkata bima ya afya ya yeye na familia yake,akinunua chochote iwe chakula,mavazi na mahitaji mengine unakata kodi iwe directly au indirectly.Huyo akinunua gari unampiga kodi kuanzia kwenye gari lenyewe,bima ya gari na mafuta kila siku anapotumia gari lake(mafuta yenye kodi 21)!!!!Mtz huyohuyo anakatwa mafao kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.Sasa niambie hali ya huyo mtz mpaka hapo itakuaje?Chukulia mtz huyo ni mwaminifu sio mpigaji sio mlarushwa nk.Niambie kama anaweza kutoboa vzuri.
Mwisho umezungumzia kuhusu gharama za bidhaa kutoka nje na zile za ndani hasahasa umejikita katika kumlinda mzalishaji wa mdani.Unaweza kuwa na point hapa lakini mm nilitaka kukuonesha kuwa nchi za wenzetu ambao tunawaangalia kama mfano bado wanakodi ndogo sana kulinganisha na kwetu.Wenzetu wanambinu za kutanua wigo wa kodi tofauti na sisi.Hebu fikiria kama kodi ya magari ingeshushwa watu wengi wangeweza kununua magari mapya na hivyo pesa ya kodi lazima ingeongezeka.Tungepunguza uchafuzi wa mazingira na pengine tungepunguza hata ajali na kuepusha vifo...mambo n mengi.
Changamoto haipo kwenye watu kutolipa kodi ila ipo kwenye namna nzuri ya kutanua huo wigo..
 
Kila ununuapo bidhaa unalipa kodi sasa iweje wasifike robo?🐼
Hoja za ki-lumumba huwa sijui mnazitoa wapi...

Fikiria unaponunua mafuta pale Victoria au pale masaki Kwa tibaijukq na kulipa 18% ya VAT jee ukienda Kisutu kununua mchele utalipa Kodi gani?

Kodi za uficho (indirect taxes) huwa hazijengi nchi isipokuwa kodi za Moja kwa moja (direct taxes).
 
Leo naomba niseme mtibeli umetoa boko😂hakuna mwananchi asiyelipa indirect tax...kupanda daladala tu ushalipa kodi... Labda kama vituo vyote wanaingiza mafuta kwa magendo..na sisi si wajibu wetu kufatalia ni wajibu wa serikali...haya kuna wale wa vijijini tuseme hawapandi daladala..watanunua vocha tiyari kodi...kitu pekee hatulipii kodi ni pumzi...vyanzo vya kodi vilivyopo vinatosha kabisa kuibadili hii nchi..tatizo tuna wachumia tumbo wengi ambao tumewapa mamlaka ya kutuamulia mstakabali wetu hapo hata tungeongeza vyanzo elfu 20 au wananchi wote watafutiwe namna ya kuingia kwenye direct tax bado hatutoboi😂
 
Hoja ni nani anayelipa! Je ni Yule aliyekuuzia mafuta au ni uliyenunua mafuta?
Na kama aliyekuuzia mafuta, hiyo 18% ni ya nini kwa mnunua mafuta?
Je hiyo direct taxes analipa muuzaji au mnunuaji?
(Ukiondoa hiyo indirect taxes)
 
Hoja ni nani anayelipa! Je ni Yule aliyekuuzia mafuta au ni uliyenunua mafuta?
Na kama aliyekuuzia mafuta, hiyo 18% ni ya nini kwa mnunua mafuta?
Je hiyo direct taxes analipa muuzaji au mnunuaji?
(Ukiondoa hiyo indirect taxes)
Swali zuri...

Mleta mada anazungumzia direct taxes kuwa hazilipwi. Hizo indirect taxes nyingi zake hata wanaolipa direct taxes hulipa pia.

Fikiria mtumishi anayelipa Pay As You Earn (PAYE) na ana gari, jee naye ile "Consumer tax" ya "Value Added Tax (VAT)" ya kwenye mafuta hatalipa!??

Mfano wa pili ni wa wauza vyombo vya nyumbani kwa reja reja. Mmoja ana duka mwingine ni " machinga" wote wawili mauzo Yao Kwa siku ni laki 2.

Muuzaji mwenye duka kwanza kabisa atatakiwa awe na "Electronic Fiscal Device (EFD)"na atatakiwa aitumie na kuthibitisha kihasibu mapato na matumizi yake.

Huyu atatakiwa alipie leseni na tozo ya ushuru wa huduma (Service levy) ushuru wa usalama wa zimamoto na kadhalika.

Hayo yote wakati yanatokea mmachinga anayefanya biashara sawa na yeye hana anachotozwa.

