Wanaoitwa Wazee wa Dar es Salaam ambao kila Rais wa Tanzania anatamani kukutana nao ni akina nani?

Wanaoitwa Wazee wa Dar es Salaam ambao kila Rais wa Tanzania anatamani kukutana nao ni akina nani?

Kesho kaa karibu na Luninga. Popcorn kwa pembeni. Utawaona wazee hao wa Dar Es Salaam
 
Kuna siku nilimsikia Askofu Kakobe ( enzi hizo ) akisema alishawahi kualikwa lakini alivyoenda akakuta kazi yao ni kusikiliza tu na kupiga makofi.

Baada ya hapo hakushiriki tena. Sasa tunaweza kulaumu lakini kumbe watu wengine hawataki kushiriki wenyewe.
Hapo kuna hoja, maana yake badala ya kuwa kuwahutubia unaweza kuwaambia watoe hoja zao za msingi
 
Ninaomba yeyote anayewajua anieleweshe ili mimi na wengine wasioelewa kama mimi tuwafahamu Wazee hawa ambao kila kiongozi anapenda kukutana nao.

Natanguliza shukrani.
Hapa Mwanza yupo Mzee Kafiti. Anakaa Nyakato National. Kama wewe ni Mtumishi wa Serikali na ukatofautiana nae, unapata uhamisho wa ghafla na unalipwa stahili zako zote za uhamisho kiasi kwamba unashindwa kujua kama umeonewa au umependelewa!
 
Wazee wa Dar ni kizazi cha akina Dossa Aziz, Mshume Kiate, Abdulwahid Sykes, Zuberi Mtemvu, Mohamed Ramia, Sheikh Yahaya Hussein, Jumbe Tambaza, Mwinjuma, Mbaraka Mavemba,Abdallah Shomari Mazongera, nk
Kwa kifupi ni familia zile ambazo wazee wao walishiriki vilivyo kwenye harakati za uhuru wa Tanganyika
Kasome uzi wa Forojo Ganze
 
Jan 2021

RC KUNENGE AKUTANA NA WAZEE WA MKOA WA DAR ES SALAAM

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge leo amekutana na kufanya kikao na Wawakilishi wa Wazee wa Mkoa huo kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili Wazee ili Serikali iweze kuzifanyia kazi. Katika kikao hicho RC Kunenge amepokea changamoto na mapendekezo mbalimbali kutoka kwa Wazee hao ambapo zipo changamoto zililizopatiwa majibu ya papo kwa papo na nyingine za kisera na kisheria ambazo ameahidi kuzifikisha katika ngazi husika. Aidha RC Kunenge amewashukuru na kuwapongeza Wazee wote wa Mkoa huo kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya Katika kueneza Busara, hekima na maarifa kwa jamii Jambo linalosaidia kuwa na kizazi kinachofuata maadili na kulinda amani na usalama mkoani humo. Hata hivyo RC Kunenge amewaeleza Wazee hao kuwa ofisi yake iko wazi kupokea na kusikiliza ushauri kutoka kwa Wazee na ataweka utaratibu kukutana na Wazee wa Mkoa huo kila baada ya miezi mitatu. Pamoja na hayo RC Kunenge amewasihi Wazee kuendelea kuwa kisima Cha maarifa na kuhakikisha wanakuwa washauri wazuri wa Amani, Upendo, upatanisho na watoe nasaha kwa jamii. Kwa upande wao Wazee walioshiriki kikao hicho wamemshukuru RC Kunenge kwa namna anavyowakumbuka na kuwathamini Wazee wa Mkoa huo na wamemuahidi watampatia ushirikiano wa kimawazo Katika kila Jambo.
 
Kumekucha !
 
Wazee wa Dar ni kizazi cha akina Dossa Aziz, Mshume Kiate, Abdulwahid Sykes, Zuberi Mtemvu, Mohamed Ramia, Sheikh Yahaya Hussein, Jumbe Tambaza, Mwinjuma, Mbaraka Mavemba,Abdallah Shomari Mazongera, nk
Kwa kifupi ni familia zile ambazo wazee wao walishiriki vilivyo kwenye harakati za uhuru wa Tanganyika
Kasome uzi wa Forojo Ganze

BARAZA LA WAZEE WA TANU 1954 - 1963
Mohamed Said

Mara tu baada ya kuundwa kwa TANU mwaka wa 1954 Baraza la Wazee wa TANU liliundwa katika makao makuu, New Stret Dar es Salaam.

