Wanaopinga kuanzishwa mkoa wa Chato hawana hoja

Wanaopinga kuanzishwa mkoa wa Chato hawana hoja

MenukaJr

Member
Joined
Apr 24, 2021
Posts
50
Reaction score
128
Hoja kama NNE hivi zinatumiwa na watu wenye kupinga Chato kufanywa Mkoa. Bahati mbaya kwao, HOJA zote ni dhaifu. Kwa sababu hiyo, Chato isipokuwa Mkoa ni kwa sababu mwenye mamlaka (Rais) hapendi kuifanya kuwa Mkoa sio kwa sababu haina sifa. Chato ina sifa za kuwa Mikoa miwili sio mmoja.

Hoja zinazotumiwa kupinga Chato kuwa Mkoa na udhaifu wake;

1. Historia
Wanasema kwamba ramani inaonesha Chato ni sehemu ya Wilaya ya Bihalamulo Mkoa wa Kagera. Nadhani hapa wanajaribu kuonesha kwamba Chato haipaswi kuwa Mkoa wa kujitegemea nje ya Kagera. Ni bahati mbaya sana kwamba hizi ni fikra za Profesa. Kama watu hawa na historia zao wangesikilizwa tangu zamani, leo tusingalikua na Mikoa 31 kwa sababu tulianza na Mikoa 15 hivyo Mikoa mingine 16 imetokana na hiyo 15. Ni lazima Mikoa ya asili ikubali kuzaa Mikoa mingine ili nchi ichangamke. Hizi ni fikra potofu, dhaifu za kizamani. Historia haiwezi kutumika kama kingo za maendeleo badala yake historia itusaidie kuendelea sio kusimama tulipo, kutengeneza Mkoa ni maendeleo!! Hii hoja ya historia haipo, inakufa.

2. Udogo wa eneo
Sababu hii pia haipo, haina maana yoyote. Katika sababu na vigezo vya kuanzisha mamlaka za Serikali za Mitaa kigezo cha ukubwa au umbali wa eneo hakipo. Chato ikiwa na watu 300,000 na ukubwa wa Kilomita za mraba 10,000 halafu Tabora ikawa na watu 200,000 kwa kilomita za mraba 76,000 bado Chato itafaa kuwa Mkoa kuliko Tabora. Wenye hoja hii sijui wanaipata wapi, vigezo vikubwa katika kuanzisha Mikoa ni shughuli za uchumi na idadi ya watu. Zingine ni huduma za kijamii, basi. Hakuna kigezo cha ukubwa wa eneo wala urefu. Chato inaweza isichukue hata hizo Wilaya 1 Kigoma na 2 Kagera na bado ikastahili kuwa Mkoa kwa sababu ina idadi ya watu wenye kukidhi mahitaji. Kuzisogeza Wilaya hizo za Kagera na Kigoma ni kujali zaidi watu, kuwasogezea karibu huduma. Sababu hii ya ukubwa wa eneo haina maana yoyote, inakufa kabisa.

2. Ukabila
Ukisoma maoni yao au kuwasikiliza kwa makini wenye kupinga hoja ya Chato kuwa Mkoa japo hawasemi lakini wanasukumwa na Ukabila (ubinafsi). Wote ni watu wa Mkoa wa Kagera, wote wanasema historia ya Kagera itapotea ikiwa Wilaya za Bihalamulo na Ngara zitapelekwa Chato. Wanachosema hapo ni kwamba kuchukua Wilaya za Kagera ni kuvunja historia ya watu wa Kagera. Huu ndio ukabila wenyewe!! Hii ni sababu ya hovyo sana, sababu ya kibinafsi, kibaguzi na ni hatari kwa ustawi wa nchi ikiwa itaachwa iendelee. Tulianzisha Mikoa kama replacement ya tawala za ki-chief ili kuvunja Ukabila halafu watu wa Kagera wanaleta ukabila katika karne hii, tunapaswa kuwaonya.

