KERO Wanaofunga barabara ili kuabudu wako juu ya sheria?

KERO Wanaofunga barabara ili kuabudu wako juu ya sheria?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Lavit

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2011
Posts
14,834
Reaction score
32,522
Wakuu habarini!

Leo mchana nilikuwa Kariakoo, sasa kilichonishtua ni kuona mitaa mingi imefungwa watu wanaabudu barabarani.

Mbaya zaidi hakuna ishara yeyote utaiona kwamba mtaa husiku umefungwa, mtu unatembea mpaka katikati ya mtaa then unakuta kamba, ukizunguka mtaa mwingine unakuta watu wako mbio mbio na mikeka yao.

Nilivyojaribu kudadisi kinachondelea nikaambiwa ni kawaida, tena siyo K.koo tu ni mpaka Posta!

Ninachojiuliza hawa jamaa kinachowashinda kujenga nyumba za ibada zenye nafasi ni kitu gani!? Hili la kukatisha shughuli za wengine kisa imani yako sidhani kama ni ustaarabu!
 
Wakuu habarini!

Leo mchana nilikuwa kariakoo, sasa kilichonishtua ni kuona mitaa mingi imefungwa watu wanaabudu barabarani...
Siyo hawa wenye ijumaa yao tu hata nyinyi wa jumapili mitaa huwa inafungwa, njoo kariakoo jumapili mitaa ya likoma na masasi likoma na magila muhonda na ndanda mita ya asubuhi mitaa hiyo yote utakuta imefungwa.
Wakuu habarini!

Leo mchana nilikuwa kariakoo, sasa kilichonishtua ni kuona mitaa mingi imefungwa watu wanaabudu barabarani...
 
Mimi ni muislamu ila ninashawishika kureasoning na wewe. Hoja yako ina mashiko sana!

1. Tujitahidi kuongeza majengo ya kuabudia katika maeneo ya posta na kariakoo.

2. Kwa kuwa maeneo hayo yanajaa sana watu wajaribu kwenda mbali zaidi kama bakwata kinondoni na maeneo mengine ya karibu na kkoo na posta, tena kwenda mbali zaidi kuabudu ni thawabu zaidi.

3. Waumini wajitahidi kuwahi ili kuepuka kuswali nje.

Mwisho bandiko lako lina mashiko ila title yako ni kama unatukebehi flani hivi... uliposema hawa wa dini ya haki ina maana wapo juu ya sheria? Hapo ndipo unapoattract matusi na majibu ya jazba kwa wasio kuwa wavumilivu. Ungeweza kuiweka vizuri na ukaeleweka vizuri sana.
 
watu wengi wa posta na kkoo hawaishi maeneo hayo, kwahiyo hata ujenge jengo gani huwezi kujua idadi kamili ya waumini, kumbuka hayo maeneo yana wafanyabiashara na wateja, kwahiyo kwa ijumaa tuvumiliane tu hakuna jinsi ila siku za kawaida huwezi kukuta hilo jambo
 
watu wengi wa posta na kkoo hawaishi maeneo hayo, kwahiyo hata ujenge jengo gani huwezi kujua idadi kamili ya waumini, kumbuka hayo maeneo yana wafanyabiashara na wateja, kwahiyo kwa ijumaa tuvumiliane tu hakuna jinsi ila siku za kawaida huwezi kukuta hilo jambo
Jengeni ghorofa Kadhaa kwenda juu pia wekeni sound proof
 
hili jambo ni kawaida kwa ijumaa,.ukopita kesho jumamosi huwezi kukuta
Sema itatokea siku yatotokea majanga maana mda mwngn yanasababisha foleni maana Kuna mda magari yanatokea huku bara bara ya mataa ya big bon.

Yanakuja kutokea msikiti wa Idrisa (tandamti) yanapandisha kupitia msikiti wa Madina sasa kukipigwa pin pale panakua na foleni sana
 
Back
Top Bottom