Wanaosema kujenga ni kuzika pesa

Wanaosema kujenga ni kuzika pesa

Mimi naongea facts, siongei blah blah.
Nimerithi nyumba na ardhi. Nyumba ni headache na nimekatazwa na ukoo kuiuza.
Nyumba inaleta heshima kwa utamaduni wetu.

Kama heshima kwa jamii ingeweza kuwekwa thamani yake kifedha labda.
Ila huwezi.

Viwanja vina thamani inayokua. Hata by looking at the population increase. Mapori mengi ya miaka 15 iliyopita Sasa ni miji.

Nyumba haiongezeki thamani. Huo ni ukweli wa kimahesabu siyo hadithi njoo .
Huwezi kupigiana hesabu za nyumba ukanipa faida above interest rate ya Benki kuu.

Ukitaka tupigiane mahesabu hapa.
Unaizungumzia nyumba iliyojengwa hewani au kwenye hiyo ardhi unayoisema inaongezeka thamani?
 
Mambo mengine yasikie tu nyuma ya keyboard. Nilinunua viwanja sehemu fulani. Sina mpango wa kujenga kwa sababu ni nje ya mji na majirani hawajajenga bado. Kila mwaka nalipia kodi. Ni upotevu wa pesa zangu. Kama una pesa weka benki ama fanya biashara. mambo ya kununua viwanja eti vitapanda bei ni biashara kichaa.
Mambo mengine ni akili ya biashara tu. Kununua viwanja inategemea na eneo, kama unataka fedha ya haraka usinunue porini sana, Dodoma watu wamepiga fedha sana hadi hata sasa. Ilikuwa kununua maeneo kwa bei rahisi, baadae mtu anapima viwanja na kuuza. Biashara hii ni nzuri kwa yale maeneo mji unapoelekea au maeneo ya kimkakati. Hata biashara ukiiendea vibaya unapigwa vizuri tu.
 
Wanaosema kujenga ni kuzika pesa utawakuta wanatoa mifano ya kina Bakhresa, Mo Dewji hivi kwa akili yako kuna tajiri hana nyumba?

Hivi unasemaje kujenga ni kuzika pesa wakati bei ya nyumba inapanda kila siku? Hivi mtu aliyejenga nyumba Kariakoo miaka ya 1970s kwa shs laki 1 alafu amekuja kuiuza hiyo nyumba mwaka 2021 kwa billioni 5 utamwambiaje kwamba alizika pesa?
Real estate ni biashara kubwa sana tu na imetajirisha watu wengi.

Wana timing zao, mda wa kununua, location za kununua, na namna ya kucheza na mabenki etc.
 
Sehemu yeyote ile.
Hivi kipi cha ajabu hapo?
Ardhi inapanda thamani, nyumba inashuka thamani.
Tumia uwiano mzuri ili ujenge nyumba kwa kutumia ardhi badala ya kutumia ardhi kujenga nyumba.
"Tumia uwiano mzuri ili ujenge nyumba kwa kutumia ardhi badala ya kutumia ardhi kujenga nyumba." Naomba ufafanuzi hapa mkuu.
 
Kuwa halisi haimaanishi kufuata mkumbo.
Katika kipindi hicho cha miaka kumi, badala ya kujenga, nunua viwanja.
Nyumba kama Jengo siyo asset.
Ardhi ni asset.
Nyumba ya milioni 30 utapangisha kwa laki mbili kwa mwezi ambayo ni milioni mbili kwa mwaka (maintanance laki nne ambayo ni ndogo najua).
Itachukua miaka 15 ku break even.
Baada ya hapo utakuwa unachukua mshahara wa laki mbili kwa mwezi.
Buy land, then wait.
Kama nakuelewa hivi.
 
Wanaosema kujenga ni kuzika pesa utawakuta wanatoa mifano ya kina Bakhresa, Mo Dewji hivi kwa akili yako kuna tajiri hana nyumba?

Hivi unasemaje kujenga ni kuzika pesa wakati bei ya nyumba inapanda kila siku? Hivi mtu aliyejenga nyumba Kariakoo miaka ya 1970s kwa shs laki 1 alafu amekuja kuiuza hiyo nyumba mwaka 2021 kwa billioni 5 utamwambiaje kwamba alizika pesa?
Acha uwoga wa maisha wewe, panga, achana na maujenzi.
 
Laki 1 ya mwaka 70 sio laki 1 ya mwaka 2022. Angalia ktu inaitwa "money value" au "purchasing power" ya hela
Harafu mueleze kilichoipa thamani sio nyumba,ni location ya kiwanja . Mwambie achekeche kichwa, anunue viwanja mjini...

Usijenge nyumba kwa mateso, tafuta pesa unaweza kujenga kwa miezi miwili tu. La msingi jitwalie viwanja ,kata hati.
 
Back
Top Bottom