GE2025 Wanaopinga uteuzi wa Samia wataje wagombea wao ili tumpime

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Baba yako aliuza ng'ombe wake kukusomesha kumbe kauza ng'ombe kusomesha ng'ombe
Baba yangu alikuwa mshauri wa Waziri wa kilimo pale wizarani Pamba House kuanzia miaka ya 70 mwishoni mpaka alipostaafu mwaka 1995, sisi watoto wake tumesoma forodhani primary na sekondari za Dar miaka hiyo ya 80.

Ng'ombe ni wewe ambaye unakosa hoja unajawa na mapovu kichwani.
 
Tatizo lingine ndo ilo Mwenyekiti wa chama kua Amirijeshi ili pia ni tatizo
Mzee Nyerere na wenzake ndivyo waliona iwe hivyo, na huenda hiyo ndiyo iliyotuvusha na kuwa kitovu cha amani kwenye ukanda wa maziwa makuu.

Tumshukuru Mungu Rais Samia yuko kimya, na naomba awe kimya hivyohivyo kwakuwa kuna watu hawajui walitandalo. Mama ana nia safi, moyo safi, sio mwizi, hana makundi na ni mpenda sifa za kweli alizozifanyia kazi.

"If, inside, you possess good qualities, such as compassion or spiritual forgiveness.... then external factors will not affect the internal peace of the mind", DALAI LAMA.
 
Ndiyo maana uzalishaji wa pamba ulishuka na kilimo kilionekana kama adhabu na laana.
 
Hatuna wagombea mifukoni mkuuu ,tutangaze tuweke wazi ,watu watangaze nia wafate utaratibuuu ndio hapo tutakuwa nao wakisha chukua fomuuu
 
Watu wanapinga mchakato. Hata akipitishwa Samia huyo huyo lakini utaratibu ufuatwe. Hatujadili wagombea, tunajadili mchakato ndio uliokiukwa.
Samia anatosha, fedha za kuitisha mkutano mkuu mwingine zitumike kuwaongezea askari mishahara yao. Kuna maandazi mmoja analalamika kuwa askari tu wanalipwa kidogo visivyostahili, lakini anataka itumike pesa nyingine kuitisha mkutano mwingine Mkuu ili kuja kutoa matokeo yaleyale ya mkutano mkuu uliopita; hii ni kuonyesha kuwa kuna watu hamnazo kabisa.
 
Hv kama utamaduni wao ni rais kuongoza miaka 10, kwann wanaweka mchakato wa kupigiana kura wakati tayari utaratibu wanaujua?
Kama huo ndio utaratibu wao basi Samia kishaongoza kwa miaka kumi; mitano akiwa na Magufuli na mitano mwenyewe!
Kutaka kuendelea ni uroho wa madaraka na ndio maan anatumia nguvu nyingi kupindisha taratibu za ccm za kumpata mgombea!!
Yeye Kisha maliza ngwe yake awapishe wengine waoneshe uwezo wao!
Kikwete ni mnafiki sio wa kumsikiliza ,Yeye alipoteuliwa kugombea walishindana watatu ; yeye, Salim Ahmed Salim na professor Mark James Mwandosya. Magufuli alipoteuliwa pia wagombea walikuwa watatu akiwemo Asha Rose Migiro na Amina Salum Alli!
Sio tu Samia doesn’t qualify but why does she want to abuse well established processes?
Kikwete should be sidelined from the top level ccm decision making bodies because he has hidden agendas that are not to the interests of the party and country. He is a selfish retiree, he should be shunned.
 
Kama ni hivyo wasiompenda wamkatae Samia kwenye sanduku la kura. Ila Tume ya Uchaguzi nayo ndiyo hivyo tena!!!
"Sanduku la kura"?
Mbona huko ndiko tayari kishajianddaa kuachafua!
Wakiruhusu afike huko kwenye sanduku la kura, maana yake tayari kishakuwa mshindi mara tu baada ya haya yanayomkabili sasa yatakapo kwisha.
 
Watu hawampingi Moja Kwa moja kugombea ila wanapinga njia aliyotumia kujipitisha kugombea.Tatizo ndio linaanzia hapo.Kujipitisha Kwa mlango wa nyuma,wakati watu wakisubiri mlango wa mbele🤔
 
Ndiyo maana kilimo kilikufa hiyo miaka....hiyo miaka ndiyo tulikula chakula cha yanga, ugali wa njano na nguru
 
Hatuna wagombea mifukoni mkuuu ,tutangaze tuweke wazi ,watu watangaze nia wafate utaratibuuu ndio hapo tutakuwa nao wakisha chukua fomuuu
Hebu tujikumbushe kidogo huenda tukapata majibu hapa:

Baada ya kifo cha Rais Magufuli (RIP) Spika aliwaita wabunge kwenda Dodoma (bungeni) kwa mkutano wa dharura. Je, mkutano huu ulikuwa ni wanini ili kujadili ninii? Je, mkutano huu ulifanyika? kama ulifanyika walijadili nini? kama haukufanyika ni kwanini?. je, mkutano huu ulikuwa agizo la nani? je ulikuwa na baraka za kikatiba? na Je, Mama Samia alikuwa ameshirikishwa kama makamu wa Rais kuhusu huu mkutano na agenda zake?


