Wanaopewa fidia ili wahame bonde la Msimbazi, itawatosha kununua kiwanja na kujenga?

Kwani saizi Serikali inawatoa Ili ifanyaje Sasa.

Tzn ni kubwa unakaa Mabondeni harafu useme Serikali imeshindwa wajibu wake? Hapo pote ni catchment area.

Kwanza wanatakiwa kufurushwa wote ni huruma tuu Samia anafanya.
Hilo eneo lilikua ni la serikali au wananchi?
Ikiwa ni la wananchi , mwananchi atakaekataa kupokea pesa akataka abaki eneo hilo serikali itamuondoa kwa lazima?
 
Au wakae mafuriko yakija wakae nayo kikao yawalipe fidia.
 
Hilo eneo lilikua ni la serikali au wananchi?
Ikiwa ni la wananchi , mwananchi atakaekataa kupokea pesa akataka abaki eneo hilo serikali itamuondoa kwa lazima?
Sioni ulazima wa kuondolewa kwa nguvu. Asiyetaka aachwe tu. Unless serikali ina mpango na hilo eneo ila kama ni hatari ya mafuriko na elimu ishatolewa tuachwe tu sisi ni watu wazima tutaogelea.
 
Hata hivyo Mheshimiwa Rais amewahurumia tu hata kuwapa kiasi hicho! Vinginevyo wangepaswa kubomolewa nyumba zao! Kumbuka Serikali kwa muda mrefu imekuwa ikiwataka watu wanaoishi mabondeni wahame lakini wananchi wamekuwa wakikaidi.
 
Watu na roho zenu za wivu
 
Eneo hatarishi kwa mantiki ipi? yaani serikali kushindwa wajibu wake kujenga kingo za mto kuuthibiti usifurike kwenye makazi ya watu lawama unakuja kuwatupia wananchi? Hizo kodi wanazokusanya ni kwa ajili ya kufisadi tu na kujinunulia ma viieite.​
Chief, lile eneo watu wamevamia sio makazi ya watu, na hii ni Tabia yetu Watanzania, tunavamia maeneo kwavile tunaachwa tunakaa kwa muda mwisho tunaona kama ni Haki yetu.
Mifano ipo mingi, ukienda Kinyerezi mwisho kuna umeme mkubwa umekatiza, na Tanesco wameweka umbali wa kukaa Karibu na zile nyaya, lakini kuna watu wamejenga hatua mpaka mbili na wengine kufungua biashara chini ya zile nyaya za umeme, siku wakipata madhara au wakitaka kuondolewa utasema walipwe fidia? hiyo 4M ni hisani Tu, vinginevyo wawaache mafuriko yawahamishe.
 
Watu wa jangwani waliwahi pewa viwanja kule mabwepande, waliviuza na wakarudi jagwani.

Hapo hata uwape milioni mia hawaondoki.

Mtaishia kutishiana uchawi tu.
Nini kifanyike? Kwa ambao hawajakubali kuondoka hapo bonde la msimbazi.!?
 
Hilo eneo lilikua ni la serikali au wananchi?
Ikiwa ni la wananchi , mwananchi atakaekataa kupokea pesa akataka abaki eneo hilo serikali itamuondoa kwa lazima?
Mwananchi unakaa Mabondeni kufanya nini? Ni eneo halituhusiwi Kwa makazi
 
Pembezoni mwa Dar kuna viwanja vya kuanzia bei ya laki 1 hadi laki nane.

Kuna vya milioni na milioni na nusu.

Kuna mashamba hekari moja laki 2 hadi laki 8.

Maana yake mtu anabaki na hela ya kujenga chumba kimoja ambacho ndicho kapanga hapo. Maana mtu anaweza kuhoji kwamba chumba kimoja hakitoshi.

Sasa sijui ni kwa sababu gani mtu ang'ang'anie kukaa kwenye madimbwi kama chura.
 
Hiyo 4m ukiipata usipojipanga vizuri inayeyuka bila kufanya jambo lolote la maana.
 
Wapi huko unaweza kutaja majina ya hayo maeneo
Vikindu (laki 5), Kisarawe pale Mzenga Centre laki 8.

Kisarawe shamba laki 2-4 kwa eka.

Kibaha milion na nusu kiwanja/shamba.

Chalinze shamba laki na nusu hadi laki 8.

Mlandizi, Bagamoyo n. k
 
Hakuna Mahala walitaja neno fidia ni Kifuta jasho
 
Vikindu (laki 5), Kisarawe pale Mzenga Centre laki 8.

Kisarawe shamba laki 2-4 kwa eka.

Kibaha milion na nusu kiwanja/shamba.

Chalinze shamba laki na nusu hadi laki 8.

Mlandizi, Bagamoyo n. k
Sawa lakini huko sio Dar ni mkoa wa Pwani
 
Mkuu

Wanalipwa mara ngapi wakati mwaka 2014 kuelekea 2015 walilipwa na serikali na wakapewa viwanja Mabwepande ambavyo walivitelekeza matajiri wakavichukua?

Nilivyosikia mwanzo fidia wanayopewa ni shilingi milioni nne na tathimini iliyofanywa na serikali kuna idadi ya watu 2,400 watakaoathirika na kupitiwa na mradi kwenye bonde la Msimbazi.

Kama fidia ni sh milioni 4 kwa watu 2,400 serikali itawajibika kuwalipa jumla ya shilingi bilioni 9.6. Lakini kama watatumia kiwango ulichotaja hapa cha shilingi mil 6 serikali itawatoka shilingi bilioni 14.4

Maswali ya kujiuliza kwanini watu wanakuwa wanalipwa mara mbili mbili ni kwa manufaa ya nani?

Kwa maoni yangu serikali inunue maeneo yote ya Magomeni mapipa na Magomeni Mzimuni ili wajenge au kuingia ubia na sekata binafsi kujenga miundo mbinu rafiki kwa mazingira ya bonde la Msimbazi.
 
Sawa lakini huko sio Dar ni mkoa wa Pwani
Kwamba hawaruhusiwi kwenda huko?

Kwa taarifa yako Dar imejaa. Ukitaka kiwanja dar uwe na hela kuanzia milioni kumi. Na hapo unapata kuanzia Mbezi Malamba Mawili kuelekea Kibamba.

Kwani hao toka wanaishi hapo ni milioni ngapi zimepita mikononi mwao?
 
Kwamba hawaruhusiwi kwenda huko?

Kwa taarifa yako Dar imejaa. Ukitaka kiwanja dar uwe na hela kuanzia milioni kumi. Na hapo unapata kuanzia Mbezi Malamba Mawili kuelekea Kibamba.

Kwani hao toka wanaishi hapo ni milioni ngapi zimepita mikononi mwao?
Sawa ila tumekubaliana kuwa hayo maeneo ni mkoa wa Pwani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…