Wanaochukia mapinduzi matukufu ya Zanzibar 1964 wana ajenda gani nyuma ya pazia?

Kaka capone unatoa hoja kisomi na kwa weledi wa hali ya juu kisiasa!!!Nakuelewa kaka
 
Mzee wangu nahisi unanizungumzia mimi😂
Na kama si mimi niambie nikae chonjo😂

Ila kama ni mimi ninayo ya kukuambia

Kwenye falsafa kuna fallacy katika kutengeneza hoja tunaiita appeal to authority fallacy

Hapa ni mtu anajenga hoja akijibasibisha na ufahamu wake au uzoefu ktk kada fulani

Sasa hapa kuna ka loophole, mtu huyu anaweza tumia uchochoro huu kuwalisha matangopori watu wengine ati kisa ni alifanya hili na lile

Mimi ninataka tuifikie kweli ya kweli ndiyo maana vitabu na majarida yako nimeyaweka kando ninadeal na hoja zako tu

Sasa nilipotoa majarida yako na historia yako nikakuacha na hoja pekee katika hoja zako mpaka sasa sijaona jambo lolote la maana

1. Umeshindwa jibu swali la msingi
Kulikuwa na haki kati ya matabaka yote enzi za sultan?

Hujajibu badala yake unauliza swali

Nikakupa njia kuwa nitajibu swali lako endapo utajibu langu lkn bado hujajibu

Sasa nikawaza majarida vitabu na wasifu unaosema unao unafaa nini kama unashindwa kujibu swali jepesi kama hilo?

Nikaona ya nini nibabaike na wasifu wako ikiwa huwezi jibu swali jepesi sana kama hili?

Ndipo nikaona aidha unalipwa na kufanya propaganda za kimakusudi kuturudisha enzi za utumwa wa sultan au wasifu wako si chochote ila uzushi, mpaka sasa sijapata jibu sahihi kati ya hayo mawili,
 
Hii ni Qur'an.
Amerehemewa yule atakaejiepusha na ubishi hata kama atakuwa kwenye haki.
 

Mzee said waga anakwepa maswali haya!!!!Yeye anaamini sultan alikua anagawa maziwa na asali na kwa sababu ya udini hataki kutambua udhalimu wa walowezi wa kiarabu kwa ndugu zetu wa kibantu
 
Hii ni Qur'an.
Amerehemewa yule atakaejiepusha na ubishi hata kama atakuwa kwenye haki.
Abu Ghifar ktk hadithi sahih alisema aliwahi msikia Mtume (saw) akisema akisema “sema ukweli hata kama mchungu”

Na pia Abuu said al khudree amepokea hadith sahih toka kwa mtume isemayo tunapoona uovu na tuuondoe kwa mikono yetu, ikiwa hatuwezi, tuukemee kwa vinywa vyetu na ikiwa hatuwezi basi tukae kimya na tuuchukie kwa mioyo yetu na Mtume (saw) anasema kukaa kimya ni udhaifu katika imaan

Yote inaonesha Uislam si kichaka cha kuficha uovu hata afanye nani
 
Mzee said waga anakwepa maswali haya!!!!Yeye anaamini sultan alikua anagawa maziwa na asali na kwa sababu ya udini hataki kutambua udhalimu wa walowezi wa kiarabu kwa ndugu zetu wa kibantu
Mkuu binafsi sina shida nae

Alete madai yote atakayo ila athibitishe tu

Yakithibitika kuwa ni kweli nitaungana nae ktk kupigia chapuo usultan Zanzibar 😂
 
Mzee said waga anakwepa maswali haya!!!!Yeye anaamini sultan alikua anagawa maziwa na asali na kwa sababu ya udini hataki kutambua udhalimu wa walowezi wa kiarabu kwa ndugu zetu wa kibantu
Nelson...
Unafurahisha kwa namna yako ya pekee kabisa.
 
Nelson...
Basi wewe ndiyo wa kunihoji mimi kwa historia usioijua?
Wewe unakuja kwangu kusoma siyo kuhoji.

Una chochote cha kuonyesha kuwa unajua unachohoji kwangu?
Sasa hapo ndipo
Unapokosea mzee wetu😂

Kwanini usitake kuhojiwa?
Mitume ilihojiwa kwanini watu waje kwako kusoma kibubusa?

Chuoni tunahoji tena sana kwanini utake kufundisha watu bila
Kuhoji??
Unakimbia nini mzee?

Ninavyojuq msomi haogopi kuhojiwa na akihojiwa hachukulii vitu personal anajibu hoja kama ilivyoulizwa msomi hajivuni eti hahojiwi na nini hapana

Wasomi wanakaribisha hoja wanataka kuhojiwa nakumbuka nilipokuwa UDSM kuna Profesa wetu wa Public Administration alikuwa ni Prof. Malya alikua akituhamasisha tumhoji tusikae kae tu kukubali kila tunachoambiwa mzee

Kama unachosema ni kweli kubali kuhojiwa na unapohojiwa jibu hoja kwa hoja usikimbie hoja kwa kutuonesha picha na kuhama mada mzee wetu
 
Kaka capone unatoa hoja kisomi na kwa weledi wa hali ya juu kisiasa!!!Nakuelewa kaka
Hizi asilimia ni kwa mujibu wa tafiti gani ?
Nelson...
Waraka huo hapo chini:

 
Upo sahii mzee wangu Said mohamed hapendi kuhojiwa kabisa ila anapenda kuzungimza tu upande wa mitazamo yake ya kisiasa na kiimani
Ni kweli mkuu kuna post yake humu kamjibu mtu eti anadai “wewe ndio wa kunihoji?”

Binafsi nimeshtuka sana nikahisi
Amekosea

Ni msomi gani zama hizi anathubutu kukataa kuhojiwa?
Yani inachekesha inanitia mashaka ana agenda gani mzee wetu

Na wanafunzi wake wanawezaje kusoma bila kuhoji yani wanaelewaje sasa aaargh

Nimesikia kero sana leo

Msomi hutaki kuhojiwa??

Kuna kitu tunaita intellectual honesty sasa bila kuhoji tutakipata wapi kwa mzee wetu?
 
Sasa nitauamini vipi waraka huu wakati umeanza salamu tu kwa mrengo flani wa kiafidhina upande wa itikadi za kisiasa na kiimani!!!Napata shida kidogo kuamini huu ni waraka wa mawazo na maoni huru yasiyo ns chembechembe za kiitikadi za kisiasa na kiimani?????
 
Hata mimi kaniambia siwezi kumuhoji kuhusu zanzbar sababu yeye kazaliwa kkoo na ana ubini wa kindugu na kiimani na wafuasi wa hizbu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…