Wanaochukia mapinduzi matukufu ya Zanzibar 1964 wana ajenda gani nyuma ya pazia?

Sina shaka wewe mzee wetu ni mtaalam wa maswala ya Zanzibar

Ila
Nina swali moja tu

Enzi za sultan ambae ‘hakuwa na damu vidoleni mwake’ hakukuwa na ubaguzi wala matabaka?
Kulikuwa na haki kwa wakazi wote wa Zanzibar bilq kujali rangi wala dini zao?
 
Mkuu twende sawa, hali ya kiuchumi kwa matabaka yote matatu Zanzibar enzi za sultan ilikuaje?

Kulikuwa na usawa? Ama tabaka fulani lilipendelewa huku jingine lilikandamizwa systematically?

acha kukariri hadithi za ovyo.
 
Kwa nini hatajwi?
Today,
Swali hili ingependeza lijibiiwe na ASP kwa sababu Hanga alikuwa kiongozi wao na dunia inamtambua kuwa ndiye aliyepanga mipango yote akishirikiana na Oscar Kambona.
 
Count...
"Haki kwa wakazi wote bila kujali rangi wala dini."

Kuna utafiti ulifanyika katika mahakama za Zanzibar kutazama kesi na mashauri ambayo Mwarabu na Mwafrika walihusika.

Watafiti wakaangali endapo kuna mahali hukumu ilitolewa kwa upendeleo.

Matokeo yalionyesha kuwa hapakuwa na kesi hata moja ambayo hukumu ilimpendelea Mwarabu.

Sasa tutazame hali ilikuwaje baada ya mapinduzi.

Haihitaji kuingia katika mahakama kwa sababu inajulikana kuwa mahakama zilikufa na watu wengi waliuawa na wanafahamika kwa majina.

Wauaji na watesaji watu halikadhalika wanajulikana.

Jambo la ajabu ni kuwa ASP walianza pia kuuana wenyewe kwa wenyewe.

Zanzibar suala la dini halina nafasi katika kufanyiana ubaya kwani wote ni Waislam.
 
@TODAYS
Swali hili ingependeza lijibiiwe na ASP kwa sababu Hanga alikuwa kiongozi wao na dunia inamtambua kuwa ndiye aliyepanga mipango yote akishirikiana na Oscar Kambona.
Mkuu nikipata nafasi tena kuja Unguja nitapitia pale maskani ya CUF ngome kongwe niulize hilo swali, lakini lazima nijihakikishie usalama, maana Zanzibari bana mguu nje mguu ndani!.
 
Mzee wangu hili swali ni kubwa sana ila unalijibu kihuni

Nisamehe kutumia neno hilo
Ila ni ukweli

Niambie ni tafiti gani na kafanya nani usiishie kusema ni tafiti tu

Ni wazimu usiosameheka kutetea tawala dhalimu ya kisultan kwa kujificha kwenye kichaka chenye nyasi kavu cha dini ati kulikuwa na usawa baina ya weusi, wa brown (waarabu na wahindi) na wazungu

Ninauliza kwa mara ya mwisho

Hakukuwa na ubaguzi wa rangi na uonevu systematically kwa wenyeji wa visiwa vile?

Kulikua na umiliki sawa wa ardhi kati ya wenyeji na wageni?

Kulikua na umiliki sawa wa watumwa kati ya wenyeji na wavamizi?

Kulikuwa na mgawanyo sawa wa nyenzo za uzalishaji mali kati ya wenyeji na wavamizi?

Hawa washenzi waliokimbia mitafaruku huko kwao na kuloweza katika visiwa vyetu waki take advantage ya uduni wa wenyeji na kujisimika kama watawala
Halali wakawadhalilisha wenyeji wanawezaje kuonewa huruma?
 
Kama unajua chochote kuhusu siasa na human nature hutatenganisha kilichotokea south sudan na hayo wanayoyatengeneza unguja na pemba
Wanayatengeneza lakini ni vigumu sana , maana hapo ni kugombanisha familia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…