hapo ulipo unajivimbisha kwa sababu ya silaha za waTanzania. Tutakunyang'anya hizi silaha tuone kama utaendelea kujivimbisha.Hebu anza wewe kupoteza woga wako tuone. Umevimbiwa na kiporo cha ugali wa mahindi wewe. Tumia hizo nguvu kuchimba majaruba upande mpunga ili upunguze kula mahindi
Mawazo ya aina hii ndiyo alama ilio wazi kujuwa wewe ni mtu wa aina gani; na nikatika fikra hizo hizo Samia na nyinyi wote mnajigeuza kuwa ni watu bora kuzidi wengine.Unajua wewe kwani wazungu, wachina, wahindi, waarabu hawali ugali wa mahindi? Unadhani hawajui kwamba mahindi ni chakula? Uwezo wao wa kufikiri unauonaje? Hapa Tanganyika ni makabila gani chakula chao kikuu sio ugali wa mahindi? maendeleo yao yakoje?
Sasa tambua kwamba kukikweza kwenu huko hakutawasaidia tena.
Mnauza raslimali zote za waTanzania, hata bandari mnaona hawana uwezo wa kuiendesha?
Kila kitu mnataka hao uliowataja hapo ndio waje kuzitumia kwa faida yao mkijidanganya kuwa ndiyo kuendelea kwa waTanzania!
Mentality za kitumwa hizo hapa tulizikataa tokea 1961, nyinyi mnaturudisha huko.
WaTanzania hawawezi kuwa watwana tena hata mara moja.