Waachie Wazanzibari waiseme wenyewe,
Mwanzo umesema Zuluma/zulma ukasahihiswa, sasa hivi umesema Dhuluma, mimi si Mzanzibari ila kwa Lafudhi tu yako naona wewe sio Mzanzibari.
Haimake sense kwa mtu anatoka bara mambo yanayoendelea pwani yanamuuma sana kuliko watu wa pwani wenyewe.
Na huu uongo munaoupakaza unadudumiza Taifa, Hao masultani wa Zanzibar ni pride ya Nchi wafundisheni watoto mashuleni waambieni pia sio wote walikuwa waarabu walikuwepo weusi pia.
Hizi Propaganda zenu zinafanya watu kuwa na mentality ya kitumwa, mtoto toka kazaliwa anaambiwa babu yako mtumwa, mweusi hana IQ, Mweupe ana Akili etc hizi blah blah zenu zimetengeneza Nchi isio na Confidence na isiyojiamini.
Ila mungefundisha Historia ya Ukweli, kwamba wakanda sio Finction tu bali kulikuwepo watu weusi na walikuwa Wafalme waliongoza na walikuwa na Elimu ya Hali ya Juu.
Nimekupa Mfano wa huyo Humudi, Sio tu Alikuwa Sultan Mweusi wa Zanzibar, Jamaa alisoma Uingereza na Ana Tuzo kibao za Elimu alikuwa Kichwa, mifano ya Tuzo zake kama
- King Edward VII Coronation Medal-1902
- Special Class in brilliants of the Nishan-e-Osmanieh of the Ottoman Empire-1905
- Grand Cross of the Order of the Crown of Italy-1905
- Grand Cross of the Order of the Red Eagle, 1st Class of Prussia-1905
- Grand Cross of the Order of the Immaculate Conception of Vila Viçosa of Portugal-1905
- King George V Coronation Medal-1911
Prussia (Ujerumani), Italy, Uingereza, Ottoman (Uturuki), Portugal kote jamaa ana Tuzo, mtu kama Huyu ndio wewe mtu mweusi ulitakiwa umjue, ila munawaficha na kuwaita masultan waovu, badala yake mnafundisha watoto kwamba wahenga wenu ni kina Mangungo.