Kua nchi huru ya waarabu na machotara tu na sio wabantu alisia!!!Maana mihadhara yao ya kuponda mapinduzi wanaaita watu wa bara"Machogo"
sasa kwanini hao wabantu asilia ndio wanaoongoza hiyo mihadhara?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kua nchi huru ya waarabu na machotara tu na sio wabantu alisia!!!Maana mihadhara yao ya kuponda mapinduzi wanaaita watu wa bara"Machogo"
Kisingizio hili kitakuwa justified endapo tutaona hakukua na utumwa wala ubaguzi dhidi ya wenyeji Zanzibar vinginevyo mzee wetu atakuwa anakosea na kutukosea sana wazanzibarHii mind set ya Oman oriented anayo mzee wangu said mohamed kwa kisingizio cja unasaba wa kindugu na kidini
Sina shaka wewe mzee wetu ni mtaalam wa maswala ya ZanzibarNelson...
Ukweli haukataliki muhimu ni kuwa uwe kweli ni ukweli.
Lakini ni muhimu ujue kuwa kuna propaganda nyingi katika historia ya utumwa.
Unazungumza utumwa Zanzibar lakini umekuwa kimya kuhusu Transatlantic Slave Trade.
Yawezekana huna ujuzi wala maarifa ya historia hii.
Ninapokusoma jinsi unavyoandika na hata pale ninapokuongoza katika kanuni za uandishi unakuwa mkaidi na kurejea katika makosa yale yale basi najua kuwa hapa hakuna kitu.
Sultan kaondoka Zanzibar hana damu katika vidole vyake.
Jela za mateso na mauaji ziliingia Zanzibar baada ya mapinduzi.
Historia ya jela hizi Wazanzibari wote wangependa kusahau.
Wazanzibari wameukataa utawala ulioko madarakani toka 1964 kwenye sanduku la kura mara sita kuanzia 1995.
Nakupa yote haya kwa ushahidi na jambo la kusikitisha maraisi wote hao wameshindwa na mgombea yule yule mmoja.
Kilele cha fedheha hii ni pale baada ya kushindwa wa 2015.
Uchaguzi ule ukafutwa.
Kila uchaguzi damu ya Wazanzibari inamwagika.
Wewe unakuja na lugha "Wabantu hatusahau."
Wajue kwanza Wazanzibari ni nani.
Ndipo nikakuuliza nini tafsiri ya CCM kushindwa kila uchaguzi?
Wazanzibari wanayakataa mapinduzi?
Huenda hadi hapa tulipo hujanijua labda ungenijua ungechukua tahadhari lau kidogo.
Nimeshiriki katika uandishi wa historia ya mapinduzi nikiwa Mtafiti Msaidizi wa Dr. Harith Ghassany.
Mradi huu ulichukua miaka saba kukamilika.
Kitabu kutokana na utafiti huu kipo mtandaoni bure, "Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru."
Dr. Ghassany haitaji kuelezwa.
Nimealikwa Zanzibar mara nne kufanya mihadhara ya wazi kuhusu historia ya Zanzibar:
Zanzibar State University, Mwinyi Baraka Foundation, na mara mbili na Zanzibar Institute of Research and Public Policy (ZIRPP) kufanya pitio kwa vitabu viwili kuhusu historia ya mapinduzi.
Nimezungumza kuhusu kitabu cha Hashir Seif Hashir: "Mimi Umma Party na Mapinduzi ya Zanzibar," na kitabu cha Khamis Abdulla Ameir, "Maisha Yangu."
![]()
![]()
HaijalishiMapinduzi hayakutokea ndani yalimalizia tu ndani, Na hapo ndipo matatizo yote yanapoanzia.
Nani ananyonywa na nani?Bila ya hata aibu unajisifia ukandamizaji na unyonyaji.
Sijasema hivyo hebu soma tena halafu komentikwahiyo hadithi za ukweli zinasimuliwa na Wakristo?
Mzee experience inatuonesha yanayoendelea south sudan toka 2011Baharia...
Mdomo haumkatai bwana wake.
Wapemba na Waunguja wamekuwapo toka dunia ilipoumbwa na hayo anayosema Nyerere hayakutokea.
Haijalishi
Uhalali au uharamu wake ni je, Sultan na mfumo wake waliwakandamiza walio wengi au la?
Mkuu twende sawa, hali ya kiuchumi kwa matabaka yote matatu Zanzibar enzi za sultan ilikuaje?
Kulikuwa na usawa? Ama tabaka fulani lilipendelewa huku jingine lilikandamizwa systematically?
Ungenijibu swali kwanza kisha ukauliza swali twende sawakwani mfumo wa CCM haukandamizi walio wengi?
Jibu swali kama hujui unasema hujuiacha kukariri hadithi za ovyo.
Sisi ASP tunajua zaidi na wewe hujui zaidi kuhusu mapinduzi matukufu ndugu yangu!!!Hayo ni maneno yako
Today,Kwa nini hatajwi?
Kisingizio hili kitakuwa justified endapo tutaona hakukua na utumwa wala ubaguzi dhidi ya wenyeji Zanzibar vinginevyo mzee wetu atakuwa anakosea na kutukosea sana wazanzibar
Tunaongelea Unguja na PembaMzee experience inatuonesha yanayoendelea south sudan toka 2011
Count...Sina shaka wewe mzee wetu ni mtaalam wa maswala ya Zanzibar
Ila
Nina swali moja tu
Enzi za sultan ambae ‘hakuwa na damu vidoleni mwake’ hakukuwa na ubaguzi wala matabaka?
Kulikuwa na haki kwa wakazi wote wa Zanzibar bilq kujali rangi wala dini zao?
Kama unajua chochote kuhusu siasa na human nature hutatenganisha kilichotokea south sudan na hayo wanayoyatengeneza unguja na pembaTunaongelea Unguja na Pemba
Mkuu nikipata nafasi tena kuja Unguja nitapitia pale maskani ya CUF ngome kongwe niulize hilo swali, lakini lazima nijihakikishie usalama, maana Zanzibari bana mguu nje mguu ndani!.@TODAYS
Swali hili ingependeza lijibiiwe na ASP kwa sababu Hanga alikuwa kiongozi wao na dunia inamtambua kuwa ndiye aliyepanga mipango yote akishirikiana na Oscar Kambona.
Mzee wangu hili swali ni kubwa sana ila unalijibu kihuniCount...
"Haki kwa wakazi wote bila kujali rangi wala dini."
Kuna utafiti ulifanyika katika mahakama za Zanzibar kutazama kesi na mashauri ambayo Mwarabu na Mwafrika walihusika.
Watafiti wakaangali endapo kuna mahali hukumu ilitolewa kwa upendeleo.
Matokeo yalionyesha kuwa hapakuwa na kesi hata moja ambayo hukumu ilimpendelea Mwarabu.
Sasa tutazame hali ilikuwaje baada ya mapinduzi.
Haihitaji kuingia katika mahakama kwa sababu inajulikana kuwa mahakama zilikufa na watu wengi waliuawa na wanafahamika kwa majina.
Wauaji na watesaji watu halikadhalika wanajulikana.
Jambo la ajabu ni kuwa ASP walianza pia kuuana wenyewe kwa wenyewe.
Zanzibar suala la dini halina nafasi katika kufanyiana ubaya kwani wote ni Waislam.
Wanayatengeneza lakini ni vigumu sana , maana hapo ni kugombanisha familiaKama unajua chochote kuhusu siasa na human nature hutatenganisha kilichotokea south sudan na hayo wanayoyatengeneza unguja na pemba