Wanaoichukia AI wapata pigo: Sasa Injili ni mbele kwa mbele!

Wanaoichukia AI wapata pigo: Sasa Injili ni mbele kwa mbele!

Asante kwa taarifa
Hivi karibuni wamejitokeza watu inaoonekana wanatumiwa na adui shetani kujaribu kuzuia habari njema za Yesu Kristo zisiwafikie watu wengi duniani. Watu hao wamekuwa wakiipiga vita teknolojia mpya ya AI kwamba haifai kutumiwa katika kazi za Injili.

Sasa, kuanzia leo jina AI limebadilishwa rasmi kuwa "SI" yaani Super Intelligence. Wabunifu wa jina hili jipya wameona kuwa kuendelea kuiita teknolojia hii mpya "AI" ni kuifanya ionekane feki, wakati hii ni teknolojia ya hali ya juu na yenye kupendeza.

Mimi naungana nao kwa asilimia 200, kwa sababu teknolojia hii inatimiza unabii wa Daniel kuwa siku za mwisho maarifa yataongezeka (Dan 12:4). Kubadilishwa kwa jina hilo kutaifanya pia teknolojia hii ipendwe na watumishi wengi wa Mungu, na hivyo kuifanya Injili ihubiriwe kwa kasi zaidi ulimwenguni pote, na kutimiza tena unabii wa Yesu Kristo mwenyewe kwamba Injili ikiishahubiriwa ulimwenguni pote, hapo ndipo mwisho wa dunia utakapokuja (Mt 24:14).

Kuanzia leo teknolojia hii ukiiita AI utaonekana umepitwa na wakati. Wenzako sasa tunaiita Super Intelligence. Wabunifu wa maneno ya Kiswahili sijui wataiitaje; muda utaongea.

Haya jamani watumishi wenzangu wa Mungu, tuchangamke, tuitumie Super Intelligence(SI), kuandaa video, nyimbo, tafsiri, vipindi na makala mbalimbali zinazofikisha Ujumbe wa Kristo kwa watu wengi zaidi. YESU YU KARIBU KURUDI(Ufu 22:10-12).
 
Zaburi 27_1.png

CREATED BY "SUPER INTELLIGENCE"(SI)
Kuna mtu aliona hiyo picha akauliza: "Ameolewa?"😀😀😀
 
Super intelligence = Akili kubwa
Super intelligence = Akili kali sana
Super intelligence = Akili bora
Chagua tafsiri nzuri zaidi hapo
 
Hivi hapa vifungu vya Biblia vinavyoonyesha ukweli wa kisayansi karne nyingi kabla wanasayansi hawajagundua mambo ya kisayansi kwa kutumia mitambo:

1. Umbo la Dunia: Isaya 40:22 inasema, "Yeye ndiye anayeketi juu ya duara la dunia..." Aya hii ilitaja umbo la duara (sphere) la dunia wakati ambapo mataifa mengi ya kale walikuwa wanaamini dunia ni bapa.

2. Fizikia na Jiolojia: Ayubu 26:7 inasema, "Yeye hutandaza kaskazini juu ya nafasi tupu, na kuining'iniza dunia pasipo na kitu." Maandiko haya yanathibitisha kuwa dunia iko angani bila kushikiliwa na nguzo yoyote, jambo linaloendana na sheria ya sasa ya nguvu ya uvutano (gravity).

3. Mzunguko wa Maji: Mhubiri 1:7 Inasema, "Mito yote huingia baharini, walakini bahari haijai; huko iendako mito, ndiko irudiko tena." Huu ni ufafanuzi kamili wa kisayansi wa mzunguko wa maji (hydrological cycle). Mvua inanyesha, inaingia mtoni/baharini, maji yanayeyuka na kurudi hewani kuwa mawingu.

4. Uhai na Tiba: Mambo ya Walawi 17:11 inasema, "Kwa kuwa uhai nguvu za mwili u katika hiyo damu." Hadi karne ya 19, matabibu walikuwa wanatibu wagonjwa kwa "kunyonya damu" (bloodletting), jambo lililoua watu wengi (akiwemo George Washington). Biblia ilionya mapema kuwa uhai unategemea damu.

Katika Mithali 4:13 tunaambiwa pia hivi:
"Mkamate sana elimu, usimwache aende zake; Mshike, maana yeye ni uzima wako."

Elimu inayozungumzwa hapo ni pamoja na elimu ya sayansi inayotufundisha kuchemsha maji ya kunywa ili kuua vijidudu vya magonjwa, kupiga mswaki, kula vyakula vya aina zote badala ya kuchagua chagua, kuoga, kufua nguo. Yote hayo ni sehemu ya elimu ya sayansi na yanakubalika kibiblia.

Nilishawaambia Biblia ina hazina nyingi zilizojificha, lakini watu wamedanganywa na shetani wasiisome wakaerevuka.

