Wanaomiliki Toyota Starlet wanaonekana vituko wakiwa mjini na Vigari vyao

Wanaomiliki Toyota Starlet wanaonekana vituko wakiwa mjini na Vigari vyao

Mimi similiki gari lakini kuna Vigari ukivimiliki unaonekana kituko hasa huku maeneo ya mjini.

Sipo apa kuleta Kashfa ama kukejeli wanaomiliki aya magari ila inabidi niwaambie ukweli ukimiliki starlet unaonekana kituko.

Unakuta jitu lina mwili mkubwa linaendesha starlet halafu vioo kashusha maana hakina Ac, mwili wote unajaa kwenye gari yaani ni vituko halafu unakuta mtu kama huyu anajiamini kumiliki gari Aisee mimi bora niendelee kutembea kwa mguu lakini sio kumiliki hili gari la starlet na aina nyingine za baby Walker.

Kwa leo ngoja niishie apa, nitarudi pindi Mungu akinipa Kibari cha kumiliki gari.View attachment 2743879
Ni kweki ni ka ajabu, lakini wewe usiye na gari na yeye kati yenu wawili nani anayepata shida?
Jamaa anawahi mishe zake, kama mvua hanyeshewi kituoni, kama shida ya usafiri bado anapeta.
Maisha ni kupanga mkuu. Ukikaa usubiri kumiliki V8 wakati huna uwezo nayo utapata tabu sana
 
Mume WA mtu mtarajiwa huyo.... Anongea hizo shiiit kama wakike
Wakati naolewa nilimkuta mume wangu ana Corolla ya zamani....
8 yrs ago....mpaka Leo nakuona mwanaume maana kitu kilikua akina hata ac.....lakin alikua anapambana.....nilibadili mentality from there....chako ni chako.....at least sikupanda madaladala......na ilikua yetu .....period
Wa kulaumiwa ni wazazi wanao Fuga mijitu mizima majumbani mwao ambayo haiwazi hata kesho ikishavimbiwa basi ishasahau Kila kitu
 
Mimi similiki gari lakini kuna Vigari ukivimiliki unaonekana kituko hasa huku maeneo ya mjini.

Sipo apa kuleta Kashfa ama kukejeli wanaomiliki aya magari ila inabidi niwaambie ukweli ukimiliki starlet unaonekana kituko.

Unakuta jitu lina mwili mkubwa linaendesha starlet halafu vioo kashusha maana hakina Ac, mwili wote unajaa kwenye gari yaani ni vituko halafu unakuta mtu kama huyu anajiamini kumiliki gari Aisee mimi bora niendelee kutembea kwa mguu lakini sio kumiliki hili gari la starlet na aina nyingine za baby Walker.

Kwa leo ngoja niishie apa, nitarudi pindi Mungu akinipa Kibari cha kumiliki gari.View attachment 2743879

Nikuelimishe tu kuwa;
Kazi ya msingi ya gari binafsi ni kukutoa point A hadi Point B kwa haraka na wakati unaouhitaji lakini pia kwa gharama inayoendana na kipato chako. Hiyo gari mahala unachajiwa boda shs 20,000 yeye ataweka mafuta ya shs 7000 aende tena kwa raha zake. Wewe endelea kupuyanga, kupanga ni kuchagua!
 
Hivi hicho Kigari ukiwa nacho safarini na ile mikimiki ya kuovertake malori huwa mnajisikiaje. Unaweza kumuona malaika Israel huyu hapa.

Wala mimi sina mpango wa kumiliki V8 ntaendelea kupanda daladala maisha yangu yote mpaka pale nitakapoongeza bajeti yangu nivute angalau chuma cha mjerumani na sio kuharakisha kumiliki gari vya bei rahisi mwishowe nionekane kituko
Nimegundua jambo kwa hii comment yako, huyajui magari ama ni mtoto wa mama sana huelewi chochote kuhusu maisha!!! Jifunze kwanza kuhusu magari ndipo utajua hoja uliyotoa ina utoto kiasi gani!!
 
Voltz nayo ni gari?. Ukiendesha unatofauti na dereva wa bajaji, nyie ndio mnaotujazia foleni barabarani siziso na sababu maalum maana Vigari vyenu vimejaa sa road na kujipitisha barabarani.

Utanunuaje gari halafu kipato chako ni kidogo? Mnalazimisha kumiliki gari matokeo yake mnanunua vigari mkiiendesha mnaonekana vituko ni heri kupanda daladala huku mtachanganyikana na kila mtu mwenye kipato tofauti tofauti.
Unatumia nguvu kubwa sana kutujaza iyo mitazamo yako ya kipuuzi tukuone uko correct,yaan huna hata baskel halafu unasema voltz sio gari? Ni Bora ungekaa kimya ufiche ujinga wako, learn how to respect other people's choice!
 
