KERO Wanaofunga barabara ili kuabudu wako juu ya sheria?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Kuna mmoja kwenye ndege kaanza kusali kwenye corridor hapo hapo. Abiria wacha wapanick wakajua ndo anataka kulipua pipa huko huko angani
Hawa jamaa sijui vipi,siku kazini jamaa kaacha kitengo chake yuko chooni kabinuka.
Nikamshtua oyaah wateja wanasubiri huko.
"Kashtuka"sawa boss nakuja
nikamwambia ndo utoe hivyo virago vyako twende.
maana alikua kabongöa jasho linamtoka viatu kavua.
Kuuliza naambiwa ndo hivyohivyo daily anapotea nusu saa anarudi.
 
KWa hiyo mkuu kwa kuwa wewe ni boss wake na unachukia imani yake ukaamua umkurupue?? Na kabisa unajiona una busara ya kuwa boss?? Basi mwambie abadilishe dini ili aendelee kuwa chini yako na kukusikiliza.

WAkati anaswali hukuweza kumhandle huyo mteja au ndio wale maboss tuma tuma? Eyes on Hands off?
 
Hallo kila mtu na kitengo chake.
Ntamudumia vipi huyo mteja wakati yeye huko anaswali na ndio ana maelezo yote.
Mwenyewe nilikua busy mda huo ntaanza vipi kufanya kazi yake?
 
It's a matter of Tolerance, hawasali siku nzima.
 
Ni uhuni tu
 
Haiwezi kuwa kawaida, ni kukosa ustaarabu...kama msikiti umejaa rudi nyumbani! Huu ujinga huwezi kuukuta London wala NewYork!
....hatuna standard, kama machinga wanavyobana njia au kuifunga kabisa kwa kutandaza bidhaa zao njiani.
 
Majanga gani yatatokea? Huo utaratibu haujaanza jana wala leo upo miaka na miaka na hakuna majanga yeyote anayotokea na ndo maana serikali ipo kimya ni utaratibu ambao umezoeleka. Acheni watu waabudu. Kama mtu anakereka asipite ilo eneo atafute njia nyingine njia ziko nyingi!
 
Haiwezi kuwa kawaida, ni kukosa ustaarabu...kama msikiti umejaa rudi nyumbani! Huu ujinga huwezi kuukuta London wala NewYork!
Umeshasema London hapa sio London. Kwavile London hakuna na hapa isiwepo? Au kwavile London ipo na hapa iwepo? Kama ndo ivyo London wanatetea ushoga na mashoga wana haki zao, kwahiyo na Tanzania pia tuwape nafasi mashoga? Hii ni Tanzania na kila nchi ina taratibu zake na mazoea yake, unakereka usipite hiyo njia au hamia London!
 
Wanaolalamika humu wengi wao ni wakuja wameanza kuyaona leo haya
 
Hakuna haja ya kuwalaumu waumini,hapo wa kulaumiwa ni watu wa Mipango Miji,hivi nyie mnaosafiri kwenda Dubai kwani wanafunga mitaa kama Kariakoo!? Cha msigi hapa sio lawama bali ni kupata suluhisho
 
Serikali iingie kwa miguu miwili kabisa hii itaenda mbali kama wasipo ingilia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…