Wanaofanyakazi ya kupamba kumbi za starehe, kusherehesha (Ma-MC), wapishi wa sherehe na wapiga picha, watatakiwa kulipa ada na ushuru

Wanaofanyakazi ya kupamba kumbi za starehe, kusherehesha (Ma-MC), wapishi wa sherehe na wapiga picha, watatakiwa kulipa ada na ushuru

Nakumbuka kuna Mc tulimlipa 50,000/= nadogo alifanya poa tu kiroho safi sasa leo hii ikitakiwa nae aanze kulipa kodi 50,000/= itabidi nae apandishe afanye laki ili alipe 50 nayy abaki na 50
Kuna sherehe mnaamua mjomba au kaka mtu awe mc na hamumlipi. Madada na mashangazi wawe wapishi kubana bajeti sasa na wao watalipa au vipi? Au nao wakakate leseni sasa

Nchi ina vituko hii na mpaka mkome
 
Tujenge nchi yetu kwa makusanyo ya fedha za ndani...
 
Yes! Namba zimechapwa ukutani, na zisomwe na watu wote. Muiskiapo sauti ya baragumu, na kinubi, na kinanda, na tarumbeta wote muanguke kifudifudi - heshima kwa mfalme. Ole wake atakayekaidi agizo hili; pahala pake ni katika tundu ya simba.
Asije tu kukosa usingingizi akadamka asubuhi na mapema nakuanza kuita Kwa mbali Dudus Dudus je Mungu unayemtumaini ameweza kukuokoa na makang'wa ya simba?
 
WATU wanaofanyakazi ya kupamba kumbi za starehe, kusherehesha (Ma-MC), wapishi wa sherehe na wapiga picha, watatakiwa kulipa ada na ushuru.

Ni baada ya Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema jijini Mwanza, kupitisha sheria ndogo za ada na ushuri ambazo tayari zimepata baraka za Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

Barua iliyosainiwa na Emmanuel Kaponoke, Afisa Utamaduni wa halmashauri hiyo ya tarehe 15 Januari 2021 kwenda kwa walengwa, inabainisha ada hizo.

Washereheshaji (MC) watapaswa kulipa Sh.50,000 kwa sherehe moja huku wapambaji kumbi za burudani/sherehe watalipa Sh.30,000.

Wamiliki wa kumbi, unaochukua watu kati ya 100-200 ni Sh.50,000 kwa siku, ukumbi unaochukua watu kati ya 201-500 atalipa Sh.100,000.

Wapishi wa vyakula kwa siku moja ya tukio atapaswa kulipa Sh.30,000 na wapiga picha za video na mnato watapaswa kulipa Sh.30,000 huku muziki ikiwa ni Sh.30,000

“Kamwe, mmiliki wa ukumbi asiruhusu sherehe kufanyika ndani ya ukumbi wake bila kibali cha halmashauri,” inaeleza sehemu ya barua hiyo

“Ikumbukwe, ada hii ni kwa ajili ya kubali cha halmashauri tu na si gharama ya kukodi ukumbi.”

Mbona waokota makopo wanarukwa??????
 
Nakumbuka kuna Mc tulimlipa 50,000/= nadogo alifanya poa tu kiroho safi sasa leo hii ikitakiwa nae aanze kulipa kodi 50,000/= itabidi nae apandishe afanye laki ili alipe 50 nayy abaki na 50
Hizo gharama unalipa wewe mwenye sherehe ili upate kibali ndo uruhusiwe kufanya hiyo sherehe.
 
Asije tu kukosa usingingizi akadamka asubuhi na mapema nakuanza kuita Kwa mbali Dudus Dudus je Mungu unayemtumaini ameweza kukuokoa na makang'wa ya simba?
teh! teh! teh! Kuna mmoja alipoona maandishi ukutani fahamu zikamruka; akaita wanajimu na waganga wote wa nchi ile wamfasirie maana yake ni nini mwandiko ule wasiweze! Akaja kijana mmoja mdogo tu mpakwa mafuta wa Bwana akadadavua mistari ile kwa uzamivu wa ajabu kabisa.

Usiku ule ule mfalme akararuliwa; mzoga wake ukawa sherehe ya tai na fisi na hayawani wengine wakafaidi mzoga wa mfalme maporini mbali huko.
 
teh! teh! teh! Kuna mmoja alipoona maandishi ukutani fahamu zikamruka; akaita wanajimu na waganga wote wa nchi ile wamfasirie maana yake ni nini mwandiko ule wasiweze! Akaja kijana mmoja mdogo tu mpakwa mafuta wa Bwana akadadavua mistari ile kwa uzamivu wa ajabu kabisa.

Usiku ule ule mfalme akararuliwa; mzoga wake wake ukaliwa na tai na fisi maporini mbali huko.
Kabisa mkuu. Tena anamwambia Ufalme wako wamepwewa wengine.MENEMENE TEKELI NA PELESI
 
Mwaka 2020 Watanzania walikataa wokovu wa chadema na matokeo yake wokovu huo umepelekwa kwa mataifa!
 
Back
Top Bottom