Wanaomiliki Toyota Starlet wanaonekana vituko wakiwa mjini na Vigari vyao

Wanaomiliki Toyota Starlet wanaonekana vituko wakiwa mjini na Vigari vyao

Kuna kutembea Kwa miguu Kwa maana ya zoezi na kutembea Kwa miguu kukosa nauli au gari, hii ya kukosa gari au nauli sio zoezi Bali ni adhabu
Hakuna anayekosoa hela ya nauli labda mtu mwenyewe apende kwenda sehemu flani kama huna nauli hujalazimishwa kutoka

Kwani anayekosa nauli na mwenye gari anayekosa mafuta wanatofauti gani
 
Mkuu hiyo gari wewe uione tuu hivyo ukizarau ila, jaribu kwenda nje ya nchi zinazojielewa uwone dhamani ya hayo magari madogo madogo ndio utashangaa. Unakuta tajiri anacho hapo kwake na ndio unakuta anatembelea sometimes, magari makubwa yakifahari hayo niya vacation tuu, ila kama hakuna mtoko hayo ndio magari yakutembelea mjini
 
Hii ni forum ya great thinkers kweli? Inafaa kuanza kuwachuja wanao jaza server na kumaliza oxygen kwa kuleta mada zisizo na maana.
Humu kila mtu hutoa kutokana na mawazo yake na mimi nimeamua kutoa mawazo yangu kwa namna moja ama nyingine sijakejeli wa kudharau watu bali nimetoa facts zinazoendana na mawazo yangu
 
Hakuna kadhaa kubwa kama kupanda daladala, ni basi tu hatuna hela ila daladala hapana kwa kweli.

Mwenzako yupo kwa ndinga yake, iwe starlet au VX V8 ni gari yake na anafurahia anachoendesha.
Inategemea unakaa maeneo gani kwa huku kwetu daladala zinatusaidia sana kwenye mizunguko yetu ya maisha hasa ukija mbezi mwisho daladala zimejaa za kwenda kila sehemu unapata siti safi bila kugombania
 
Daladala ni usafiri wa hovyo kabisa, hauna afadhali yoyote, hapo mbezi mwisho napita kila iitwayo leo, ni kero kuanzia mwendokasi hadi hizo daladala, kukanyagana, kuchafuana, kunusishana vikwapa na midomo inayonuka. Huwezi linganisha anayeendesha starket/vitz na anayeshika bomba ya daladala. Tusiwaonee wivu mkuu.
 
Tulia wewe kwanza umekula?
Watu wamegonga sana bata na hivyo vitorori utakua ulikua kwenu unagombea ukoko na watoto wa mjomba.
Endelea kusubiri vieiti,
Hako katoroli mwanza poa tu unafika kwa mafuta buku 20 tu.
Hivi hicho Kigari ukiwa nacho safarini na ile mikimiki ya kuovertake malori huwa mnajisikiaje. Unaweza kumuona malaika Israel huyu hapa.

Wala mimi sina mpango wa kumiliki V8 ntaendelea kupanda daladala maisha yangu yote mpaka pale nitakapoongeza bajeti yangu nivute angalau chuma cha mjerumani na sio kuharakisha kumiliki gari vya bei rahisi mwishowe nionekane kituko
 
Daladala ni usafiri wa hovyo kabisa, hauna afadhali yoyote, hapo mbezi mwisho napita kila iitwayo leo, ni kero kuanzia mwendokasi hadi hizo daladala, kukanyagana, kuchafuana, kunusishana vikwapa na midomo inayonuka. Huwezi linganisha anayeendesha starket/vitz na anayeshika bomba ya daladala. Tusiwaonee wivu mkuu.
Kero za daladala zinategemea na jinsi wewe ulivyoamua kuishi. Kama ni mtu wa kulazimisha kupanda daladala zilizojaa abiria apo utaona kero kila siku. Sasa kwanini ulazimishe kupanda gari lililojaa abiria wakati daladala zingine zipo nyingi tu na hazina abiria
 
Mkuu hiyo gari wewe uione tuu hivyo ukizarau ila, jaribu kwenda nje ya nchi zinazojielewa uwone dhamani ya hayo magari madogo madogo ndio utashangaa. Unakuta tajiri anacho hapo kwake na ndio unakuta anatembelea sometimes, magari makubwa yakifahari hayo niya vacation tuu, ila kama hakuna mtoko hayo ndio magari yakutembelea mjini
Sio kila gari kubwa ni ya vocation, inategemea na mmiliki mbona huku town tunaziona nyingi zikiwa road zikielekea kwenye mishe mishe sametimes wengine wanaenda nazo site, shamba nk
 
Mimi similiki gari lakini kuna Vigari ukivimiliki unaonekana kituko hasa huku maeneo ya mjini.

Sipo apa kuleta Kashfa ama kukejeli wanaomiliki aya magari ila inabidi niwaambie ukweli ukimiliki starlet unaonekana kituko.

Unakuta jitu lina mwili mkubwa linaendesha starlet halafu vioo kashusha maana hakina Ac, mwili wote unajaa kwenye gari yaani ni vituko halafu unakuta mtu kama huyu anajiamini kumiliki gari Aisee mimi bora niendelee kutembea kwa mguu lakini sio kumiliki hili gari la starlet na aina nyingine za baby Walker.

Kwa leo ngoja niishie apa, nitarudi pindi Mungu akinipa Kibari cha kumiliki gari.View attachment 2743879
Hasira na wivu wa maskini ni mbaya sana
 
Sio kila gari kubwa ni ya vocation, inategemea na mmiliki mbona huku town tunaziona nyingi zikiwa road zikielekea kwenye mishe mishe sametimes wengine wanaenda nazo site, shamba nk
Kila gari imetengezwa kwa ajili ya shuhuli fulani, huwezi kuwa na SUV ukaipa majukumu ya pickup au huwezi kuwa na pickup
 
Back
Top Bottom