Wanaojua kutumia pesa, akaunti zao zinasoma salio kidogo

Wanaojua kutumia pesa, akaunti zao zinasoma salio kidogo

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Utafiti wangu mdogo nilioufanya nimegundua, watu wanaojua matumizi ya hela akaunti zao zinasoma hela ndogo ndogo tu; kama elfu kumi, ishirini au hamsini na haizidi laki; ila kwa wale wasiojua matumizi ya pesa akaunti zao zimenona, zinaweza kusoma kuanzia milioni nakuendelea.

Hii inatafsiri, wasiojua matumizi ya pesa wao ukusanya pesa na kuzilundika kwenye akaunti zao; ila wanaojua kutumia pesa, pesa ikiingia lazima iende kwenye mzunguko na kusababisha akaunti zao kuwa tupu.

Kama unabisha, njoo tubishane​
 
Vipi, je wanaopata mshahara wote unaishia kwenye matumizi na kubakisha zero balance hadi mshahara ujao naoa wanajua kutumia au wanalazimika kutokana na ufinyu
Wanajua kutumia, ila hawajajua njia mbadala za kuwawezesha kuendeleza huo mnyororo ili asiishi kwa tabu baada ya akaunti kukauka.
 
Nimekuja mkuu kubishana.

Pesa huwa inatafutwa kwa ajili ya mambo ya msingi 6. Mavazi, makazi, chakula, Elimu, Usafiri na Afya. Ziada ni starehe na burudani.

Ukishayapata haya pesa inayobaki haina matumizi unatakiwa kuisave iongezeke iwe nyingi kwa matumizi ya mambo ya msingi ya mbeleni.

Sasa kuna watu hawajui saving, wao pesa ikiwepo lazima aifuje ndo hujikuta hadi kwenye online casino na betting, ilimradi tu awe broke.
 
Nimekuja mkuu kubishana.

Pesa huwa inatafutwa kwa ajili ya mambo ya msingi 6. Mavazi, makazi, chakula,Elimu,Usafiri na Afya. Ziada ni starehe na burudani...
Nimeipenda hii ''It's true that poor people focus on saving but rich people focus on investing''

Pesa haitakiwi kutunzwa, inatakiwa iende kwenye matumizi; kama bado unatunza jua hujui kutumia pesa.
 
Matajiri wanasifika sana kuwa na tabia ya ubahili sana wa fedha.

Hawatumii kabisa fedha zao bila kuwepo na sababu ya msingi kwa sababu wanajua matumizi sahihi ya fedha, kuanzia kuweka bajeti, kupangilia fedha zao, kujilipa kwanza wao wenyewe, wanawekeza fedha zao sehemu ambazo zina faida, kuweka fedha ya dharura na kuishi chini ya kipato!
 
Huyo anajua matumizi ya pesa; pesa haitakiwi kutunzwa, inatakiwa iende kwenye matumizi
Kuna dharura ambazo ukiwa na saving zinakuepusha na aibu ndogo ndogo.

Upo matembezini umejikwaa ukaangukia trei za watu za mayai unaambiwa ni laki mbili na nusu badala ya kumwambia twende bank nikutolee unatangulizwa polisi ndugu zako na marafiki ndo wakuchangie.
 
Matajiri wanasifika sana kuwa na tabia ya ubahili sana wa fedha.

Hawatumii kabisa fedha zao bila kuwepo na sababu ya msingi kwa sababu wanajua matumizi sahihi ya fedha, kuanzia kuweka bajeti, kupangilia fedha zao, kujilipa kwanza wao wenyewe, wanawekeza fedha zao sehemu ambazo zina faida, kuweka fedha ya dharura na kuishi chini ya kipato!
Wa namna hiyo hawajajua matumizi ya pesa
 
Nimeipenda hii ''It's true that poor people focus on saving but rich people focus on investing''

Pesa haitakiwi kutunzwa, inatakiwa iende kwenye matumizi; kama bado unatunza jua hujui kutumia pesa.
Ndo maana nikasema kama unatunza inayobaki baada ya kutimiza mambo yako muhimu upo sawa.
 
Kuna dharura ambazo ukiwa na saving zinakuepusha na aibu ndogo ndogo.

Upo matembezini umejikwaa ukaangukia trei za watu za mayai unaambiwa ni laki mbili na nusu badala ya kumwambia twende bank nikutolee unatangulizwa polisi ndugu zako na marafiki ndo wakuchangie.
Na wengi wanaojua matumizi ya pesa, wanakuwa wametengeneza 'brand', vitatizo vidogo vidogo brand yake inamaliza.
 
Back
Top Bottom