GE2025 Wanaopinga uteuzi wa Samia wataje wagombea wao ili tumpime

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Wacha uongo. Salim Ahmed Salim alifanyiwa hujuma gani; hujui?

Lakini pamoja na kujisahaulisha hayo, ninakushukuru sana kwa kuweka hiyo video ya huyo mwananchi. Kama ndani ya nchi hii bado wamo wananchi wa aina hii, kwa nini tuwe na hofu hivi?
Membe alikuwa wazi kuwa alitaka kugombea dhidi ya Magufuli kwenye uchaguzi wa 2020. Tena alitangaza nia yake hiyo mapema hata kabla ya wakati wa kuchukua form haujaanza, kila mtu alikuwa anaijua dhamira yake hiyo na watu walianza kuzijadili sifa za Membe vs Magufuli. Hawa ma ghost wa safari hii wanapiga kelele tu kuwa Samia hafai lakini wao wanaodhani wanafaa hawajitokezi hadharani kwanini? Wakifanya hivyo huwenda wakawashawishi watu wengi kutokana na sifa za mgombea wao.
 
Kwanini mlazimisha awe mgombea pekee, badala ya watatu kama ilivyo utaratibu? muwekeeni wengine wawili hapo ili wawe watatu wajumbe wapige kura wanayemtaka
Kwani hao wajumbe hawakuwepo kwenye ule mkutano? Si walipigwa kura na alishinda kwa 98-98, sasa hao wajumbe asilimia moja wataathiri nini?
 
Kwani hao wajumbe hawakuwepo kwenye ule mkutano? Si walipigwa kura na alishinda kwa 98-98, sasa hao wajumbe asilimia moja wataathiri nini?
Ushasikia wapi kura zinapigwa ikiwa mpigiwa kura yuko hapo hapo, halafu kukawa na uhuru hapo, si unaona wajumbe walitaka atoke nje akagoma?
 
vifungu vya yule mzee labda vya kwenye chama ndo viko sawa
 
Ushasikia wapi kura zinapigwa ikiwa mpigiwa kura yuko hapo hapo, halafu kukawa na uhuru hapo, si unaona wajumbe walitaka atoke nje akagoma?
Kama unayo hoja na unadhani ni hoja yenye manufaa kwa taifa na chama unaitoa tu hata kama nani yuko ndani ya mkutano au la. Ukiona mtu anaogopa kutoa hoja yake ujue kuwa hiyo hoja haiko sawasawa; ni majungu au hisia zake tu.

Siasa ni mkakati unaotumia mbinu mbalimbali. Usalama wa taifa upo kwaajili ya kumpatia taarifa Amirijeshi Mkuu wa majeshi na Mkuu wa nchi. Bila shaka kulikuwa na taarifa ya uwepo wa wakora ndani ya mkutano.
 
Mchakato wa wapambe kumtaja samia mgombea pekee ulilenga kumwondolea aibu ya kushindwa wakipambanishwa. Hana uwezo wa kupita hata mbele ya mgombea dhaifu yeyote atakae wekwa.
 
Kama unayo hoja na unadhani ni hoja yenye manufaa kwa taifa na chama unaitoa tu hata kama nani yuko ndani ya mkutano au la. Ukiona mtu anaogopa kutoa hoja yake ujue kuwa hiyo hoja haiko sawasawa; ni majungu au hisia zake tu.
Watu mbele ya boss hawawezi kuwa huru kumjadili. Aligoma kutoka alijua Kikwete na kundi lake (nae akiwemo) wataumbuka.
 
Rais Samia atosha,tunae na tutazidi kuwa nae kimwili na kiroho.
Mimi nakumbuka kulikuwepo na watu ambao hawakukemewa ambao walitaka Katiba abadilishwe kifungu cha ukomo wa Rais ili Magufuli aongozewe muda wa urais kwa kipindi kisichojulkana kwa kigezo kuwa aachwe amalizie miradi yake ambayo alianzisha kana kwamba kama ataondoka miradi haitakamilika. Samia amewaprove wrong wale wale wahuni waliokuwa na wasiwasi hiyo. Miradi yote imekamilika in time.
 
Watanzania tunao umahiri wa kutumiwa na wenye mamlaka huku mitandaoni. Mada nyingi wahusika wakuu wanakaa nyuma na wanaachia machawa wao kazi ya kupayuka humu JF na kule instagram.

Matusi yanaelekezwa kwa hao chawa wao wakati wenyewe wametulia sehemu wakinywa juice za makopo huku wakipulizwa na upepo mwanana.

