Wanaobahatika kuwa Marais wa nchi hii wanapoteza fursa ya kuingia katika historia ya kudumu kwa kushindwa tu kuwapa Watanzania Katiba Mpya

Wanaobahatika kuwa Marais wa nchi hii wanapoteza fursa ya kuingia katika historia ya kudumu kwa kushindwa tu kuwapa Watanzania Katiba Mpya

Mtu anayepigania katiba nakuacha kupigania masuala ya msingi yanayomgusa mtu mmojammoja ni kama kichaa tu anayeikota makopo jalalani
We ndo kichaa mla mavi kabsa. Hujui hata katiba ni nini.Jitaidi kuwa unajitengea muda wa kukaa na wasomi au wazee upate maarifa. Uko kapa sana.
 
Katiba ya sasa ina shida gani
Maisha ni siasa.
Siasa ni maisha.
Anzia na mamlaka ya rais akiharib nchi makusudi unamfanyaje!
Rudi kwenye namna viongoz wanapatikana.
Njoo kwenye misingi ya demokrasia na utawala bora uangalie uhuru wa mihimili mitatu na namna inachekiana.
Njoo kwenye kinachokusanywa kwa ajiri ya wote kama keki ya Taifa na namna kinatumika. Si ajab unaamin haya mambo hayakuhusu!
 
Katiba za vyama vyao wenyewe wanazivunja sijui ni nani aliyewaaminisha kwamba ukosefu wa katiba mpya ndiyo chanzo cha matatizo yao, ikiwemo na migogoro isiyoisha ya vyama vyao.
Huoni utitiri wa viongozi ambao hawana majukumu ya kueleweka, una DC, DAS, DED na Mwenyekiti wa Council eneo moja kama sio uharibifu wa pesa na rasilimali zinazotumika kama magari na mishahara yao, itoshe tu kusema wananchi tunabebeshwa mizigo mizito kwasababu ya nguvu ya wanasiasa
 
Hoja hapa ni kwamba usifikiri kwamba mwarobaini wa kila kitu kisichoenda sawa au usichoridhika nacho ni "katiba mpya". Hao ma DC, ma DED na mazagazaga wengineo si wamepewa majukumu kulingana na miongozo yao ya kazi? Kama wangetekeleza kwa ufanisi hayo majukumu yao inavyostahili mimi nadhani hilo siyo jambo linalosukuma ulazima wa kuwepo kwa katiba mpya. Wanasiasa wana mapungufu yao, lakini mapungufu yao ni mapungufu ya binadamu kwa ujumla kama ambavyo wale wanaojaribu kutuaminisha kwamba tunahitaji katiba mpya walivyo na mapungufu ya msingi wanayopaswa kuyashughulikia kuliko kunyooshea vidole au kupeleka lawama kwingineko.
 
Huu ndio ukweli mchungu kwa wote waliowahi kuwa Maraisi wa nchi hii baada ya Mwalimu Nyerere kuondoka madarakani.Raisi Mstaafu Kikwete alikaribia sana kupata nafasi hii ya kihistoria ila inawezekana alipotoshwa na wenzake ndani ya chama na huenda hili ni jambo analolijutia katika maisha yake na si ajabu siku moja anaweza kuja kukiri/kusema hadharani.

Watawala watambue hakuna kitu wanachoweza ku-achieve na kitachowapa heshima ya kudumu kama kuipatia nchi hii katiba Mpya, Katiba itayokubaliwa na makundi karibu yote ya watanzania kuanzia wanasiasa, wakulima,wafanyakazi,viongozi wa dini, watanganyika, wazanzibari, n.k.

Unaweza kujenga barabara na ma-flyover nchi nzima, kusimamisha majengo makubwa nchi nzima, kuinua uchumi wa watu na Taifa kwa ujumla, n,k, lakini baada ya muda yote haya yatazoeleka na kuonekana ni ya kawaida tu lakini kamwe sio Katiba Mpya inayoweza kuweka msingi bora wa ku-achieve zaidi ya hayo katika Taifa letu.

Raisi Samia, wewe ndio Raisi uliepo madarakani leo hii, hivyo uzi huu unakulenga wewe moja kwa moja na ukiifunyia kazi utakuja kukumbuka maneno yangu haya siku zote za maisha yako.

Mama kazi kwako, kwani fursa sasa iko kwako, hivyo usiache mwingine akaja kuitumia ukaishia kujilaumu.

Unapokuwa Raisi, si ajabu ukazungukwa na watu wanaotamani kuipata fursa hiyo, hivyo wanaweza kukupotosha ili wao au watu wao waje waipate hiyo fursa(sio rahisi kuliona hili au kuliamini, ila ni jambo linalowezekana kabisa kwa wenye kuona mbali).

