Wanaochukia mapinduzi matukufu ya Zanzibar 1964 wana ajenda gani nyuma ya pazia?

Wanaochukia mapinduzi matukufu ya Zanzibar 1964 wana ajenda gani nyuma ya pazia?

Waachie Wazanzibari waiseme wenyewe,

Mwanzo umesema Zuluma/zulma ukasahihiswa, sasa hivi umesema Dhuluma, mimi si Mzanzibari ila kwa Lafudhi tu yako naona wewe sio Mzanzibari.

Haimake sense kwa mtu anatoka bara mambo yanayoendelea pwani yanamuuma sana kuliko watu wa pwani wenyewe.

Na huu uongo munaoupakaza unadudumiza Taifa, Hao masultani wa Zanzibar ni pride ya Nchi wafundisheni watoto mashuleni waambieni pia sio wote walikuwa waarabu walikuwepo weusi pia.

Hizi Propaganda zenu zinafanya watu kuwa na mentality ya kitumwa, mtoto toka kazaliwa anaambiwa babu yako mtumwa, mweusi hana IQ, Mweupe ana Akili etc hizi blah blah zenu zimetengeneza Nchi isio na Confidence na isiyojiamini.

Ila mungefundisha Historia ya Ukweli, kwamba wakanda sio Finction tu bali kulikuwepo watu weusi na walikuwa Wafalme waliongoza na walikuwa na Elimu ya Hali ya Juu.

Nimekupa Mfano wa huyo Humudi, Sio tu Alikuwa Sultan Mweusi wa Zanzibar, Jamaa alisoma Uingereza na Ana Tuzo kibao za Elimu alikuwa Kichwa, mifano ya Tuzo zake kama

  • King Edward VII Coronation Medal-1902
  • Special Class in brilliants of the Nishan-e-Osmanieh of the Ottoman Empire-1905
  • Grand Cross of the Order of the Crown of Italy-1905
  • Grand Cross of the Order of the Red Eagle, 1st Class of Prussia-1905
  • Grand Cross of the Order of the Immaculate Conception of Vila Viçosa of Portugal-1905
  • King George V Coronation Medal-1911
Prussia (Ujerumani), Italy, Uingereza, Ottoman (Uturuki), Portugal kote jamaa ana Tuzo, mtu kama Huyu ndio wewe mtu mweusi ulitakiwa umjue, ila munawaficha na kuwaita masultan waovu, badala yake mnafundisha watoto kwamba wahenga wenu ni kina Mangungo.
Uzi unasema wanaopinga mapinduzi wana ajenda gani nyuma ya pazia!!Kama unapinga mapinduzi matukufu ya 1964 kua muwazi tu!!!!!
 
Kaka huu uzi niliuweka kujadili mapinduzi matukufu ya 1964 na wale wanayoyapinga!!!!Mzee wangu saidi anaelewa!!!!Sitegemei mchango wowote wenye tija kutoka kwako!!!!Sababu wewe ni masalia ya hizbu!!!!
Kwani waliounda Hizbu ni Waarabu?
Hiyo ASP kwani ilikuwa na watu weusi tu ilikuwa haina Waarabu na makabila mengine ??
Kanisa limekunywesha mvinyo nyeusi unaona kila kitu ni cheusi 😝😝😝
 
Kaka huu uzi niliuweka kujadili mapinduzi matukufu ya 1964 na wale wanayoyapinga!!!!Mzee wangu saidi anaelewa!!!!Sitegemei mchango wowote wenye tija kutoka kwako!!!!Sababu wewe ni masalia ya hizbu!!!!
Hii sio mara ya kwanza kulumbana na wewe tatizo lako huna hoja, ukiletewa hoja huna hoja za kupangua badala yake unaleta personal attack.

Jioni njema
 
Ukweli mchungu mzee wangu ila umeze tu!!!Hizo nasaba za undugu na udini zisikuzibe macho uukatae ukweli
Kwani Nyerere alipinduliwa na wanajeshi wa kiarabu au wa kilowezi wa kiarabu? Waliomrejesha madarakani si wale wakristo wakoloni wa kizungu? Kwa nini wakamrudisha madarakani?
 
Waliofanya Mapinduzi ni kikundi cha watu wachache kilichoshindwa kwenye Kura halali zilizopigwa na Wazinzibari...
Asante kaka kwa mtazamo wako!!!!Sisi ndio mazalia ya hao watu wachache waliomuondoa mlowezi wa kiarabu na washirika wake madarakani!!!!!
 
Hii sio mara ya kwanza kulumbana na wewe tatizo lako huna hoja, ukiletewa hoja huna hoja za kupangua badala yake unaleta personal attack.

Jioni njema
Sasa baba mwajuma wewe ni mpinga mapinduzi lazima uwatetee hizbu!!!!Mimi ni msema kweli kuhusu dhuluma za walowezi wa kiarabu kabla ya mapinduzi matukufu 1964
 
Sasa baba mwajuma wewe ni mpinga mapinduzi lazima uwatetee hizbu!!!!Mimi ni msema kweli kuhusu dhuluma za walowezi wa kiarabu kabla ya mapinduzi matukufu 1964
Hili jeshi lenu mnalolileta wakati wa kila uchaguzi kupindua matakwa ya waafrika Wapiga kura ndiwo Wapinga Mapinduzi na nyinyi ndio mliowauwa Mdungi Usi, Hänga, Jaha Ubwa , Othman Sharifu , Twala nk
 
Hao ni mabaki ya sultani,wanaitwa waarabu koko,
Sawa kabisa. Ni wale waarabu koko. Walikua daraja la pili enzi ya sultani. Yaani baada ya waarabu na wahindi wao ndio wanafuata kwa hadhi. Hao machotara wakiwa wazao wa dada zetu waafrika wakiingiliwa kwa kubakwa na waarabu. Wanajiona eti ni waarabu na ndio wazanzibari halisi. Waliyokua wengi waarika na ambao walikua watumwa wanawaona ni watu duni wageni kutoka bara.
 
Ukweli mchungu mzee wangu ila umeze tu!!!Hizo nasaba za undugu na udini zisikuzibe macho uukatae ukweli
Nelson,
Jitahidi sana kuandika na kufanya mjadala kwa ustaarabu.

Unaandika ukiwa umekasirika.

Lugha za "ukweli mchungu," ''umeze tu,' "kuziba macho";si lugha za mahojiano ya kisomi.

Najaribu kuzungumza na nafsi yako ya ndani ili tujuane.

Nimekuambia najua mengi nikiamini utaelewa na utakuwa tayari kunufaika na mimi.

Lakini naona hujaelewa.

Dini ni muhimu sana kwa siasa za Tanganyika nchi yenye Waislam na Wakristo.

Wanayoiogopa dini yaani Uislam katika historia ya Tanganyika ni Wakrito na sababu zinatahamika.

Lakini ukweli ni kuwa Waislam wana historia kubwa katika mapambano na Wajerumani na Waingereza.

Waislam wamechukua nafasi kubwa katika maisha ya Nyerere.

Ukikataa kuwasikia Waislam katika historia ya Tanganyika ni kuwa unataka kufuta historia ya kweli.

Zanzibar ni nchi ya Kiislam labda 99%.

Wakati wa muungano 1964 Uislam haukuwa na nguvu katika siasa za Zanzibar.

Hali imebadilika sana.

Wazanzibari sasa wanajitambua kama taifa la Kiislam.

Ndiyo haya mabadilko unayoyaona.
In Shaa Allah tutalijadili hili huko mbele.

Muhimu tuwe na mjadala wa adabu.
 
Back
Top Bottom