Umesoma degree makaratasi ukapata kazi serikalini ukapewa na cheo basi ndo mwisho wa matumizi ya fikra zako. Kila kinacholetwa unaamua kwa kuangalia maslahi yako na mabosi wako, kazi yako kubwa ni kutia saini kila kitu bila kutafakari kiundani mambo husika.
Hakuna mwanadamu asiyekuwa mbinafsi, kauli hii inajidhiirisha wazi kabisa.
Tuna viongozi wachache sana. Wengi wapo tu wakisubiri kila kitu atafuniwe yeye ni kumeza tu.
Ukikaa kufikiria sababu za msingi za baadhi ya maamuzi yanayofanywa na kiongozi mpaka mtu unabaki unajiuliza huyu kweli nati zimekaa sawa?
Ifikie hatua kila mmoja awe flexible, kama unaona mazingira ya nchi yako hayakupi support kwa kile ulichonacho ili kuiinua, tafuta namna nenda nchi yoyote ambayo unaona uko mambo yako yataenda sawa.
Tumepoteza na tunaendelea kupoteza vipaji vingi sana hapa kwetu Tanzania na pia tumekuwa na ushabiki wa vitu vidogo hata visivyo na msingi, yaani wenzetu washafanya huko mda mrefu na hawaoni jipya, sisi kwetu mambo hayo yanaonekana kuwa mapya na ya kustaajabisha na tunadiriki kutoa pongezi kana kwamba ni muujiza umefanywa.
Umasikini wa kifikra unatutesa sana siyo siri.
Hata vyanzo vya mapato na wasomi wetu wote tulionao hakuna wa kuja na njia bora za kuongeza pato la taifa na wapo maofisini wanakula viyoyozi huku mjasiriamali mwenye nia ya dhati na ubunifu wa kutosha akiminywa na mazingira magumu ya biashara yake aliyotumia nguvu na akili kuianzisha.
Haya mambo yanauma sana aisee, na hapo watakuja kujitetea na hoja za kwenye makaratasi theory za vitabu walizosoma miaka mingi huko nyuma bila hata kuangalia uhalisia wa huyu raia kwa wakati huo na mazingira halisi.
The problem with Africa is, those with ideas has no power and those with power has no ideas.
Prof Lumumba