Wanaopinga ndoa wana matatizo au wamekulia kwenye familia zenye mgogoro

Wanaopinga ndoa wana matatizo au wamekulia kwenye familia zenye mgogoro

Silazimishi mtu kuoa au kuolewa, lakini jambo hili ni jema sana na la kheri
 
Kumekuwa na mijadala mingi sana inayowazuia vijana kuoa au kuolewa, kubwa sana ni kukataa kuoa. Hiyo ni kutokana na mfumo wa maisha ya sasa yalivyo. Ndoa nyingi hazidumu na uaminifu ndani ya ndoa umepungua sana kiasi kwamba wanandoa kusalitiana limekuwa jambo la kawaida na ndio sababu ya ndoa nyingi kuvunjika.

Pamoja na yote hayo haipaswi kuwepo na mjadala wa kuhamasishana watu wasioe/kuolewa au wasiingie kwenye ndoa. Katika hilo kuna watu wanaingia mkenge kwa kufata mkumbo au kumuiga mtu fulani kwa kuwa hataki kuoa/kuolewa nami sioi/siolewi. Hiyo sio poa kabisa kwa sababu watu wanatofautiana na kila mtu ana changamoto zake, changamoto za mke wa fulani haziwezi kuwa sawa na changamoto za mke wa fulani au za mume wa fulani haziwezi kuwa sawa na mume wa fulani. Halafu wengi wanaokataa kuoa/kuolewa wana changamoto za kisaikolojia ambazo wamezipata either kwa kushuhudia au kusimuliwa.

Kwahiyo nawaomba vijana ambao hamjaoa au kuolewa msiogope kuingia kwenye ndoa. Usiangalie na kulinganisha na ndoa ya fulani kwani ndoa yako haiwezi kufanana na hao wengine.

Kubali Ndoa
Ndoa ni Baraka
Ndoa ni Furaha
Ndoa ni Heshima
Hawa wanaopingaga ndoa ukiangalia Historia zao zina shida sana
 
Wengi wao ni

Wazazi wao walikwepa majukumu ya malezi bora eg Mume kuendekeza michepuko na kusahau familia,Mke kuwekeza kumlisha limbwata Mume na kusahau kujaza upendo kwa watoto

Watoto waliotelekezwa kwa ndugu

Watoto wa michepuko

Mimba zisizo tarajiwa kisha zikakanwa

Waliopatikana kwa matokeo ya ubakaji. Mabazazi yanayobaka yalaaniwe yanatuharibia jamii

Waliokacha shule na kukimbilia kuvuta vijiweni,dating za kipuuzi,kula kimasihara

Waliopatikana vilabu vya matapu tapu

etc etc etc
Umepita mulemule😀
 
ukishakuwa na watoto kusema kweli hakuna haja ya ndoa, unakomaa na kutafuta hela , kulea watoto wako vizuri na kuenjoy maisha
Well said, lakini kuishi na watoto pamoja ni vizuri zaidi. Imagine umemzalisha dada halafu humuoi hapo itabidi umchukue mtoto uishi nae, kama hutamchukua ataenda kulelewa na baba wa kambo au utampeleka kwa ndugu zako akalelewe huko. Huoni kama hilo ni tatizo mtoto kulelewa na mzazi mmoja?
 
Ndoa ni upumbav fulani hivi wa maisha... Sijui mnakimbilia wapi kuoa vijana... 90% ya watu walio ktk ndoa wanaish kwa stress na majuto... Stay single ukishindwa vuta mwanamke/mwanaume wako utakaye ishi naye temporary, zaa nae ikitokea akili zenu zimeendana endeleeni kuishi, ikitokea akili haziendani piganeni chini
 
Back
Top Bottom