GE2025 Wanaopinga uteuzi wa Samia wataje wagombea wao ili tumpime

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kwann Mnaolalamika ni Wapinzani wa CCM??? Wenye CCM yao Wamekubaliana kila kitu kimeenda sawaa
wamekubaliana? alafu nkuulize swali? kama mtu hayupo ccm au vyama vingine, anakuaje mpinzani? yan ccm yeyote atakae sema ukweli ni mpinzani? haya mzee yule wa moshi kaja tena na vifungu vya sheria vilivyovunjwa. Anyways unadhani hizi query zote zinazoraise ni kawaida tu?....haya tuyaache haya yote. Wanachosema hawa watu ni kweli?...kama ni uongo kipingeni kwa hoja.
 
Fuateni taratibu tu, kwani hizi sarakasi zote ni za kitu gani?

Kuna kitu mnakiogopa na mgombea wenu?
Eti huyu Mzee Malisa anasema uteuzi umevunja Katiba ya Jamhuri kwakuwa Katiba inasema shughuli za uchaguzi zinaanza baada ya bunge kuvunjwa. Na hii ni hoja yenye maana jamani?
.
Taratibu za ndani ya vyama vya siasa na katiba ya nchi ni wapi na wapi?

Kwani vyama vya siasa kama chadema au ACT wanakatazwa kumtangaza mgombea wao wakati wowote hata ikiwa ni December au January miezi 12 kabla ya uchaguzi? Wakifanya hivyo watakuwa wamevunja katiba ya jamhuri?
 
Huyo mgombea wa CCM alichukua fomu lini, wapi, aliirudisha lini?. Alipata wadhamini wangapi?. Mkoani Dar, Mwanza, Arusha, alipata wdhamini wangapi?
 
Sema Mama angepigiwa kura pia angeshinda tu huko ingawaje kelele ni nyingi ila nageshinda tu..
 
Hv kama utamaduni wao ni rais kuongoza miaka 10, kwann wanaweka mchakato wa kupigiana kura wakati tayari utaratibu wanaujua?
Hilo ni takwa la kikatiba kila baada ya miaka mitano kuwepo na chaguzi na katiba ya ccm pia inasema hivyo ila waliwekeana utamaduni awe aliepo madarakani kama ameongoza mitano ila sasaivi wanataka katiba yao ifuatwe sasa hapo aliepo madarakani asitumie dhamana ya kofia alizonazo kutaka awe yeye tu
 
Kila zama na kitabu chake sawa.

Lakini kitabu cha wakati huu kimekiukwa.
Mahakama ya rufaa ya vyama vya siasa ni Mkutano wao Mkuu. Mkutano Mkuu uko juu ya kanuni, tamaduni na taratibu zooooooote ndani ya vyama. Kama wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama wamesema ndiyoooooooooo wewe ni nani kama sio kujitafutia shida wewe mwenyewe?

Watu kama hawa Mwl Nyerere hakusita kuwaita watu malayamalaya wanaowatumikia watu wasioonekana kwenye kamera. Watu kama hawa wakati wa Nyerere wangeshaikimbia nchi au kuwekwa kwenye kifungo cha nyumbani kwao, Hawana hoja ni kelele tu za huyoo, huyooo, mchinjeee mchinjeeee.

Watu hawa wanatupotezea focus (nuisance) ya kufanya shughuli za maendeleo ya nchi yetu huku wakijua kuwa hawana hoja inayoweza kuzikilizwa ndani na nje ya nchi. Sasa hivi dunia yote ime concentrate na sarakasi za Trump, Ukraine, Gaza, Iran, DRC. Wasidhani kuwa kuna watu wa maana sana wanaowasikiliza. Mabalozi wa nchi nyingine wako hapa hapa na wana akili nyingi za kutofautisha na kufananisha kati ya Magufuli na Samia.
 
Wacha uongo. Salim Ahmed Salim alifanyiwa hujuma gani; hujui?

Lakini pamoja na kujisahaulisha hayo, ninakushukuru sana kwa kuweka hiyo video ya huyo mwananchi. Kama ndani ya nchi hii bado wamo wananchi wa aina hii, kwa nini tuwe na hofu hivi?
Nyerere alikuwa muumini mkubwa wa Muungano. Salim hakuungwa mkono na wajumbe wa zanzibar tena waziwazi bila woga kwenye vikao. Samia aliungwa mkono na wajumbe wengi kama sio woooote wa Mkutano Mkuu kutoka Bara na visiwani. Wewe ni mkubwa kuliko Mkutano Mkuu wa chama? yaani wajumbe wooote hao ni matahilla ispokuwa wewe?