Kwa ivo wanaolipa Kodi za kwa moja ni wachache. Na Kodi za moja kwa moja ndizo zinazokuwa za uhakika na ndiyo maana usipolipa, unafuatiliwa.
 
Hata mtoto mchanga analipa kodi kupitia nepi anazovalishwa !
Hakuna bidhaa yeyote isiyolipiwa kodi hata pipi zinalipiwa kodi na mlipaji mkuu ni yule mlaji wa mwisho Jombaa !🙏🙄
 
Hoja ni nani anayelipa! Je ni Yule aliyekuuzia mafuta au ni uliyenunua mafuta?
Na kama aliyekuuzia mafuta, hiyo 18% ni ya nini kwa mnunua mafuta?
Je hiyo direct taxes analipa muuzaji au mnunuaji?
(Ukiondoa hiyo indirect taxes)
Bidhaa yeyote iwe ni mafuta au pipi kwa Mangi mtaani bei atakayokuuzia amejumlisha gharama zake zote na ameweka na faida yake!

That means kodi zote zilizotozwa kwenye hiyo bidhaa kutoka kiwandani mpaka kwa muuzaji wa jumla naye ataweka hizo gharama za kodi zote na faida yake katika kila bidhaa kisha atamuuzia muuzaji mdogo naye ataweka na faida yake atakapo muuzia mlaji wa mwisho !

Kwahiyo mlaji wa mwisho atanunua bidhaa kwa bei ya juu kutokana na mlolongo wa kodi zilizotozwa bidhaa hizo !
Kwa muktadha huo hapo ni nani amelipa kodi ya hiyo bidhaa aliyoinunua huyo mlaji wa mwisho ???!!
 
mzeewaSHY unadhani wafanya biashara wanapolalamika.kuhusu mkurulo wa Kodi humaanisha kodi ya mlaji hiyo ambayo wewe umesema Kila mtu analipa!!??
 
Hakuna mwananchi asiyelipa kodi sema wafanyabiashara ambao kimsingi ni mawakala tu wa kodi ndiyo wengine wanazila hizo kodi wanazokusanya toka kwa wananchi.
Umeeleza kwa kifupi sana lakini hiyo ndio hali halisi ilivyo !!

Wafanyabiashara ni mawakala tu wa kukusanya kodi !
Kodi inalipwa na yule mtu wa mwisho atakayenunua bidhaa kisha akaenda kuivaa au kuila au kuitumia kwa matumizi mengine ya kawaida ya kila siku !!
 
Mkuu, mahesabu ya kodi hayaendi hivi. Kodi huhesabika imekusanywa kwenye tax points. Na kila kodi inayo point yake.

Muktadha huu uliouleta ni jambo lingine kabisa, huwezi kuiaccount.

Hoja ni kuwa, watanzania wengi hawako kwenye tax net, jambo linalowapelekea kushindwa kuifanya serikali iwajibike.
 
mzeewaSHY unadhani wafanya biashara wanapolalamika.kuhusu mkurulo wa Kodi humaanisha kodi ya mlaji hiyo ambayo wewe umesema Kila mtu analipa!!??
Mkuu Allen Kilewella ukiona mfanyabiashara anaendelea kufanya biashara ujue biashara zake zinamuingizia faida, vinginevyo assingeendelea kufanya biashara anazozifanya !

Ile kulalamika ni kwa sababu pesa siku zote huwa hazitoshi kwa mtu hivyo anataka apate faida kubwa zaidi na zaidi katika biashara zake akidhani labda atakidhi kiu yake ya mafanikio !

Lakini kumbe anasahau the bigger your income the bigger your problems !
Wanaishia kulalamikia kodi kama vile walipaji ni wao !
 
Mkuu logic ni moja tu kwamba kila mtu analipa kodi sio kusema kwamba eti watu wanaolipa kodi ni watu wachache tu !
 
Ha
Mkuu logic ni moja tu kwamba kila mtu analipa kodi sio kusema kwamba eti watu wanaolipa kodi ni watu wachache tu !
Hapana Mkuu, logic inakataa. Vipi kwa bidhaa zilizosamehewa Kodi?

Pia kwa muktadha huo, kodi iliyolipwa kwenye hatua fulani huenda kuwa gharama za uzalishaji. Hivyo katika point hiyo walaji hulipia gharama na sio kodi.

Ndiyo maana kikodi ukiulizwa una walipa kodi wangapi kwenye nchi yako huwezi semi wote. Principles zinakataa.

Sisi kwetu, kundi la walipa kodi ni kidogo sana. Kwa maana ya registered taxpayers.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…