Awamu ziko kwenye katiba ya nchi na zinafuata mpangilio wa miaka ya uchaguzi. Uchaguzi una lengo la kumchagua Rais ambaye akiisha kuchaguliwa ana mandate ya kutawala kwa kipindi cha miaka kumi kinachogawanyika katika vipindi viwili vya miaka mitano mitano.
Baada ya Nyerere kutangaza kung'atuka alipendekeza Mzee Mwinyi kuwa mrithi wake na hivyo kutawala awamu ya pili iliyoanza 1985-1995 mwaka 1990 alichaguliwa kuendelea na kipindi chake cha pili.
Awamu ya tatu, Ilikuwa ya Ben Mkapa 1995-2005 akichaguliwa tena mwaka 2000 kwa kipindi chake cha pili.
Kikwete ndie aliyemfuata Mkapa kuanzia 2005-2015, kumbuka 2010 akichaguliwa kuhudumu kipindi chake cha pili.
Baada ya Kikwete alifuata Magufuli 2015-2015 ambaye alihudumu kipindi chake kimoja hadi 2020.
Pamoja na kuchaguliwa kuhudumu kipindi chake cha mwisho ambacho kinaishia 2025 October, alifariki tarehe isiyojulikana ya mwezi March na hivyo Samia aliyekuwa makamo wake kutawazwa kama Rais wa sita wa JMT akimalizia awamu ya Rais wa tano. . . Hii bado ni awamu ya tano kipindi cha pili kinamaliziwa na Rais wa sita aliyekuwa makamo wake!.