Wanaoongea peke yao wanazidi kuongezeka

Wanaoongea peke yao wanazidi kuongezeka

Ukiwa hujapitia hiyo stage basi jua bado una safari ndefu sana ,kuongea mwenyewe,sleepless nights
mkuu mi hata sjafka 25 na nipo stage hyo na naona kama safar yangu inaishia hapa..maisha haya
 
ASUBUHI YA LEO NIMEKUTANA NA MEU GHAFLA NAMSIKIA AKISEMA MAMBO MAGUMU AKARUDIA TENA KUSEMA MAMBO YAMEKUWA MAGUMU SANA NIKAMPITIA MWALI NKAJUA GARI IMEWAKA ASIJENICHAPA MAKOFI BURE
 
Maisha yana maajabu mengi na mojawapo ni hili la watu kuongea pekeyao. ...achana na mazungumzo ya kimya achana na mawazo ya kawaida...hiki ni kitu kilichojengwa katika wizara nyingine kabisa wizara ya mawazo halisia
Sio wendawazimu sio vichaa hawajarogwa hawajalewa ni watu wana akili zao timamu na familia zao na kazi zao lakini wanaongea pekeyao barabarani
Ni changamoto za maisha na mikwamo mingi ndio husababisha yote haya
Migogoro kwenye mahusiano
Changamoto za kipato
Matumizi ya kila siku
Watoto Shuleni
Kodi za nyumba
Madeni
Ndugu...!
d729d3f53c6c09178ec38b59a2ae8e4b.jpg
Inafika mahali mtu anawaza kwa sauti anaongea na kujijibu mwenyewe, yani katengeneza nafsi mbili kwenye moja anauliza anajijibu anabisha anabisha anashangaa yeye huyo huyo anafikia maamuzi au anasonya au anatukana yeye huyo huyo
Anaweza kutoka ubungo mpaka kimara bila kujijua
Anaweza kukujibu kuwa na fahamu kamili
Ukikutana na mtu kapatwa na ajali ya kugongwa au kugonga usikimbilie kumlaumu ....watu wamebeba mizigo mingi kichwani
Pamoja na changamoto zote ulizo nazo jitahidi Usiwe mmoja wao
.

Mkuu, umenikumbusha miaka ya nyuma kulikuwa jamaa mmoja alikuwa wenyekiti wa CCM na muda wote alivaa suruali nyeusi na shati la kijani.

Kwa bahati mbaya (nasema bahati mbaya kwa sababu hatua hizi huwa ni haramu wa ccm) akastafishwa kazi. Hapo ndipo shughuli ikawa kubwa.

Alikuwa anatembea na nguzo zake za kijani na nyeusi. Akifika kwenye maashamba ya mitama au mahindi yamestawi wakati wa kilimo, halafu mahindi na mitama ikiyumba kwa tune ya upepo, atasimama na kuiangalia muda mrefu sana na kisha ananyoosha mkono wake wa kulia na kusema kwa sauti "Kidumu Chama Cha Mapind..".

Kumbe muda anapokuwa anashangaa mimea ile ikiyumba na upepo, anakuwa anaona ni wanachama wa ccm wamevaa jezi wakiimba "Ccm ccm".

Nakubali kabisa kwamba kwa hali ya maisha jinsi ilivyo na inavyozidi kuwa ngumu huku watu wakizidi kupoteza matumaini, mambo ya kusema mtu pekee yatazidi kuongezeka tena kwa kasi..

Mungu asaidie Tanzania na vijana wetu. Ajira hakuna, maisha magumu, kutoa mapendekezo hakuna!. Sasa mwisho wake ni nini kama siyo huo?
 
Hapa pa kuona mimea na kudhani ni wanachama nimejikuta nacheka pekeyangu japo inaumiza kama ni ndugu yako
 
Back
Top Bottom