Wanaofanyakazi ya kupamba kumbi za starehe, kusherehesha (Ma-MC), wapishi wa sherehe na wapiga picha, watatakiwa kulipa ada na ushuru

Mkuu Yaani wewe Tii sheria za nchi bila masharti
Lipa kodi
Utafaidi sana
Vinginevyo utaumia maana maana mianya ya wapiga dili imeziba kabisa
Hakuna asiyependa kulipa kodi mkuu tatizo kodi kubwa na zinaumiza... fikiria kuna baadhi ya kumbi ndogo za kawaida mc analipwa 50k halafu unamwambie huyo mc alipe tozo ya 50k inaingia akilini kweli.?? Yaana afanye kazi hela yote serekali ichukue?
Kuna biashara zina kodi na tozo zaidi ya 4 unafikiri kuna kufaidi au kuumia?
 
Kama wamefuata hata maiti watashindwa kanisani??
 
Mnyonge ni mtu ambaye,hajitambui,mjinga ,legelege ,au zuzu,na unaweza kugeuzwa vyovyite atakavyo,
Acha waendelee kiitwa wanyonge huku wakishangilia na kupiga makofi.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Unapaswa kupimwa akili...nadhani kuna shida mahali...aidha kichwan au tumboni
 
Sasa huyo mc analipwa 50k tozo yake sasa atoe 50k abaki na nini?
Wapishi wanalipwa mpaka 70k sasa tozo 30k mnataka nn nyie maCCM??
Hapo mwenye ukumbi ashalipa kodi na tozo nyingine
Gharama za huduma zao zitapanda kodi itabebwa na mtumiaji.
 
Hao MA mc wanatakiwa walipwe zaidi ili wawaze kulipa kodi ya nchi
Nchi haiwezi kuendeshwa bila kodi
 
WATU wanaofanyakazi ya kupamba kumbi za starehe, kusherehesha (Ma-MC), wapishi wa sherehe na wapiga picha, watatakiwa kulipa ada na ushuru.

Ni baada ya Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema jijini Mwanza, kupitisha sheria ndogo za ada na ushuri ambazo tayari zimepata baraka za Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

Barua iliyosainiwa na Emmanuel Kaponoke, Afisa Utamaduni wa halmashauri hiyo ya tarehe 15 Januari 2021 kwenda kwa walengwa, inabainisha ada hizo.

Washereheshaji (MC) watapaswa kulipa Sh.50,000 kwa sherehe moja huku wapambaji kumbi za burudani/sherehe watalipa Sh.30,000.

Wamiliki wa kumbi, unaochukua watu kati ya 100-200 ni Sh.50,000 kwa siku, ukumbi unaochukua watu kati ya 201-500 atalipa Sh.100,000.

Wapishi wa vyakula kwa siku moja ya tukio atapaswa kulipa Sh.30,000 na wapiga picha za video na mnato watapaswa kulipa Sh.30,000 huku muziki ikiwa ni Sh.30,000

“Kamwe, mmiliki wa ukumbi asiruhusu sherehe kufanyika ndani ya ukumbi wake bila kibali cha halmashauri,” inaeleza sehemu ya barua hiyo

“Ikumbukwe, ada hii ni kwa ajili ya kubali cha halmashauri tu na si gharama ya kukodi ukumbi.”

 
55555[emoji847][emoji847][emoji847][emoji106][emoji106][emoji106]
 
Nakumbuka kuna Mc tulimlipa 50,000/= nadogo alifanya poa tu kiroho safi sasa leo hii ikitakiwa nae aanze kulipa kodi 50,000/= itabidi nae apandishe afanye laki ili alipe 50 nayy abaki na 50
Yes! Namba zimechapwa ukutani, na zisomwe na watu wote. Muiskiapo sauti ya baragumu, na kinubi, na kinanda, na tarumbeta wote muanguke kifudifudi - heshima kwa mfalme. Ole wake atakayekaidi agizo hili; pahala pake ni katika tundu ya simba.
 
Kwa sengerema ninayoijua kuna mc mpaka 70k sasa hapo akilipa hiyo tozo anabaki na kiasi gani?

Hapo bado mwenye ukumbi ana ada kodi na tozo anazolipa yeye kama yeye. Saaa huu mrundikano wa matozo sijui wanataka tusibaki hata na 100 mfukoni?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…