Nelson Mandela aliepigani uhuru na usawa wa watu weusi nchini mwake, anaheshimika nchini mwake na duniani kuliko makaburu walioijenga Afrika Kusini tena akiwa amekaa madarakani kwa muhula mmoja wa miaka mitano tu.
Kwa kweli tuwafungue macho wapate kuona. Tanzania hii haiwezi kupata maendeleo bila utawala bora. Tutajidanganya tu.
 
Huoni utitiri wa viongozi ambao hawana majukumu ya kueleweka, una DC, DAS, DED na Mwenyekiti wa Council eneo moja kama sio uharibifu wa pesa na rasilimali zinazotumika kama magari na mishahara yao, itoshe tu kusema wananchi tunabebeshwa mizigo mizito kwasababu ya nguvu ya wanasiasa
Hapo bado kuna heads of departments DSO, DMO, DNO , DHO yaani ni vurugu tu.
 
Maisha ni siasa.
Siasa ni maisha.
Anzia na mamlaka ya rais akiharib nchi makusudi unamfanyaje!
Rudi kwenye namna viongoz wanapatikana.
Njoo kwenye misingi ya demokrasia na utawala bora uangalie uhuru wa mihimili mitatu na namna inachekiana.
Njoo kwenye kinachokusanywa kwa ajiri ya wote kama keki ya Taifa na namna kinatumika. Si ajab unaamin haya mambo hayakuhusu!

Unahisi shida ni katiba au wafata katiba?
 
Unahisi shida ni katiba au wafata katiba?
Katiba iliyopo ingefuatwa bado kama nchi tungefika mbali tu.
Sasa tatizo haifuatwi kwa sababu baadhi ya vipengere muhim vinatoa mwanya wa kutowajibishana vyema.
Kila binadam anahitaji cha kuhofia kukaa kwenye mstari.
Fikiria kama dini zingekuwepo ila kikaondolewa kipengere kimoja tu cha adhabu baada ya kifo! Jehanam
 
Katiba mpya ya kutafuta kushika dola. Ndio za wanaharakati.
 
Hawezi kushinda katika uchaguzi ulio huru na wa haki. Analijua hilo.
Raisi Samia, wewe ndio Raisi uliepo madarakani leo hii, hivyo uzi huu unakulenga wewe moja kwa moja na ukiifunyia kazi utakuja kukumbuka maneno yangu haya siku zote za maisha yako.
 
Nchi gani ilimaliza kujenga miundombinu? Hata Marekani bado wanajenga. It is a stupid argument kusema kuwa tufanye jambo fulani kwanza ndio Katiba ije. Taja nchi moja ambayo unafikiri ilimaliza maendeleo yote na sasa watu wake wamepumzika.
Bwashee huku kwetu makonde plateau tuna matatizo ya maji, shule, barabara, masoko ya uhakika ya mazao yetu, huduma bora za afya, nk. Tushughurikieni hayo kwanza maana ni basic needs za kuishi, katiba itafuata baadae.
 
Nchi gani ilimaliza kujenga miundombinu? Hata Marekani bado wanajenga. It is a stupid argument kusema kuwa tufanye jambo fulani kwanza ndio Katiba ije. Taja nchi moja ambayo unafikiri ilimaliza maendeleo yote na sasa watu wake wamepumzika.
In the same way, it is stupid kufikiria kwamba katiba mpya ndiyo itakuwa suluhisho la matatizo yetu yote. Ni mtu mjinga peke yake anayeweza kufikiri hivyo. Ninachosema mimi ni kushughulikia basic human needs: hatuhitaji katiba ili kupatia watu wetu haduma za maji, afya, shule nk. Kenya wana katiba mpya, ebu nenda kaone kama imepunguza umaskini huko karamoja!
 
Ili KINYONGA apate mtoto, lazima TUMBO lipasuke Ili watoto watoke salama, SACRIFCE lazima.

Kuzaliwa Kwa KATIBA iliyopo na CCM, sacrifice ilifanyika, TANU na TAA vilikufa.

Hivyo hivyo Kuzaliwa Kwa KATIBA mpya Kwa njia ya AMANI, lazima CCM ijitoe KAFARA, na Muundo wa Serikali iliyopo ubadilike.

Ni JAMBO gumu sana kulikubali Kwa kiongozi aliyepo, Mungu atasaidia lisowezekana,LIWEZEKANE . Amen.
Mkuu
Na muundo ninaodhani ni wa upinzani KUPEWA uwaziri mkuu wa jamuhuri na umakamu wake na Baraza mseto la mawaziri!!!
Tusubiri!!!
 
Mkuu
Na muundo ninaodhani ni wa upinzani KUPEWA uwaziri mkuu wa jamuhuri na umakamu wake na Baraza mseto la mawaziri!!!
Tusubiri!!!
Wananchi watapendekeza Muundo mzuri wa wawakilishi wao ktk Ngazi mbalimbali za uongozi. Tunapata KATIBA mpya Kwa Amani. TANZANIA ni NCHI iliyobarikiwa sana na Mungu. Amen
 
Back
Top Bottom