3. Gharama za Uendeshaji
Wanasema ni gharama kuendesha Mkoa karibu na Mikoa mingine, Mkoa mdogo usio na sababu ya kuwepo. Wanasema wananchi watabebeshwa mzigo mkubwa kuhudumia isivyo na maana yoyote. Unaweza kujiuliza kama watu hawa wanaishi nchi hii. Huu ni uongo tu, Tanzania haijawahi kuwa na tatizo la gharama za kuendesha mamlaka zake. Tunahudumia ofisi za Wakuu wa Wilaya nchi nzima wasio na kazi, Wakuu wa Mikoa nchi nzima wasio na kazi, Mawaziri wasio na kazi yoyote.

Kwa vyovyote Mkoa wa Chato sio lolote katika gharama. Hii haiwezi kuwa hoja ya msingi kuzuia Chato kuanzishwa. Kwa kawaida kila jambo lina faida na hasara zake, Mkoa wa Chato utakua na faida na hasara zake. Kinachoitwa gharama ni fursa ya ajira kwa watu wetu. Kwa lugha nyingine hizo ndizo njia ambazo nchi yetu hutengenezea ajira zake. Kwa kuanzisha Mkoa wa Chato, tutaanzisha Idara zote za wataalam katika kada zote. Kuanzia elimu, afya, jamii hadi Polisi. Kwa kufanya hivyo tutapata nafasi ya kuajiri watu wetu, nchi yetu haina namna nyingine ya kutengeneza ajira zaidi ya hizo. Tunataka ajira halafu tunaogopa gharama za kutengeneza ajira, haiwezekani.

Kwa kifupi hakuna HOJA ya maana ya kuizuia Chato kuwa Mkoa. Ni watu wenye chuki na ukabila tu ndio wanaweza kupinga hoja hiyo. Wenye kuipinga hoja hiyo kwa sababu ni ahadi ya Rais Magufuli wanakosea pia. Hayati John Pombe Magufuli aliahidi na kutekeleza mambo mengi, aliahidi Barabara ya Morroco Dar, ikajengwa. Aliahidi Hospital ya Rufaa Dodoma (Uhuru) nje ya Ilani ikajengwa. Aliahidi Msikiti Mkubwa Dodoma na Uwanja wa Mpira vinajengwa.

Aliahidi vingi vingine vilikamilika vingine bado na vitakamilishwa. Ahadi zote hizo ni pamoja na Chato kuwa Mkoa, ni lazima tukamilishe ahadi za Rais. Rais akiahidi Urais umeahidi hata akifa ahadi inabaki Ikulu, Urais ni mamlaka sio mtu.Tuache longolongo tutekeleze ahadi Chato ni zaidi ya Mkoa mmoja.

#TutakuenziDaimaJPM.
MenukaJr .
Da'slama.
 
images.jpg
mtajijua wennyewe ..
 
Uhoja, ni upendeleo, na maslahi ya wachache kwa manufaa ya wachache. Ikiwa hatani mgawanyo wa kieneo Kama sii ukanda au vinginevyo.
 
Hawana hoja ya msingi kwa sababu hakuna anayefahamu vigezo gani vinatumika kulifanya eneo mkoa.
 
Tofauti na hizo sababu alizoziita za longolongo na kuziponda, na wewe si ushuke na sababu zako za utetezi basi ili tulinganishe.

Ikiwa sababu za kuanzisha mkoa wa Chato hakuna,wewe unataka nishuke na sababu ambazo hakuna. Nitakuwa mwehu kama si kichaa.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Chato kama Chato haipo Sawa ni upendeleo wa kijinga kama itapewa hadhi hiyo.

Maendeleo yapi ya watu laki mbili wanaotaka kulishwa eti Njemba yao ilizaliwa pale au kahamia pale.

Basi tuanzie Butiama kwa Mwalimu Nyerere. Harafu labda tuende Lupaso kwa Mkapa.
Magufuli .
 
Hahahahaaaa! Nimecheka hadi basi tena! Ni mama yetu Huyo, yule wa milioni kumi ya mboga. Kweli hii nchi imechezewa sana. Lkn kwa hili suala LA CHATO angebaki kimya ili kulinda heshima yake.
Kabisa aisee.
Wanachomfanyia hayati sio sawa kabisaa..
 
Back
Top Bottom