Wanaoongea peke yao wanazidi kuongezeka

Wanaoongea peke yao wanazidi kuongezeka

kweli mkuu yaani mtu anakuwa anafanya vikao vya ndani mpaka anaongea mwenyewe. unaweza ukamkuta mtu anawaza sana ukamshtua na kumdanganya kuwa ulikuwa unaongea peke yako na akaamini
 
inasikitisha sana. kuna kijana, rafiki yangu naona siku zinavosonga mbele haka kaugonjwa kanazidi kukua kwa kasi. mwanzoni alionekana akifanya mahesabu makali sana kimya kimya kwa msaada wa vidole vya mikono, siku hizi amebadili style. anawaza kwa sauti njiani. inafika mahali akikosea jambo anajiadïbu mwenyewe aidha kwa kujikoa au kujinasa kibao stahiki shavuni. so sad!
 
Mshana Jr ...nisaidie nijue na wale wanaotingisha vichwa tatizo lao n nn?
Kuna wenye tatizo la kineva
-kujipangusa uso kila mara
-kutikisa kichwa
-kushtuka
-kuuma meno/mdomo ndani na nje/ulimi
-kujilamba lips
-kufinya macho
-kuchezesha midomo /mashavu/paji la uso
Hutokea bila kutaka (involuntary )na ni kila baada ya muda fulani hasa mtu akiwa anatatizwa na jambo fulani
 
inasikitisha sana. kuna kijana, rafiki yangu naona siku zinavosonga mbele haka kaugonjwa kanazidi kukua kwa kasi. mwanzoni alionekana akifanya mahesabu makali sana kimya kimya kwa msaada wa vidole vya mikono, siku hizi amebadili style. anawaza kwa sauti njiani. inafika mahali akikosea jambo anajiadïbu mwenyewe aidha kwa kujikoa au kujinasa kibao stahiki shavuni. so sad!
Muwahisheni hospital athari zisije kuwa kubwa zaidi medulla imeanza kucheza
 
Maisha yana maajabu mengi na mojawapo ni hili la watu kuongea pekeyao. ...achana na mazungumzo ya kimya achana na mawazo ya kawaida...hiki ni kitu kilichojengwa katika wizara nyingine kabisa wizara ya mawazo halisia
Sio wendawazimu sio vichaa hawajarogwa hawajalewa ni watu wana akili zao timamu na familia zao na kazi zao lakini wanaongea pekeyao barabarani
Ni changamoto za maisha na mikwamo mingi ndio husababisha yote haya
Migogoro kwenye mahusiano
Changamoto za kipato
Matumizi ya kila siku
Watoto Shuleni
Kodi za nyumba
Madeni
Ndugu...!
d729d3f53c6c09178ec38b59a2ae8e4b.jpg
Inafika mahali mtu anawaza kwa sauti anaongea na kujijibu mwenyewe, yani katengeneza nafsi mbili kwenye moja anauliza anajijibu anabisha anabisha anashangaa yeye huyo huyo anafikia maamuzi au anasonya au anatukana yeye huyo huyo
Anaweza kutoka ubungo mpaka kimara bila kujijua
Anaweza kukujibu kuwa na fahamu kamili
Ukikutana na mtu kapatwa na ajali ya kugongwa au kugonga usikimbilie kumlaumu ....watu wamebeba mizigo mingi kichwani
Pamoja na changamoto zote ulizo nazo jitahidi Usiwe mmoja wao
.
Mshana hiyo hali ishawahi kunikumba miaka kadhaa iliyopita lkn mimi nilikuwa najihoji na kujijibu peke yangu kimoyomoyo huku nikiishia kutikisa kichwa na chanzo ilikuwa kudhulumiwa katika biashara ya mbao miaka ya 1999 na 2000. Nilianza biashara ya mbao kuzitoa maeneo ya Ushirombo kijiji cha Mwanzayamadaso nikinunua miti ya mininga na kusafirisha mbao kuzileta Kakola Kahama, sasa nikawakabidhi wachana mbao hiyo miti na baadhi ya mbao ambazo walikuwa wamechana ili mzigo uwe mkubwa harafu nikodi matera ya kukokotwa na ng'ombe hadi Kakola!! Sasa wale jamaa niliporudi kufuatilia pesa kwa matajiri huku nyuma wakaalikana wakachana mbao na kuchana miti yote na mbao zile za kwangu wakauza zote na msumeno mmoja niliokuwa nimenunua!! Baadae wakaandaa mazigira kuwa walikamatwa na bwana miti hivyo mbao na msumeno wangu ulichukuliwa!! Kumbuka huwezi kushitaki kwa kuwa ni illegal business. Mwanangu nilikuwa natembea naongea hasa baada ya mmoja wao kuniambia A-Z na aliyechonga huo mchongo!! Nilifikiria sijui nikodi watu wakamtoe uhai baadae nikarejea mafundisho yetu kuwa samehe saba mara sabini. Hivyo mimi nikimuona mtu wa hivyo mara nyingi kama niko kwenye biashara yangu huwa namuita na kuanzisha story za mbali baadae atafunguka na kukuambia na ndipo tampatia ushauri. Kuna mmoja alikuwa anaongea hadi anajipinga mapajani makofi na kichwani mwanzoni nilifikiri ameanza kutumia bangi kumbe masikini alikuwa anuguliwa mke na watoto magojwa ya ajabu (yasiyotibika hospital zetu isipokuwa kwa waganga wa jadi). Baadae walipopona sijamuona tena na hali hiyo.
 
Haswa humu mtandaoni, watu wamezidi kuongea peke yao….
Mhuku humu tunaongea wote tumechanganyikiwa kiasi. Imagine Mshana Jr. mimi na wengine masaa yote ya kuwa macho tumo JF kweli tutakuwa wazima. Unacheka, unalia, unatukana, unasahau ulikoanzia halafu unakuja jibu lisilohusu. Ni ka ugonjwa. Mimi naomba tiba ili niondokane na ka JFmiligne naumwa ndo maana nasahau hata chai kwenye kikombe. Nite nite ikiwezekana.
 
Mhuku humu tunaongea wote tumechanganyikiwa kiasi. Imagine Mshana Jr. mimi na wengine masaa yote ya kuwa macho tumo JF kweli tutakuwa wazima. Unacheka, unalia, unatukana, unasahau ulikoanzia halafu unakuja jibu lisilohusu. Ni ka ugonjwa. Mimi naomba tiba ili niondokane na ka JFmiligne naumwa ndo maana nasahau hata chai kwenye kikombe. Nite nite ikiwezekana.
Hahhahahaaaa niah bwana...! Ila kuna kaukweli ndani yake
 
Hahhahahaaaa niah bwana...! Ila kuna kaukweli ndani yake[/QU OTE]
We naona nizime Chrome yangu nikalale sababu mimi sasa natumia giga zaidi ya 10 kwa mwezi kweli is this health? Naomba mods watuwekee kiwango cha kuingia.
 
Back
Top Bottom