Collective responsibility must be observed, otherwise hawa ni "maaalayamalaya tu"
 
Miaka 6 akiwa makamu na miaka 4 akiwa raisi uoni hio ni 10 tayari na awamu kabisa, au akiwa makamu hio sio awamu?
Unasoma Katiba ya nchi gani inayosema hivyo? Umesoma wapi katiba inasema makamu wa Rais mwisho wake ni miaka 10 na hawezi kuwa Rais. Nyie mnataka kuvunja Katiba sasa.
 
Nmeandika utaratibu wao hapo afu tena unaniuliza Wana utaratibu gani 🗑️


Bro, unajielewa?

Sasa kuwa makamu na kuwa rais kuna ingiliana vp?
Bc na mtu akiwa Waziri afu akija kuwa rais nae miaka yake ihesabike kama ulivyosema hapo.
Kama akili ndio hizo HATA akiwa mbunge asigombee urais tena.
 
Mental health 101: Keep a distance from people who worship religious & political figures. They tend to be more emotional than logical
 
kwanini Taratibu zimevunjwa? kwa Maslai ya Nani?....
Membe wakati anafukuzwa uwanachama kwa kung'ang'ania kugombea ilikuwa kwa maslahi ya nani?

Oscar Kambona wakati anafukuzwa kwa kupinga ujamaa na Azimio la Arusha ilikuwa kwa maslahi ya nani?

Wakati Kikwete alipoambiwa ampishe Mkapa yeye bado ni kijana ilikuwa kwa maslahi ya nani?

Wakati Bilali aliyeongoza kura za maoni kuachwa na kuchaguliwa Abeid Amani Karume kuwa Rais kule Zanzibar ilikuwa kwa maslahi ya nani?
 
Kwa maelezo haya fuateni utaratibu basi, maana hapo hakuna utaratibu uliofuatwa. Miaka kumi unamuhesabia vipi samia, minne kamaliza unamtafutia 6? Au unamtafutia 10 aanze kuitumikia?...tuelewe she nasi tupate elimu Yako kidogo
 
Kwa ccm hakuna mgombea yeyote ANAYEFAA....WOTE WABOVU...si udiwani,si ubunge,wala urais ,wote hawafai.
 
Nmeandika utaratibu wao hapo afu tena unaniuliza Wana utaratibu gani 🗑️


Bro, unajielewa?

Sasa kuwa makamu na kuwa rais kuna ingiliana vp?
Bc na mtu akiwa Waziri afu akija kuwa rais nae miaka yake ihesabike kama ulivyosema hapo.
Hivi kumbe huna akili? Makamu wa Raisi ni Raisi, anatekeleza majukumu ya Raisi, ana anahudumiwa vile Raisi anavyohudumiwa, anakaa ikulu, na anachukua full control Raisi anapokuwa hayupo,anaumwa au amekufa kama ilivyo sasa, kwahiyo kwa kifupi muda wake wa miaka 10 umeisha, Raisi sio waziri, waziri anateuliwa na Raisi, ila Raisi anachaguliwa, huyo ameshachaguliwa mara mbili katika nafasi hiyo hiyo ya uraisi
 
Kwa maelezo haya fuateni utaratibu basi, maana hapo hakuna utaratibu uliofuatwa. Miaka kumi unamuhesabia vipi samia, minne kamaliza unamtafutia 6? Au unamtafutia 10 aanze kuitumikia?...tuelewe she nasi tupate elimu Yako kidogo
Huyo ameshamaliza miaka yake 10 kwenye kiti cha uraisi hakuna alichobakiza zaidi labda tamaa tu, awaachie wengine taifa letu sote
 
Kimekiukwa wapi? Tangu lini na wewe umeanza kuwa nyumbu wa kudandia agenda za kupita!
Kwanini mlazimisha awe mgombea pekee, badala ya watatu kama ilivyo utaratibu? muwekeeni wengine wawili hapo ili wawe watatu wajumbe wapige kura wanayemtaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…