Wanaomkosoa sana Samia sasa hivi ndio watakaomkumbuka siku Mwigulu au Makonda ndio Rais wa Tanzania

Wanaomkosoa sana Samia sasa hivi ndio watakaomkumbuka siku Mwigulu au Makonda ndio Rais wa Tanzania

Johnny Sack

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2017
Posts
8,984
Reaction score
19,288
Tanzania ina matatizo mengi, na Samia anastahili lawama kwa baadhi ya matatizo yanayoikabiki Tanzania kwa sasa kama hili la mgao wa umeme n.k

Lakini kama wewe unaamini kama mimi kuwa maendeleo ya watu yanapaswa kuendana na uhuru, umoja na mshikamano wa taifa yafaa tukumbuke tulikotoka na ku appreciate machache Samia aliyoyafanya, na sio kumdhihaki kila siku kwa vigezo vya asili yake, jinsia au kutweza heshima yake

Ama tutakuja kumkumbuka sana siku amestaafu na Mwigulu Nchemba (Savimbi) ama Daudi Albert Badhite ndio rais wa nchi hii

Eddo Kumwembe ni kati ya watu wachache ambao genuinely wana appreciate machache aliyoyafanya Samia ambayo hatuna uhakika kama tutaendelea kuwa nayo siku akiondoka madarakani

Screenshot_20231229-125545.png
 
Wanaomkosoa kwa vishindo Samia ni wale waliokuwa wanamsifia mtangulizi wake.
Naye akiondoka hawa wanaomsifia mama leo ndiyo wataomkosoa rais mpya.
Ni haki ya kila mtu kusifu, kuksoa, kubeza nk.
Kubwa ni kwamba Tanzania sasa kuna uhuru wa mawazo.
Tanzania ya leo siyo ya jana, unaweza kumkosoa rais wa nchi popote na bado unabaki kuwa huru
 
Matumaini yetu Wapenda HAKI yalikuwa makubwa Samia alipokuwa Rais wa GHAFLA tulijua ni OUTSIDER na MWANAMKE kutoka Visiwani tukawa tunasema MABADILIKO MAKUBWA yanakuja. Daah!!! GHAFLA SIO YULE BIBIE WA MARASHI YA KARAFUU KANOGEWA NA KITI KAAJIRI MACHAWA KILA KONA.

KAANZA KUTUHADAA NA KUTULAGHAI NA SASA HIVI ANAPANGA KUPORA UCHAGUZI .

ATI KUNA WENGINE WANASEMA ANAWAOGOPA WAHAFIDHINA MAKONDA SIO MUHAFIDHINA NI MUUAJI.

MARASHI YA KARAFUU YAMEVUNDA WANAYAWASHIA UBANI LAKINI WAPI BORA HAO KINA MADELU WANAJULIKANA NI WEZI WAKIINGIA TUTAJUA MOJA KUWA WEZI WAMEINGIA "RASMI".

LAKINI MAMA HATUJUI AMESIMAMIA WAPI ANATUHADAA WAZI WAZI BILA HATA AIBU.

TUNAJUA AMEPANGA KUPORA UCHAGUZI BASI ANYAMAZE ANATUHADAA NA KUTULAGHAI KWANINI.

6_bonobos_WHCalvin_IMG_1341 (1).jpg

TIMESALITIWA NA HUYU MAMA TUMEACHWA KAMA MAYATIMA.
 
Wanamkosoa kwa vishindo Samia ni wale waliokuwa wanamsifia mtangulizi wake.
Naye akiondoka hawa wanaomsifia mama leo ndiyo wataomkosoa rais mpya.
Ni haki ya kila mtu kusifu, kuksoa, kubeza nk.
Kubwa ni kwamba Tanzania sasa kuna uhuru wa mawazo.
Tanzania ya leo siyo ya jana, unaweza kumkosoa rais wa nchi popote na bado unabaki kuwa huru
wengi wanaomkosoa Samia ndio walewale waliokuwa wanamkosoa mwendazake wakawa wanamkumbuka Kikwete. Na ndio hao hao waliokuwa wanamkosoa Kikwete na kusema hii nchi inahitaji rais dikteta
 
By the way hawana hoja za msingi ila kutafutiza mambo ya kipumbavu.

Huwezi kuwakuta wakitoa takwimu za Elimu,maji, uchumi, miundombinu nk.
Samia analipwa mshahara ili kutekeleza hayo yote, pamoja na mengine, ikiwamo umeme. Kama mwajiriwa wetu hatuna haja ya kumsifu eti sababu ya miradi fulani iliyotekelezwa. Ni sehemu ya wajibu wake kusimamia hayo, na tumemlipa. Kwa yale ambayo yeye na serikali wameshindwa, tena kwa uzembe, yeye kama kiranja mkuu anapaswa kubeba lawama zote. Mfano ni kama ktk familia: mzazi hawezi kusifiwa sababu watoto wameshina, na wanalala, lakini hajawalipia ada ya shule, au hajawalipia bima ya afya.
 
Basi tutamsifia mkeo
 
Usikereke, hiyo Ni kawaida ya wanadamu.

Kuna wakati watu hawathamini kile unachokifanya kwa ajili yao mpaka utakapoacha kukifanya.

So si kitu Cha ajabu. Alipokuja mkwele watu wakamkumbuka mzee wa lupaso.

Alipokuja jiwe watu wakamkumbuka mkwele. Kaja mama Abdul Sasa watu wanamkumbuka jiwe.

Yajayo yanafurahisha.
 
Huyu mama kwa nchi zilizo serious kabsa, hafai hata kuwa Mtendaji wa Kata tupilia mbali Ubalozi wa nyumba kumi.
 
Kwani Mwingulu na Samia,Characters & Style za kuendesha Serikali zina tofauti gani
 
Back
Top Bottom