Wanaopewa fidia ili wahame bonde la Msimbazi, itawatosha kununua kiwanja na kujenga?

Ujenge mtoni wewe afu hadara uisingizie jamuhuri ya muungano wa Tanzania. Ingewezekana hata wakaondolewa bila malipo kwa maana ni kwa ajili ya usalama wao kwanza. Imagine wangebebwa na maji. Wale waliopo sehemu zisizo njia ya maji walipwe fidia sawa sawa na mali zao
 
Ni mtaji wa kubet nenda kabet kwa bukubuku hadi iishe utabahatisha hela ya kiwanja na kujengea chumba kimoja
 
Kwani milioni 4 si kwa ajili ya ardhi tu na jengo linathaminiwa kivyake ama mimi sikuelewa!?

Mara nyingi naipinga serikali ila mwa hili wapo sahihi, hiyo pesa ni msaada tu. Viwanja vya milioni 4 nje ya mji vipo vingi tu.
 
Kwani milioni 4 si kwa ajili ya ardhi tu na jengo linathaminiwa kivyake ama mimi sikuelewa!?

Mara nyingi naipinga serikali ila mwa hili wapo sahihi, hiyo pesa ni msaada tu. Viwanja vya milioni 4 nje ya mji vipo vingi tu.
Tatizo hawa watu wana umasikini ambao chanzo kikuu ni ukosefu wa mipango. Hawana mipango kwa sababu hawana akili.
 
Sioni ulazima wa kuondolewa kwa nguvu. Asiyetaka aachwe tu. Unless serikali ina mpango na hilo eneo ila kama ni hatari ya mafuriko na elimu ishatolewa tuachwe tu sisi ni watu wazima tutaogelea.
Unatakiwa uchapwe na viboko kichwa ngumu aina yako!
 
Dah bongo raha sana hizo 4m ni ndogo waendelee kukaa pale pale mpka wafe serikali sio lazima izingatie watu wake maana usalama wako upo mikononi mwa mungu baba muumba
 
Hawawezi kwenda huko,wengi wao( kama sio wrote) wanategemea kufanya shughuli ndogondogo katikati ya mji,hususani kkoo ili kujikimu.Kuwashauri waende chalinze au msata huko hawawezi kuelewa.
 
Hapo serikali itafute eneo Kigamboni au Mkuranga,wajenge vijumba kama vile vya Msomera vya Masai wa Ngorongoro.Kisha wenye nyumba wote kila mtu akabidhiwe nyumba yake na Wapangaji kila mtu milioni 1.Alafu kijiko cha Jiji kije kusawazisha nyumba zote,tuone kama Kuna mtu atarudi kukaa pale.
Watu wengi wanaoishi pale ni Walala hoi na wachache sana ndiyo wanajiweza!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Naona wasipewe hata Senti tano watimuliwe tu,kama mtakumbuka Kwa wale old school sio,vitoto vya 2000 ha a watu wa msimbazi walipewa viwanja bureeee mabwepande,mbona wamerudi Tena?
Wabishi waache wake hapo hapo.
 
Kwani wewe ulipokuwa unajenga hukujua kama unajenga katika mkondo wa maji walishapewa viwanja mabwe pande wakauza wakarudi tena palepale eti serikali ya ccm Kwani ndiyo iliyokuuzia
 
HAO WATU HAWAKUPEWA VILE VIWANJA NA SERIKALI BALI WALIVAMIA HAYO MAENEO
SERIKALI ILIWAKATAZA KUJENGA KTK HAYO MAENEO LAKINI WALIKAIDI KWA NINI LEO SERIKALI IBEBE JUKUMU LISILO LAKE
ANGALAU HATA SERIKALI ILIVYOAMUA KUWAPA HATA HIZO FEDHA

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
Kwani saizi Serikali inawatoa Ili ifanyaje Sasa.

Tzn ni kubwa unakaa Mabondeni harafu useme Serikali imeshindwa wajibu wake? Hapo pote ni catchment area.

Kwanza wanatakiwa kufurushwa wote ni huruma tuu Samia anafanya.
Hili jambo wengi wanalichukulia kwa ujumla wake na wanashindwa kulijua kwa undani wake!
Kwanza, fidia ya maeneo ya bonde la Msimbazi ni msimamo wa World Bank (wafadhili wa mradi)! Serikali haikuwa na nia ya kuyatoa fidia yoyote (rejea wale waliohamishwa awali kwa kupewa viwanja mabwepande)
Pili, fidia ya bonde la Msimbazi imegawanyika kwa aina ya eneo na athari. Kuna wale ambao ardhi/nyumba zao zipo ndani ya eneo la mafuriko muda wote (flood plain). Na kuna ambao wataathirika na shughuli za maboresho (ujenzi wa miundombinu)!
Tatu, wengi kama si wote waliokuwa ndani ya flood plain hawakuwa na vibali vya ujenzi. Na makazi yao yalikuwa yanatumika kwa msimu wa kiangazi tu! Na yalihabomoka kitambo!
Nne, fidia kwa watu waliokuwa na ardhi/nyumba kwenye flood plain ndiyo flat rate. Fidia kwa watu ambao ardhi/nyumba zao zimefuatwa na athari za shughuli za mradi zenyewe Zina formula yao tofauti.
Tano, fidia Ina formula zake. Na World Bank waliangalia hadi usumbufu na gharama kadhaa wa kadhaa... Hivyo grand total kwa PAP inaweza kuzidi 4M!
Sita, kwamba imetangazwa 4M hizo ni namba tu kwa ajili ya media... Fidia ina mambo mengi inabidi PAP walindwe... Na mbinu mojawapo ni hiyo!
 
Ni World Bank ndo imeamua kutoa kifuta jasho walahu kuwasitiri...!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…