Mimi similiki gari lakini kuna Vigari ukivimiliki unaonekana kituko hasa huku maeneo ya mjini.

Sipo apa kuleta Kashfa ama kukejeli wanaomiliki aya magari ila inabidi niwaambie ukweli ukimiliki starlet unaonekana kituko.

Unakuta jitu lina mwili mkubwa linaendesha starlet halafu vioo kashusha maana hakina Ac, mwili wote unajaa kwenye gari yaani ni vituko halafu unakuta mtu kama huyu anajiamini kumiliki gari Aisee mimi bora niendelee kutembea kwa mguu lakini sio kumiliki hili gari la starlet na aina nyingine za baby Walker.

Kwa leo ngoja niishie apa, nitarudi pindi Mungu akinipa Kibari cha kumiliki gari.View attachment 2743879

Mimi nina Toyota Voltz.

Mtu ambaye hamiliki hata baiskeli, anapata wapi ujasiri wa kuponda aina fulani ya gari?

Ulishawahi kumiliki Bajaj na Starlet hadi ukaona Bajaj ni bora kuliko Starlet? Illogical comparison.

Maliza shule kwanza. Ukishaanza ku hustle utaelewa tu kwamba kuna magari yanayolingana na kipato cha mtu.

Anayevimba kwenye Starlet aliyonunua kwa jasho lake si sawa na wewe uliye nyuma ya keyboard na kuipondea huku ukitoka hapo unagombea daladala tena kwa nafasi tu ya kushika bomba.

Maturity comes with wisdom
Wisdom can guide knowledge 😁😁😁

Knowledge without wisdom is uselessness..
 
Hivyo vigari bora viwe vigari vya delivery, hususan kwa vijana wafanya biashara nchini. Nafkiri wazo zuri kagari kakirembwa na kupendezeshwa kwa rangi, stickers, brandname ya biashara na contacts.

Vijana mfanye hivyo.
 
Umeongea point sana. Hivi ni bora wavipake rangi za matangazo then wafanyie delivery kusafirishia bidhaa kutangaza biashara nk vinavafaa sana
 
Watu kama nyie ndo mnaosababishaga waafrika tuitwe nyani kutokana na mawazo yenu na mambo yenu ya kishamba ,hivi unaipata wapi nguvu ya kusema eti gari fulani haifai kutumika town na kama utaitumia eti utaonekana kituko,Yani unaongea utafikiri kama ni car expert kutoka Toyota kumbe hujui lolote Kwa taarifa Yako ukiona gari ya Toyota imeuzwa sana hadi ulaya basi hio ni gari,na Toyota starlet ni mojawapo ya gari za Toyota ambazo zimenunuliwa sana ulaya tofauti na hizo ist zilizojazana huko unapopaita town,halafu unaonekana bila shaka magari umeyaanza kuyajua juzi,si Kila umwonae anasukuma starlet ukadhani ni chokambaya aisee Yan ni big no ,mfano gari zipo za kutosha tu lakini starlet ni gari pendwa Yan tangu 2003 ni kama family legacy ndo maana tunakatunza.
Mshamba tu huyu boya! Tatizo la kuja mjini ukubwani! Kuna group moja linaitwa Toyota starlet in UK humo utakutana na watu wanapesa za bajeti ya nchi zetu za kiafrica na wanaendesha starlet! Kwaiyo anataka kusema yeye ana akili kuliko wao? This guy has to learn how to respect other person's choices
 
Mtoa mada punguza makasiriko!
Inaonekana upo kwa daladala na umeshikiria bomba halafu kuna foleni, ukitupa jicho pembeni unaona watu na vigari vyao wametulia😁 basi unasonya kwa hasira! Enjoy the life u have!😉
 
Mshamba tu huyu boya! Tatizo la kuja mjini ukubwani! Kuna group moja linaitwa Toyota starlet in UK humo utakutana na watu wanapesa za bajeti ya nchi zetu za kiafrica na wanaendesha starlet! Kwaiyo anataka kusema yeye ana akili kuliko wao? This guy has to learn how to respect other person's choices
Starlet ni gari Kali ndo maana hadi Leo gharama yake ya kununua Kwa Japan ipo juu tofauti na gari ndogo zingine kama ractis,sienta,ist,runx,Alex,porte na funcargo,
Wajapan wanaelewa kama ni chuma kile ndo maana hawataki kushusha price na pia ukiona wanatumia muda mrefu Toyota kutoa new model ya gari husika ujue basi huwa hiyo gari ni reliable,hebu cheki Ile new model ya 2020 ya Toyota starlet,bongo hapa nimeiona mara moja tu.
 
Back
Top Bottom