Wanaojua magari Naomba kujua changamoto za Toyota Sienta

Wanaojua magari Naomba kujua changamoto za Toyota Sienta

Wakuu, moja kwa moja kwenye mada nomba kujulishwa changamoto na ubora wa Toyota Sienta,

Nataka kukanunua kwa ajili ya harakati zangu ndogo ndogo hasa biashara ya usambazaji bidhaa vijijini vip wataalam vigari hivi vina chngamoto gani na ubora gani?

Hasa katika barabara za vijijini?
Achana na hilo kopo! Kama uko kijijini kwenye barabara za hovyo chukua probox utakuja unishukuru! Kidude kinabeba mzigo kama hakina akili nzuri!
 
Nikurekebishe tu, Sienta na ndugu zake sio Magari ni vifaa vya usafiri kutoka sehem moja kwenda nyingine.

Angalia mambo mengi ikiwemo hali zote za hewa (Mvua, jua etc).

Tafuta Suzuki kisha nunua Teller funga nyuma kula maisha.. siku hauna ishu za kusupply mzigo unachomoa teller..

Yapo mateller mazuri na muonekano mzr
 
Ninayo tangu 2015.Changamoto mbili kubwa nilizopitia ni kwamba moja,milango yake ya nyuma iko complex,inajam kirahisi sana.Mafundi wengi hawawezi kurekebisha milango hiyo.Mpaka sasa nimeitelekeza kwakuwa nimekosa fundi mzuri wa milango.Pili,siku ikianza kutema moshi utapata usumbufu wakati wa kutafuta ringi za piston,maana hazipatikani kwa urahisi
 
Nje ya mada 🤝Mkuu Extrovert tia neno kwenye kwenye uimara wa Toyota Vits ya 2015 engine 1KR cc 990 kwa matumizi ya mizururo ya town na off road za hapa na pale.Vipi uimara wa body na engine.Pia changamoto zake kubwa hii gari ni zipi???🤝
1KR tu inatosha kusema kwamba hio gari achana nayo
 
Wakuu, moja kwa moja kwenye mada nomba kujulishwa changamoto na ubora wa Toyota Sienta,

Nataka kukanunua kwa ajili ya harakati zangu ndogo ndogo hasa biashara ya usambazaji bidhaa vijijini vip wataalam vigari hivi vina chngamoto gani na ubora gani?

Hasa katika barabara za vijijini?
Hiyo gari kwa kijijini utaionea sana
jibane uchukue Probox
 
Toyota probox ndiyo itamudu kazi unayotaka kuifanya.
 
Back
Top Bottom