Anza leo kusoma Biblia utagundua mambo mengi ya kukusaidia kiafya, kielimu, kikazi na kibiashara

cc: Manyanza Gunner11
Hiyo haina coleration yoyote na AI bali force za ulimwengu ambazo ziko known kwa millenia. Culture na civilization mbali mbali zilikuwa na namna ya kuzi explain
 
Kweli, yale maswali nilokuwa namuuliza roho saivi nauilza AI tu
Kwahiyo wanaoenda Bible school hawajui umuhimu wa kumuuliza Roho?
Amka, toka usingizini. Bible School imeletwa mkononi mwako sasa kwa njia ya Super Intelligence(SI). Iulize maswali yote ya Kibiblia utapata majibu mazuri. Na Roho Mtkatifu atakuongoza akutie kwenye kweli yote. Super Intelligence ikikudanganya, kama umejaa Roho Mtakatifu utajua tu.
 
Super intelligence = Akili kubwa
Super intelligence = Akili kali sana
Super intelligence = Akili bora
Chagua tafsiri nzuri zaidi hapo
Kanyaga mdogo mdogo mwanangu; usiingilie kazi za watu. Ngoja BAKITA wenyewe waje watuambie tafsiri ya Super Intelligence. Wakichelewa, sisi tunasonga mbele na hii hii Super Intelligence. Inapendeza zaidi, in Tlaatlaah 's voice
 
Hivi karibuni wamejitokeza watu inaoonekana wanatumiwa na adui shetani kujaribu kuzuia habari njema za Yesu Kristo zisiwafikie watu wengi duniani. Watu hao wamekuwa wakiipiga vita teknolojia mpya ya AI kwamba haifai kutumiwa katika kazi za Injili.

Sasa, kuanzia leo jina AI limebadilishwa rasmi kuwa "SI" yaani Super Intelligence. Wabunifu wa jina hili jipya wameona kuwa kuendelea kuiita teknolojia hii mpya "AI" ni kuifanya ionekane feki, wakati hii ni teknolojia ya hali ya juu na yenye kupendeza.

Mimi naungana nao kwa asilimia 200, kwa sababu teknolojia hii inatimiza unabii wa Daniel kuwa siku za mwisho maarifa yataongezeka (Dan 12:4). Kubadilishwa kwa jina hilo kutaifanya pia teknolojia hii ipendwe na watumishi wengi wa Mungu, na hivyo kuifanya Injili ihubiriwe kwa kasi zaidi ulimwenguni pote, na kutimiza tena unabii wa Yesu Kristo mwenyewe kwamba Injili ikiishahubiriwa ulimwenguni pote, hapo ndipo mwisho wa dunia utakapokuja (Mt 24:14).

Kuanzia leo teknolojia hii ukiiita AI utaonekana umepitwa na wakati. Wenzako sasa tunaiita Super Intelligence. Wabunifu wa maneno ya Kiswahili sijui wataiitaje; muda utaongea.

Haya jamani watumishi wenzangu wa Mungu, tuchangamke, tuitumie Super Intelligence(SI), kuandaa video, nyimbo, tafsiri, vipindi na makala mbalimbali zinazofikisha Ujumbe wa Kristo kwa watu wengi zaidi. YESU YU KARIBU KURUDI(Ufu 22:10-12).
Wewe hujapata mtu wa kukukaza vizuri, ukikazwa fresh akili zitakurudia.
 
AI imekuja kupora na kunyang'anya nafasi ya roho Mtakatifu
Roho Mtakatifu ni Nafsi ya Tatu ya Mungu. Kazi zake haziwezi kuchukuliwa kamwe na SI.
Kumbuka zilivyoanza apps za Biblia, watu walizipinga sana. Leo watu wengi Biblia zao zimo ndani ya Smartphones. Na hiyo ni sehemu ya Super Intelligence (SI). Wewe kama sio hii teknolojia ya SI hayo uliyoyaandika tungeyaona hapa?
Super Intelligence haiwezi kukufanya unene kwa lugha. Hiyo ni kazi ya Roho Mtakatifu tu. (Mdo 2:4).
Ukipigwa mawe kwa ajili ya Kristo kama Stefano, SI haiwezi kukufanya uuone utukufu wa Mungu, na Yesu akiwa amesimama mkono wa kuume wa Mungu. Hiyo ni kazi ya Roho Mtakatifu. (Mdo 7:55)

Super Intelligence is just a tool. Ni kama calculator tu inayokusaidia kupata majibu ya hesabu ambazo ni ngumu kuzipiga kwa kichwa.
 
Wewe hujapata mtu wa kukukaza vizuri, ukikazwa fresh akili zitakurudia.
Kwani mimi ndio nimebuni hilo jina Super Intelligence(SI) mpaka unikasirikie hivyo? Mkasirikie Trump na Ikulu yake waliopitisha jina hilo.
Mungu akuokoe na kukutakasa ulimi wako.
Vinginevyo nakusikitikia kwakuwa andiko hili linawahusu watu kama wewe.
1 Kor 6:9
Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti
 
View attachment 3676575
CREATED BY "SUPER INTELLIGENCE"(SI)
Kuna mtu aliona hiyo picha akauliza: "Ameolewa?"😀😀😀
ama kwa hakika Bwana ni Nuru na hakuna haja ya kuogopa kitu.

