Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapo kuna hoja, maana yake badala ya kuwa kuwahutubia unaweza kuwaambia watoe hoja zao za msingiKuna siku nilimsikia Askofu Kakobe ( enzi hizo ) akisema alishawahi kualikwa lakini alivyoenda akakuta kazi yao ni kusikiliza tu na kupiga makofi.
Baada ya hapo hakushiriki tena. Sasa tunaweza kulaumu lakini kumbe watu wengine hawataki kushiriki wenyewe.
Hapa Mwanza yupo Mzee Kafiti. Anakaa Nyakato National. Kama wewe ni Mtumishi wa Serikali na ukatofautiana nae, unapata uhamisho wa ghafla na unalipwa stahili zako zote za uhamisho kiasi kwamba unashindwa kujua kama umeonewa au umependelewa!Ninaomba yeyote anayewajua anieleweshe ili mimi na wengine wasioelewa kama mimi tuwafahamu Wazee hawa ambao kila kiongozi anapenda kukutana nao.
Natanguliza shukrani.
So fursa kwa watakao kuhamaHapa Mwanza yupo Mzee Kafiti. Anakaa Nyakato National. Kama wewe ni Mtumishi wa Serikali na ukatofautiana nae, unapata uhamisho wa ghafla na unalipwa stahili zako zote za uhamisho kiasi kwamba unashindwa kujua kama umeonewa au umependelewa!
Pilau na ubwabwa muhimu viwepo Ili kuwakosha wazee wetu wa kamatiNasikia wako mia tisa. Kesho nitasoge pale mlimani city nikawaone aisee
Usichokijua usiku wa giza.Hao siyo wazee ni kundi la watu walioze3ka sababu ya uduni wa maisha,kesho wakati anaongea nao watazame vizuri ,wapiga makofi tu.
Ndio ni fursa, lakini kazi kweri kweri. Kuna stori hapo Nyakato National kwamba Mzee "alichepusha" Barabara ya Musoma ili tu nyumba yake isibomolewe.So fursa kwa watakao kuhama
Wazee wa Dar ndiyo wazee waliowaongoza wazee wenzao Tanganyika nzima kudai uhuru.Why wa dar tu?
1. Je, hao wazee wanapatikana Dar tu au wapo kila mkoa?
2. Je, wa Dar ndio muhimu kuliko wa mikoa mingine?
Wakwanza nimimi. Nitakuwepooo. Wengine utawaona.Ninaomba yeyote anayewajua anieleweshe ili mimi na wengine wasioelewa kama mimi tuwafahamu Wazee hawa ambao kila kiongozi anapenda kukutana nao.
Natanguliza shukrani.
Jan 2021
RC KUNENGE AKUTANA NA WAZEE WA MKOA WA DAR ES SALAAM
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge leo amekutana na kufanya kikao na Wawakilishi wa Wazee wa Mkoa huo kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili Wazee ili Serikali iweze kuzifanyia kazi. Katika kikao hicho RC Kunenge amepokea changamoto na mapendekezo mbalimbali kutoka kwa Wazee hao ambapo zipo changamoto zililizopatiwa majibu ya papo kwa papo na nyingine za kisera na kisheria ambazo ameahidi kuzifikisha katika ngazi husika. Aidha RC Kunenge amewashukuru na kuwapongeza Wazee wote wa Mkoa huo kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya Katika kueneza Busara, hekima na maarifa kwa jamii Jambo linalosaidia kuwa na kizazi kinachofuata maadili na kulinda amani na usalama mkoani humo. Hata hivyo RC Kunenge amewaeleza Wazee hao kuwa ofisi yake iko wazi kupokea na kusikiliza ushauri kutoka kwa Wazee na ataweka utaratibu kukutana na Wazee wa Mkoa huo kila baada ya miezi mitatu. Pamoja na hayo RC Kunenge amewasihi Wazee kuendelea kuwa kisima Cha maarifa na kuhakikisha wanakuwa washauri wazuri wa Amani, Upendo, upatanisho na watoe nasaha kwa jamii. Kwa upande wao Wazee walioshiriki kikao hicho wamemshukuru RC Kunenge kwa namna anavyowakumbuka na kuwathamini Wazee wa Mkoa huo na wamemuahidi watampatia ushirikiano wa kimawazo Katika kila Jambo.
Wazee wa Dar ni kizazi cha akina Dossa Aziz, Mshume Kiate, Abdulwahid Sykes, Zuberi Mtemvu, Mohamed Ramia, Sheikh Yahaya Hussein, Jumbe Tambaza, Mwinjuma, Mbaraka Mavemba,Abdallah Shomari Mazongera, nk
Kwa kifupi ni familia zile ambazo wazee wao walishiriki vilivyo kwenye harakati za uhuru wa Tanganyika
Kasome uzi wa Forojo Ganze
Hii Post yako wataifanyia kazi.Ni wanachama wa chama cha mapinduzi, hakunaga wazee wa dar ambao ni mchanganyiko wa vyama. utawaona kesho wamevaa kijani, na ili msiwashtukie watakatazwa kuvaa nguo za chama. vinginevyo Rais angekuwa anawaomba kila chama kiwasilishe majina ya wazee watakao udhuri akikao
Na sijui nani huwa ana waalika, nadhani ni makada wa CCM