Wanaoongea peke yao wanazidi kuongezeka

Wanaoongea peke yao wanazidi kuongezeka

Kuna tatizo kama ugonjwa na kuna tatizo kutokana na kuwaza sana inabidi ujue ni lipi mojawapo hapo
Mimi naongea.nacheka mwenyewe sana tu. Kuna kipindi unaenda kumuona mtu basi naanza kuongea jinsi nitakavyomhoji na majibu yake, najijibu mwenyewe hhadi nacheka! Inawezekana kichaa kinaninyemelea?
 
Mimi naongea.nacheka mwenyewe sana tu. Kuna kipindi unaenda kumuona mtu basi naanza kuongea jinsi nitakavyomhoji na majibu yake, najijibu mwenyewe hhadi nacheka! Inawezekana kichaa kinaninyemelea?
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Kucheka au Kutabasamu mwenyewe maisha bana "who doesn't like fantasies"! Mi nshakuwa kilema nikiwa eneo moja kwa muda kidogo especially nikiwa bored mind lazima ishifti!Daah!Hatari sana.Nikiwa na earphones nasikiliza music ndo majanga kabisa iko siku manusura nife nimeweka earphones nakula madudez mind iko mwezini hamadi!Sema gari halikuwa kwenye mwendo mkali.
 
Haha! Ilibidi tu lakini kila nikifikiriaga naona ulikuwa ni utoto.
Ni utoto wenye ubunifu mzuri kulazimisha mkono usioweza kuandika uushindanishe na unaoweza ni kipaji na ubunifu mkubwa.....
 
Ni utoto wenye ubunifu mzuri kulazimisha mkono usioweza kuandika uushindanishe na unaoweza ni kipaji na ubunifu mkubwa.....
Na amini mkuu,mpaka sasa hv bado naandikia mikono yote ila wa kushoto umeuzid ujanja wa kulia......uliokuwa superior than the other.....
 
Maisha yana maajabu mengi na mojawapo ni hili la watu kuongea pekeyao. ...achana na mazungumzo ya kimya achana na mawazo ya kawaida...hiki ni kitu kilichojengwa katika wizara nyingine kabisa wizara ya mawazo halisia
Sio wendawazimu sio vichaa hawajarogwa hawajalewa ni watu wana akili zao timamu na familia zao na kazi zao lakini wanaongea pekeyao barabarani
Ni changamoto za maisha na mikwamo mingi ndio husababisha yote haya
Migogoro kwenye mahusiano
Changamoto za kipato
Matumizi ya kila siku
Watoto Shuleni
Kodi za nyumba
Madeni
Ndugu...!
d729d3f53c6c09178ec38b59a2ae8e4b.jpg
Inafika mahali mtu anawaza kwa sauti anaongea na kujijibu mwenyewe, yani katengeneza nafsi mbili kwenye moja anauliza anajijibu anabisha anabisha anashangaa yeye huyo huyo anafikia maamuzi au anasonya au anatukana yeye huyo huyo
Anaweza kutoka ubungo mpaka kimara bila kujijua
Anaweza kukujibu kuwa na fahamu kamili
Ukikutana na mtu kapatwa na ajali ya kugongwa au kugonga usikimbilie kumlaumu ....watu wamebeba mizigo mingi kichwani
Pamoja na changamoto zote ulizo nazo jitahidi Usiwe mmoja wao
.
kwahiyo tunaweza kuita ni stress au msongo wa mawazo;?na ikikutokea kuna tiba?mwenyewe huwa unajua kama unafanya mambo hayo peke yako?maswali ni mengi,nina hofu ya kukuchosha
 
kwahiyo tunaweza kuita ni stress au msongo wa mawazo;?na ikikutokea kuna tiba?mwenyewe huwa unajua kama unafanya mambo hayo peke yako?maswali ni mengi,nina hofu ya kukuchosha
Usijali uliza tu huwa sichoki kujibu kwa kile ninachokijua
Hawa wanaongea ukiachana na ugonjwa kama wa kichaa ni watu ambao wanaongea mawazo yao kwa sauti au wanawaza kwa sauti ...yani mambo yanamzidi mpaka mawazo anayaleta kwenye uhalisia mdomoni
 
Back
Top Bottom