Smart Dude
Senior Member
- Sep 23, 2023
- 114
- 161
Mkuu, kumbuka nchango wa hizo tozo, ushuru na ada (non tax revenue) ni chini ya asilimia 10 tu ya makusanyo yote kwa mwaka?Hizo nadharia ndiyo hali halisi kutokana na mfumo wetu wa kiuchumi ambao sekta nyingi ziko nje ya mfumo rasmi. Serikali inayajua yote hayo na kufidia mapungufu hayo, imeweka tozo na kodi kubwa kwenye kila bidhaa. tunayonunua (mfano mafuta ya petroli,dizeli nk).
Ukienda kwa hao wenzetu walioendelea kodi ni kubwa na pia almost kila kitu kiko kwenye mfumo rasmi, ila pia hawana hizi tozo na usumbufu kwa wananchi hadi kwenda kufyatua matofali ya kujengea zahanati. Ila pia hao wenzetu viongozi wao wana nidhamu iliyotukuka ya matumizi ya hizo kodi na imechochea kuwepo kwa huduma bora kabisa za kijamii na kupandisha morali ya ulipaji kodi.
Kwa hiyo hoja ya utitiri wa tozo in ngumu kueleweka. sasa, hapo kwenye kodi ya inayokusanywa na serikali kuu ndipo hapo penye changamoto kwa kuwa watu wengi hawachangii na ndipo serikali inapategemea zaidi. Mfano kwa mwaka ujao wa fedha serikali itakusanya takribani Trilion 29 kutokana na mapato ya kodi.
Ni muhimu watu kulipa kodi kwa wingi, hii itasaidia kuihoji serikali na pia kugharamia maendeleo yetu. Tusidanganyane, hizo nchi zilizoendelea watu wanalipa kodi hadi wanachanganyikiwa.