Sultan...
Niruhusu nizungumze na wewe kuhusu shida lakini kwa kitu kingine baadae nitakujibu In Shaa Allah kuhusu mapinduzi.
Kuna mtu kaniuliza kwa nini simjibu mtu fulani (kataja identify yake) ilhali yeye akimsoma na akinitazama mimi hana makamo yoyote.
Nikamwambia nimemjibu, "Ahsante."
Akaniambia hilo si jibu umemshukuru.
Nikamwambia naam nimemshukuru na hiyo shukurani yangu kwake ndiyo jibu langu.
Nikamwambia kuwa ningemjibu kwa kumjibu maneno yake ningemuongezea ghadhabu na hili ni vizuri kuliepuka.
Huyu ndugu yetu moyo wake umejaa hasad na husda ni sumu inayokula kiwiliwili na ni kitu hatari.
Nikamwambia huyu ndugu yangu tupitie pamoja yote aliyoniandikia nami nikakaamua kuwa kimya na nikamshukuru.
Tukafanya hivyo.
Nikamuuliza nini alichokiona.
Jibu alilonipa kasema hakika huyu ni hasid.
Nikamuuliza kwa nini unamwita hivyo akasema, "Yote uliyotueleza na kutuonyesha kwa nia nzuri tuelewe na jibu ulilompa la kuwa si kila kitu unaweza kupata yakini yake ijaza yake ni kukutolea fedhuli?
Mbona yeye hatuwekei aliyofanya katika medani ya usomi?"
Sasa nikamjibu huyu ndugu yangu kuwa na hasad ndani ya moyo wake imefunika yote ambayo kwayo mimi yameniweka juu kileleni.
Husda yake inamuonyesha kile kitu kidogo kisichokuwa na maana yoyote.
Akaona ijaza yangu ni hayo maneno ya kejeli kwa sababu kaumizwa na kile ambacho yeye hana Allah bado hajampa.
Husda inamfanya aamini kuwa yeye hawezi kupata nilichopewa mie.
Kama kawaida ya mahasidi
wote hakuweza kustahamili akakitapika kile kinachomchoma - kuhadhiri kwangu Vyuo Vikuu, Afrika, Ulaya na Marekani na mengineyo.
Kuandika vitabu na kuchapwa na wachapaji wa sifa duniani.
Si kila mwandishi kazi yake inachapwa na Oxford University Press.
Si kila kitabu kinapewa nafasi ndani ya Cambridge Journal of African History.
Walimu wangu walionisomesha mimi hawajaingia ndani ya majarida ya kimataifa.
Anasema yeye haya kuwanayo mimi hayamshughulishi.
Lakini ukweli ni kuwa yote anayoyaona kwangu kwa ushahidi wenye ithibati yanamchoma.
Kashindwa kustahamili.
Alikuwa kimya lakini kapata upenyo kaona autumie kutema nyongo yake.
Vitabu vyote na "paper" zote nilizoweka hapa basi ziwe si lolote kwa kumdokolea tafiti moja tu ya kimya?
Turudi kwenye mapinduzi.
Zanzibar imetulia na In Shaa Allah itavuka huu mtihani.
Wazanzibari wamekubaliana kuwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).
Agenda ya Wazanzibari ni kukubaliana kuwa na uchaguzi huru na wa haki.
Hawako mbali kufikia lengo hili.
(Ndugu yangu uliyeniomba nitoe jibu nimefanya kama ulivyosisitiza nifanye).
Mzee wangu nahisi unanizungumzia mimi😂
Na kama si mimi niambie nikae chonjo😂
Ila kama ni mimi ninayo ya kukuambia
Kwenye falsafa kuna fallacy katika kutengeneza hoja tunaiita appeal to authority fallacy
Hapa ni mtu anajenga hoja akijibasibisha na ufahamu wake au uzoefu ktk kada fulani
Sasa hapa kuna ka loophole, mtu huyu anaweza tumia uchochoro huu kuwalisha matangopori watu wengine ati kisa ni alifanya hili na lile
Mimi ninataka tuifikie kweli ya kweli ndiyo maana vitabu na majarida yako nimeyaweka kando ninadeal na hoja zako tu
Sasa nilipotoa majarida yako na historia yako nikakuacha na hoja pekee katika hoja zako mpaka sasa sijaona jambo lolote la maana
1. Umeshindwa jibu swali la msingi
Kulikuwa na haki kati ya matabaka yote enzi za sultan?
Hujajibu badala yake unauliza swali
Nikakupa njia kuwa nitajibu swali lako endapo utajibu langu lkn bado hujajibu
Sasa nikawaza majarida vitabu na wasifu unaosema unao unafaa nini kama unashindwa kujibu swali jepesi kama hilo?
Nikaona ya nini nibabaike na wasifu wako ikiwa huwezi jibu swali jepesi sana kama hili?
Ndipo nikaona aidha unalipwa na kufanya propaganda za kimakusudi kuturudisha enzi za utumwa wa sultan au wasifu wako si chochote ila uzushi, mpaka sasa sijapata jibu sahihi kati ya hayo mawili,