Wanaofanyakazi ya kupamba kumbi za starehe, kusherehesha (Ma-MC), wapishi wa sherehe na wapiga picha, watatakiwa kulipa ada na ushuru

WATU wanaofanyakazi ya kupamba kumbi za starehe, kusherehesha (Ma-MC), wapishi wa sherehe na wapiga picha, watatakiwa kulipa ada na ushuru.

Ni baada ya Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema jijini Mwanza, kupitisha sheria ndogo za ada na ushuri ambazo tayari zimepata baraka za Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

Barua iliyosainiwa na Emmanuel Kaponoke, Afisa Utamaduni wa halmashauri hiyo ya tarehe 15 Januari 2021 kwenda kwa walengwa, inabainisha ada hizo.

Washereheshaji (MC) watapaswa kulipa Sh.50,000 kwa sherehe moja huku wapambaji kumbi za burudani/sherehe watalipa Sh.30,000.

Wamiliki wa kumbi, unaochukua watu kati ya 100-200 ni Sh.50,000 kwa siku, ukumbi unaochukua watu kati ya 201-500 atalipa Sh.100,000.

Wapishi wa vyakula kwa siku moja ya tukio atapaswa kulipa Sh.30,000 na wapiga picha za video na mnato watapaswa kulipa Sh.30,000 huku muziki ikiwa ni Sh.30,000

“Kamwe, mmiliki wa ukumbi asiruhusu sherehe kufanyika ndani ya ukumbi wake bila kibali cha halmashauri,” inaeleza sehemu ya barua hiyo

“Ikumbukwe, ada hii ni kwa ajili ya kubali cha halmashauri tu na si gharama ya kukodi ukumbi.”

Mitano tena

#YNWA
 
Ngoja ni ufunge wangu mdomo, wazazi wangu wananipenda mno🤐🤐🤐🤐
 
Na itakuwaje kama ma-MC wanajitolea bure?
Au wapishi wanapika bure?
Hapa ukienda mahakamani unawashinda kirahisi hawa maboya.
La sivyo kila anayepika au kufanya kazi ya u-MC awe analipwa(aingize kipato).
Mwisho,Nina wasiwasi na elimu za viongozi watu hasa madiwani.
Anapika bure maa na yake Nini?
Yaani mpishi anauwwzo was kuwanunulia wenye harusi vyakula na akawapiki bure?
 
Waongezee na hii....

-kila chombo Cha usafiri kitakayoshiriki Kwenye msafara wa maharusi
- gari = 50,000
-bajaji= 30,000
-pikipiki= 20,000
-baskeli= 10,000
Watachuka na hii, hebu acha kuongeza ushauri maana watachukua kama ilivyo
 
Kwa hiyo hata wakianzisha kodi ya ndoa utakubali?Vibaraka wa kijani mna simple minds sana.
Mkuu kodi ipo kwa mtu anaepata kipato
Kwani kwenye ndoa kuna kipato??
Tumia akili basi wewe mpiga dili
Yaani lazima waumie tu maana mianya ya wapiga dili imeziba imeziba kabisa
 
Acha kuongea pumba wewe..au umekaa kwa shemeji ndio unaongea pumba hivyo.
Mkuu mimi napiga kazi ya kilimo cha mboga mboga na mahindi ya kuchoma
Nalipa kodi zote
Sina shida na serikali kabisa
Kama wewe ni mpiga dili lazima muumie maana sana maana mianya ya wapiga dili imeziba kabisa
 
Mkuu kodi ipo kwa mtu anaepata kipato
Kwani kwenye ndoa kuna kipato??
Tumia akili basi wewe mpiga dili
Yaani lazima waumie tu maana mianya ya wapiga dili imeziba imeziba kabisa
Umekaririshwa sana.Mianya gani iliyozibwa wakati wakubwa zenu wanapiga madili tu?Kwa elimu yako unadhani watu wakilipishwa kodi hovyohovyo wataendelea na hizo biashara au miradi wanayofanya.
Obvious wataacha,then what follows:
Wao pamoja na serikali watapungukiwa mapato,mwisho wake ni mdororo wa kiuchumi.Sema mnaongea ili mpate vyeo au ili mlinde vyeo vyenu.
Lakini I'm sure kabla ya 2023 kila kitu kitakuwa sawa.Vipofu wataona na wajinga wataelewa.
 
Mkuu mimi napiga kazi ya kilimo cha mboga mboga na mahindi ya kuchoma
Nalipa kodi zote
Sina shida na serikali kabisa
Kama wewe ni mpiga dili lazima muumie maana sana maana mianya ya wapiga dili imeziba kabisa
Wala hulimi mbogamboga,kazi yako ni kulamba miguu watawala,hata Kama wanakosea.
 
Umekaririshwa sana.Mianya gani iliyozibwa wakati wakubwa zenu wanapiga madili tu?Kwa elimu yako unadhani watu wakilipishwa kodi hovyohovyo wataendelea na hizo biashara au miradi wanayofanya.
Obvious wataacha,then what follows:
Wao pamoja na serikali watapungukiwa mapato,mwisho wake ni mdororo wa kiuchumi.Sema mnaongea ili mpate vyeo au ili mlinde vyeo vyenu.
Lakini I'm sure kabla ya 2023 kila kitu kitakuwa sawa.Vipofu wataona na wajinga wataelewa.
Mkuu mwezi Dec tulikusanya kodi ya sh trillion mbili
Hio haijawahi kutokea
Kama biashara zimefungwa tungepataje pesa yote hio?
Nchi hii ni tajiri sana
Shule bure
Huduma za afya bure
Yaani Tanzania ya Magufuli neema tupu
 
Tukikusanya kias kisitosheleze basi.

Vi carry (kirikuu) vya kubeba vyombo vya muziki wajiandae 30000

Wabeba mapambo pikipiki ya miguu mitatu 20000

Wabeba camera za picha za mnato na jongefu (bodaboda)5000.

Mpk makasi tawatoke miaka hii.
Matangazo ya mtaani kupitia maspika makubwa itabidi walipie kodi pia
 
Back
Top Bottom