View: https://youtu.be/qiraASeojr0?si=QY_i7E8YE0E_s2FI
Sikiliza hofu ya Mama:

View: https://youtu.be/4cyXGvIrLoY?si=bb813llhJ13pR-bj
 
Ananuka ananuka...huyo fara kafanya nini zaidi ya kuabudu waarabu na kufunga makanisa 🙄🙄🙄
 
Ananuka ananuka...huyo fara kafanya nini zaidi ya kuabudu waarabu na kufunga makanisa 🙄🙄🙄
Sijawahi kuona CCM imeshindwa jambo kulikabili. Hapa nawakumbuka akina jecha, G55, Mtema, Oscar Kambona, aboud, Hanga, Lowasa, sumaye, Membe, Idd Amini, wareno, captein komba,, kufuta Tanganyika, kuhamia Dodoma,, nk, hata nyie mtashindwa tu kama wale wengine.
 
Fuateni taratibu tu, kwani hizi sarakasi zote ni za kitu gani?

Kuna kitu mnakiogopa na mgombea wenu?
Watu wanaokula sana ugali wa mahindi ubongo wao haujachangamka, slow learners wengi wanataka kundi hili.. Rais wa CCM lazima aongoze miaka 10 labda afe mwenyewe. Na Samia is not exceptional. Wanataka ndiyo hivyo hawataki ndiyo hivyo
 
Watu wanaokula sana ugali wa mahindi ubongo wao haujachangamka, slow learners wengi wanataka kundi hili.. Rais wa CCM lazima aongoze miaka 10 labda afe mwenyewe. Na Samia is not exceptional.
Kabla ya yote, nikudharau juu ya hayo ya "ugali wa mahindi", kwa sababu wewe huna ujuzi wowote juu ya hilo; kwa hiyo haya mengine yote unayoweka huku kwingine ni takataka tu zile zile. Huu ni utaratibu, au jadi ambayo watu wa aina yako, na hasa huyu Samia Suluhu Hassan, na GENGE lake, wanajitahidi sana ndiyo iwe jadi/taratibu za taifa hili; ulaghai kila jambo; uongo na maovu chungu nzima

Sasa taarifa kwako ni kuwa, haya ndiyo hatutaki muyaeneze ndani ya nchi hii. Yawe ndio mambo ya kawaida.
Taifa hili lina heshima kubwa sana, msitake kuivunja heshima hiyo.
 
Je kushindana na wananchi na ccm wazalendo itaweza...au ujui kuna ccm wahuni na ccm wazalendo
 
Ndiyo maana kilimo kilikufa hiyo miaka....hiyo miaka ndiyo tulikula chakula cha yanga, ugali wa njano na nguru
Vyuo vingi vya kilimo mzee wangu alisimamia uanzishwaji wake, kula ugali wa yanga ilitokana na nchi kuwa imetoka vitani hazina haikuwa na pesa kabisa.

Umaskini ulitamalaki kila kona. Mzee Mwinyi alipoingia ikulu akakubaliana na masharti ya IMF.
 
Ndiyo maana nasema ugali wa mahindi usiwalishe watoto wako sana, vinginevyo watakuwa kama wewe. Utafiti ulifanyika kujua kwanini wayahudi wana uwezo mkubwa wa kufikiri, ndipo wakabaini kuwa wao wanatumia nafaka ya ngano sana katika forms mbalimbali kama mkate, kande, uji, pombe, nk karibia Kila siku. Nchi nyingine mahindi wanalisha nguruwe tu.

Kwanini unang'ng'ania uteuzi wa mgombea wa CCM tu wakati nchi ni ya vyama vingi? Kama CCM wameteua mgombea dhaifu hiyo ni faida kwa vyama vingine ambao watateua wagombea madhubuti watakaomshinda Samia mchana kweupe na taifa litapata Rais bora kuliko Samia. Shida Iko wapi hiyo? Mwl Nyerere alisema kama CCM itateua mgombea dhaifu wananchi watamtafuta Rais bora njje ya CCM. Kwanini unalazimisha lazima CCM ichague mgombea bora kama vile lazima Rais atoke CCM.

Ndiyo maana nasema ugali wa mahindi una walakini kama ukiutumia sana, slow learners wengi wanataka huko.
 
Vyuo vingi vya kilimo mzee wangu alisimamia uanzishwaji wake, kula ugali wa yanga ilitokana na nchi kuwa imetoka vitani hazina haikuwa na pesa kabisa.

Umaskini ulitamalaki kila kona. Mzee Mwinyi alipoingia ikulu akakubaliana na masharti ya IMF.
Mzee wako ameua kilimo, hadi Leo nchi inaagiza mafuta ya kupikia, na wakulima wanatumia kajembe ka mkono hadi Leo. Bashe ndo kigooooogo ana afadhali.
 
Mzee wako ameua kilimo, hadi Leo nchi inaagiza mafuta ya kupikia, na wakulima wanatumia kajembe ka mkono hadi Leo. Bashe ndo kigooooogo ana afadhali.
Mzee wangu hajaua kilimo, inabidi uelewe masuala mengi ya kitaifa ili uweze kujua kwanini jembe la mkono lilidumu kwa miaka mingi baada ya uhuru.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…