Baraza hili lilikuwa na takriban wajumbe 170.
Ilikuwa ni kamati ya wazee wa mji wa Dar es Salaam na kitu kimoja ni kuwa wajumbe wake wote walikuwa Waislam.

Sheikh Suleiman Takadir ndiye alikuwa mwenyekiti wa kwanza wa Baraza la Wazee wa TANU.

Kamati kama hii iliundwa Tabora mwaka wa 1956, Mwenyekiti wake akia Mzee Fundi Muhindi mwanasiasa mkongwe, muasisi wa African Association Tabora mwaka wa 1945 na muasisi wa TANU mwaka wa 1954.

Kwa nini kamati hizi zilikuwa na wajumbe Waislam watupu?

Kleist Sykes katika mswada wake wa kitabu alioandika kabla ya kufariki mwaka wa 1949 anasema kuwa waasisi wa African Association (AA) mwaka wa 1929 wengi wao walikuwa Waislam na sababu ni kuwa Wakristo walikuwa wakikatazwa na Kanisa kujiingiza katika siasa.

Katika hali kama hii hata mwakilishi wa Waafrika alikuwa Father Gibbons kutoka MInaki Misheni hii yote ilikuwa katika juhudi ya kuwaweka Waafrika chini na kuwakaia kichwani.

Kleist alipoanza harakati za kuasisi AA waliojotokeza kumuunga mkono walikuwa jamaa zake wanamji kama yeye.

Hivi ndivyo ikaja kuwa mjini Dar es Salaam waasisi wa AA wengi wao wakawa jamaa zake wanamji kama yeye wanaojuana kwa miaka kama Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamisi, Zibe Kidasi, Ali Said Mpima, Suleiman Majisu, na wakajaungwa mkono na Cecil Matola Raikes Kusi, na Rawson Watts.

Hawa watatu wa mwisho walikuwa wageni mjini Dar es Salaam.

Hapa ndipo tunaweza kuanza kuangalia asili ya Baraza la Wazee wa Dar es Salaam ndani ya AA kisha TAA pale AA ilipobadili jina na kuitwa TAA.

Lakini ili kufika hapo inabidi uangalie taasisi nyingine ambayo iliundwa ndani ya AA mwaka wa 1933 na tujue sababu za kuundwa kwake.

Mwaka wa 1933 baada ya kifo cha aliyekuwa Rais wa AA Cecil Matola nafasi yake ikajazwa na Mzee bin Sudi.

Ikawa baadhi ya mambo ya Waislam kwenda serikalini yanapitishwa kupitia AA hili likaonekana ni tatizo kwani AA ilundwa kwa nia ya kuwaunganisha Waafrika wote wa Tanganyika bila ya kujali dini wala kabila zao.

Ndipo mwaka wa 1933 ikaundwa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika Mzee bin Sudi akiwa President na Mzee bin Sudi Secretary nafasi ambao pia walikuwa wamezishikilia katika AA.

Hii ndiyo ikawa sababu kubwa sana kwa siasa za za mji wa Dar es Salaam naharakati za kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika zikawa zimetawaliwa na Waislam.

Hii ndiyo sababu Baraza la Wazee wa TANU lilipokuja kuundwa mwaka wa 1954 wajumbe wa baraza zima karibu 170 wakajikuta watu wa imani moja.

Hawa ndiyo waliojulikana kama Baraza la Wazee wa TANU.
Baraza hili lilivunjwa mwaka wa 1963 kwa kutuhumiwa kuwa, ‘’linachanganya dini na siasa.’’

Wakati linavunjwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU alikuwa Mzee Iddi Tulio.

20210506_230305.jpg
 
Ni wanachama wa chama cha mapinduzi, hakunaga wazee wa dar ambao ni mchanganyiko wa vyama. utawaona kesho wamevaa kijani, na ili msiwashtukie watakatazwa kuvaa nguo za chama. vinginevyo Rais angekuwa anawaomba kila chama kiwasilishe majina ya wazee watakao udhuri akikao
Hii Post yako wataifanyia kazi.
 
Back
Top Bottom