Wanaomlaumu na kumshambulia Prince Dube ni watu wasiojua mpira

Rudia kusoma uzi
Hujanielewa, nilikuwa nasapoti motion yako. Wengine wanaona ni mbovu wakati wewe unaona anafaa si kufunga bali assist. Ndiyo nikasema abadilishiwe majukumu ndani ya uwanja kama unavotanabaisha kuliko kutompanga
 
Hujanielewa, nilikuwa nasapoti motion yako. Wengine wanaona ni mbovu wakati wewe unaona anafaa si kufunga bali assist. Ndiyo nikasema abadilishiwe majukumu ndani ya uwanja kama unavotanabaisha kuliko kutompanga
Yah apunguziwe majukumu ya kufunga
Apewe hayo mengine ambayo anayafanya Kwa ufasaha na yanasaidia timu
 
Unatukosea heshima wana Yanga.
Mbaya zaidi unawakisea adabu na heshimu Roberto Firmino na Fernando Torres. Hao wilwili lini uliwaona wanashikwa kitete, mchecheto, au wenge wakiwa na mpira mbele ya goli?

Lini walipata pressure na woga mbele a Kopites pale Anifield ikiwa imejaa mashabiki kwenye Europian night?

Shida ya Prince Dube ni hofu au kitete siyo kwamba hajui. Sasa mchezaji wa umri wake hawezi kubadilika tena akiwa kwenye timu kubwa yenye shabiki wengi. Huyo mambo mawili tu.
Mosi aachwe aondoke zake au pili timu imtafutie mwanasaikolojia professional kutoka Ulaya siyo Afrika. Sasa hiyo option 2 Ina gharama kubwa bora tuachane naye.
Kama tumeacha watu muhimu Kama Aucho, Gamond, Lomalisa hatushindwi kwake labda Kama Kuna udalali kwenye malipo yake. Anatugharimu pakubwa. Aachie nafasi tujaribu wengine.
NB: Kaangalie video za Firmino jinsi alivyokuwa na utulivu akiwa ndani ya boksi. Huyo Torres ndiyo hatari, habari nyingine kwa kufunga akiwa LFC.
 
Kwenye akili zenu mmejiaminisha Dube ni mshambuliaji wa viwango vya juu sana, ila kiuhalisia hayupo hivyo.
Sasa shida inakuja pale mnachoamini na uhalisia havilingani.

Mkipunguza mategemeo ndo mtajua ni daraja gani huyu mtu anapaswa kuwepo.
 
Me napenda movements zake Ile pumzi ya Dube kuwa nayo sio kawaida.
Nadhani yeye yupo ivo na coach akiongea nae ampe majukumu sio ya kufunga sana Bali ku link timu ili Pacome, Doumbia, Kouma, Mzize na Ecua wafunge sana
Hata sub aliomba sio kwamba kachoka ni vile tu yaliyotokea

Uliona boyeli dakika chache tu alikuwa anatepeta?

Dube ni mwanaume sana basi tu mimi naona ajengewe uwezo wake wa kujiamini zaidi tusimlaumu
Tukumbuke msimu uliopita alikuwa na assist ngapi na alihusika kwenye magoli mangapi

Jamaa mtu sana kuna vi movement anafanyaga dah hatari
 
Shida ya Dube siyo local matches.
Shida mechi kubwa za kimataifa.
Unapo muhitaji ajitokeze wakati muhimu yeye ndiyo anapotea na kuwapoteza wenzie kisaikolojia anapo kosa kuzitumia nafasi muhimu. Anaivuruga timu yote kwa pressure.
 
Dube ni kweli anapoteza nafasi nyingi, lakini tukumbuke hizo nafasi anazozikosa hazijileti zenyewe, ni yeye anaezitafuta, akicheza mshambuliaji mwingine hizo nafasi huwa hazionekani au zinakua ni chache sana, ili Dube afanye vizuri inatakiwa acheze na striker mwingine kama Mzize au Boyeli, na msimu uliopita Dube amekua akifanya vizuri anapocheza na Mzize.
 
Nakubaliana na wewe kuwa Dube ana weaknesses kadhaa kama ulivoeleza, lakini angalia potential yake ambayo Kwenye tactics ni muhimu
Last season Dube ndo striker mwenye assists nyingi, ulivoona akina Pacome na Azizi wanafunga sana, ungepata utulivu ungeona kazi kubwa ya Dube
 
Yah akikosekana ndo tunamkumbukaga.
Haya hakucheza Malawi timu ikapoteza.
Siku hizi strikers ambao wapo clinical ni wachache mno duniani labda kama Lewandoski, Kane na Haland tu

Angalia ligi nyingi top scorers sio namba 9
England top scorer ni Salah sio namba 9
Spain top scorer ni Mbape
France top scorer ni Greenwood sio namba 9
Italy Mateo Retegui sio namba 9
 
Kwenye mpira striker hata kupata nafasi ya kukosa goli ni ngumu kupata mpaka ufanye movements nyingi za nguvu na akili kubwa
 
Umeandika vyema sana na kimpira. Ninaweza nikamlaumu Dube kwa muendelezo wa kutoweza kufanya jambo sahi pale anapokuwepo sehemu sahihi. Kwa wanaomlaumu kwa matukio ya jana watakuwa wanakosea sana.
Ninachokiina kwa Dube siyo kukosa fitness, nikionacho mimi ni anasaikological challenge, uongozi unapaswa kumsaidia hapo
 
Dube ni mzuri na Akiwa uwanjani anatengeza nafasi nyingi sana Kitu ambacho ni kizuri, Kutengeneza tu izo chances tayari inaonesha dube ni striker mzuri
 
Shida ya Dube siyo local matches.
Shida mechi kubwa za kimataifa.
Unapo muhitaji ajitokeze wakati muhimu yeye ndiyo anapotea na kuwapoteza wenzie kisaikolojia anapo kosa kuzitumia nafasi muhimu. Anaivuruga timu yote kwa pressure.
Sawa mkuu

Ila kosa la kwanza lilikuwa kumuacha mayele yule jamaa alikuwa striker hasa ila sio kosa letu sasa wenye pesa tusingeweza ku battle nao
Pyramid wenyewe hawataki kumuachia wanajua wakimuacha kupata striker inakuwa ngumu tena maana sokoni kuna upungufu.

Tulishajaribu sana kutafuta striker kwa kila namna konkoni, guede, kambole wote hao wameshindwa kuvaa viatu vya mayele

Na sasa dube angalau anatupa namba nzuri shida yake ndio kama ulivyosems hapo nadhani anacheza kwa pressure sana kichwani mwake na mashabiki wanamuandama sana.

Aachwe acheze mpira tu mpaka mwishoni mwa msimu namba zake tutaangalia mkuu
 
Nakuelewa saana mkuu. Upo sahihi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…