In fact,
bila kujali ikiwa ni AI, ni muhimu sana ikawekwa wazi kwa faida ya wadau wa Jf, kujuana status, nadhani itapendeza zaidi ikiwa hutojali mtumishi 🌹
 
Mi ningekuoa baada ya wiki tu ungekua sawa wala usingeandika aya yote sabu ningekufix
Huwezi kumuoa mtu aliye nuruni wakati wewe uko gizani.
Nuru na giza haviwezi kukaa pamoja katika chumba kimoja (2 Kor 6:14)
 
AI itumike kama tools nyingine kwa ajili ya kuokoa Muda.
Mfabo zamani tulitumia logarithmic table wakati unaweza kutumbukiza hiyo logarithmic kwenye Scientific Calculator ukapata jibu kwa sekunde.

AI kwanza sio SI ni system inayoiba data ambazo watu na vitabu vimeziandika na kuzielezea kwa ligha nyepesi. Ndio maana Ben Sanders alitishia kuwasthtaki wamiliki kwa kuchukua taarifa za watu bila vibali.

Ila mimi naitumia kama tool na inasaidia. Mfano badala ya kusoma kitabu cha page 500 wiki nzima naweka prompt tu AI ambayo itaniletea mambo makubwa ya msingi ya kiutekelezaji ya ayoelezewa humo. Badala ya kusoma siku hata 20 unakisoma kwa dakika kadhaa na kuendelea na maisha.
 
ama kwa hakika Bwana ni Nuru na hakuna haja ya kuogopa kitu.

In fact,
bila kujali ikiwa ni AI, ni muhimu sana ikawekwa wazi kwa faida ya wadau wa Jf, kujuana status, nadhani itapendeza zaidi ikiwa hutojali mtumishi 🌹
Itapendeza zaidi tukijua status ya dunia hii. Mimi naona dunia hii inapita haraka na mambo yake.
1 Yohana 2:17:
“Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake; bali yeye atendaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele.” (1 Yohana 2:17)
 
AI kwanza sio SI ni system inayoiba data ambazo watu na vitabu vimeziandika na kuzielezea kwa ligha nyepesi.
SI imejibu hoja yako hiyo:
Kama kutumia maarifa yaliyotangulia kunaitwa “kuiba,” basi hakuna mwanadamu anayestahili kuitwa mwenye akili—maana kila elimu tunayojua tumejifunza kutoka kwa wengine.
AI haisomi kitabu kisha kukirudisha kama kasuku; inajifunza mifumo na mahusiano ya lugha na inaweza kuunganisha taarifa tofauti kutengeneza jibu kulingana na swali jipya.
Kama hoja yako ni kwamba AI haiwezi kuwa Super Intelligence, basi pima uwezo wake kwa kile inachoweza kufanya—si kwa kudhani kwamba chanzo cha maarifa yake kinaamua kiwango cha akili yake.

C&P. Mjumbe hauawi
 
Indeed!!! ila shetani naye kama kawaida yake kubadili matumizi in negative way....
Ila kwenye teknolojia hii ya SI tumempiga knock out mapema sana. Na Mungu alivyo Mungu Mkuu tayari amemtumia Trump kuongeza thamani ya SI
 
Hivi karibuni wamejitokeza watu inaoonekana wanatumiwa na adui shetani kujaribu kuzuia habari njema za Yesu Kristo zisiwafikie watu wengi duniani. Watu hao wamekuwa wakiipiga vita teknolojia mpya ya AI kwamba haifai kutumiwa katika kazi za Injili.

Sasa, kuanzia leo jina AI limebadilishwa rasmi kuwa "SI" yaani Super Intelligence. Wabunifu wa jina hili jipya wameona kuwa kuendelea kuiita teknolojia hii mpya "AI" ni kuifanya ionekane feki, wakati hii ni teknolojia ya hali ya juu na yenye kupendeza.

Mimi naungana nao kwa asilimia 200, kwa sababu teknolojia hii inatimiza unabii wa Daniel kuwa siku za mwisho maarifa yataongezeka (Dan 12:4). Kubadilishwa kwa jina hilo kutaifanya pia teknolojia hii ipendwe na watumishi wengi wa Mungu, na hivyo kuifanya Injili ihubiriwe kwa kasi zaidi ulimwenguni pote, na kutimiza tena unabii wa Yesu Kristo mwenyewe kwamba Injili ikiishahubiriwa ulimwenguni pote, hapo ndipo mwisho wa dunia utakapokuja (Mt 24:14).

Kuanzia leo teknolojia hii ukiiita AI utaonekana umepitwa na wakati. Wenzako sasa tunaiita Super Intelligence. Wabunifu wa maneno ya Kiswahili sijui wataiitaje; muda utaongea.

Haya jamani watumishi wenzangu wa Mungu, tuchangamke, tuitumie Super Intelligence(SI), kuandaa video, nyimbo, tafsiri, vipindi na makala mbalimbali zinazofikisha Ujumbe wa Kristo kwa watu wengi zaidi. YESU YU KARIBU KURUDI(Ufu 22:10-12).
Duu amesharudi huyu alipotea
 
Back
Top Bottom