Huu ni wakati wa kuujadili mpango mkakati wa serikali wa miaka 25 ijayo yaani mpaka 2050 huko yapo mengi yenye kustahili mijadala halisi yenye kugusa maisha yetu moja kwa moja.

Hayo ni ya msingi zaidi kuliko majina ya wanaoteuliwa na siasa za haiba za viongozi, ni sawa na udaku kuendekeza kunyooshea vidole watu badala ya kujikita kwenye kuutazama muelekeo mzima wa TZ.
 
wataenda kuchukua fomu watapimwa mwenye uwezo atashinda
tukutajie hapa ili iwe nini? rais anapatikana jamii forums?
 
Mchakato wa wapambe kumtaja samia mgombea pekee ulilenga kumwondolea aibu ya kushindwa wakipambanishwa. Hana uwezo wa kupita hata mbele ya mgombea dhaifu yeyote atakae wekwa.
Kwani Nyerere alipokuwa anapigiwa kura ya ndiyo au hapana hofu yao ilikuwa nini?
Kwanini Kamilus Membe hakupewa formu ya kugombea urais, waliomnyima fomu Membe walikuwa wanahofia nini?

Hamna hoja.
 
Unaweza kutoa hoja kama hii kama ama IQ yako iko chini sana au umekula hela za watu ili kufanukisha jambo na unaona unaona unashindwa kufanikisha.
 
Issue ni ameikanyaga, ameidharau na kuinajisi katiba ya CCM na katiba ya Tanzania. Usihamishe magoli. Watajitokeza wengine na kushindanishwa.

Amedharau wana-CCM na Watanzania wote kwa kujipitisha kibabe bila kufuata katiba zote mbii, taratibu, misingi, tamaduni. Kazi ya kwanza ya Rais ni kufuata na kuilinda katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tannzania.

Katiba ni makubaliano jinsi tunavyotaka nchi iongozwe. Jinsi tunavyowakabidhi mmoja wetu madaraka makubwa. Alinde mali zetu, maisha yetu, rasilimali zetu, haki zetu. Yeye anafanya kinyume chake.
 
Ndo swali langu linakuja, kwann wapigiane kura wakati wao wnyw wameweka utamaduni wa rais kuongoza miaka 10?
 
T
Tupime nn wakati samia keshajipitisha mwenyewe? Alijaza fomu lini? Alizaminiwa na nani ?
Bila kujibu haya wewe ni CHAWA TU
 
Anawajua ndio maana kawakimbia kwa kutowafuata utaratibu.
 
Kamsikikize polepole itakusaidia kujua taratibu za chama chenu
JPM ndiye anaeharifu kila hoja yenu. Wakati wa JPM nchi na CCM ilikuwa kama vile imepinduliwa, na bahati mbaya Polepole alikuwa mwandamizi wakati wa JPM. Watanzania na dunia bado hawajasahau tabia na matendo ya JPM na serikali yake. Hivyo Samia anaibuka kidedea dhidi ya JPM ndani na kimataifa. Samia aliibuka shujaa pale aliporuhusu vyama vya upinzani kurejeshwa kazini na akina Lissu na Lema kurudi nyumbani. Tukio la Lissu kurejea nyumbani lilifuatiliwa na mataifa mengi, lakini kwa bahati mbaya kumbe kuwa mkimbizi ulaya Magharibi na Marekani kuna faida nyingi kuliko kuwa huru Afrika. Mwalimu wangu alikuwa akisema darasani kuwa "mbwa wa ulaya ana bajeti kubwa kuliko binadamu wa Afrika; hivyo ni heri kuwa mbwa ulaya kuliko kuwa binadamu Afrika:

Lissu na wenzake wako tayari kufanya lolote ili kudumisha status yao ya ukimbizi huko ulaya na Marekani ili waendelee kupata mafao (benefits) za ukimbizi. Ili kufanya hivyo lazima uwathibitishie pasipo shaka kuwa Tanzania sio salama kwao; watu wanatekwa, wanauawa na wanatiwa kizuizini. Yaani huenda hata matukio ya kutekwa watu na kuawa kuna uhusiano mkubwa na hili. Uchunguzi makini lazima ufanyike na taarifa zitolewe.
 
Tatizo mnajibu au kutetea hoja isiyopo Mezani, TUNATAKA UTARATIBU UFUATWE hata kama ni yeye, yaani hii chama kikoswe mgombea !! Yupo riziwani🤣🤣
Nenda mahakani kushitaki wajumbe wa mkutano mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…